Rais rudi kafikiri upya kuhusu wanafunzi na mimba.

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
5,161
5,404
Juzi limetolewa tamko na mkuu wa mtaa wa Tanzania kuwa mwanafunzi yeyote akibeba mimba huo ndo utakuwa mwisho wake kupata huduma hiyo kwa serikali.
Naweza kusema mkuu hakujipanga kwa sababu hadi sasa serikali inawahudumia wanafunzi chini ya mtaala rasmi wa serikali MEMKWA kutokana na kukosa elimu ama kwa kukosa vifaa, kubebeshwa mimba, matatizo ya kiafya na mengineyo.
Masomo ya memkwa yamegawanyika na programe hiyo inadhaminiwa na serikali na waliozaa na kuacha shule nao wamo wamerudi shule kwa mfumo huo wa memkwa ambapo kuna kundirika karibia mbili na wote wanafundishwa mashuleni hadi sasa shule zao ziko hai.
Napata ukakasi serikali kujipinga yenyewe ktk mambo ambayo tayari imeingia gharama kwa semina na uandaaji wa vitabu kisa tu mimba.
Hii ni hasara kwani mfumo wa kupata elimu nje ya mfumo rasmi unakubalika duniani kote na watu wanasoma na kufaulu. Tutafakari leo hii kama wanaume nao ukimpa mimba mtu na wewe unaibeba yamkini hata watoa matamshi pengine wangeshaachishwa shule na kuishia pabovu.
Tusimkandamize mwanamke kwa sababu tu yeye ndiyo mbebaji wa mimba natamka wazi kuwa mkuu hajatenda sawa kwa tamko lake bila kuwa na mbadala mwingine wa kuwasaidia watoto wa kike .
Shetani akikuzidi nguvu njia rahisi si kuungana naye bali kupambana ili kushinda. Hii ni roho ya ukatili ambayo hufanyiwa watoto wa kike kwa baadhi ya makabila nchini mfano wasukuma, wamasai na wengineo.Ndiyo maana hadi sasa rate ya wanawake wasomi kutoka ktk makabila mengi nchini ni ndogo mno na hivyo kuongeza umaskini.
Ijulikane wazi kuwa huwezi kuwa na maendeleo ama kufanya kazi kwa ufanisi kama nyuma yako huna mke ama wake watulivu na wasomi walioelimika. Ukimuelimisha mwanamke umelielimisha taiga zima. Leo mwanamke ndiye anayejua afya ya mtoto na kuandaa chakula bora.
Leo wakati mataifa kama uingereza, China, Japan, ujerumani, marekani yanahaha namna ya kuboresha afya za watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kwa kuwekeza elimu kwa wanawake leo sisi ndo tunaibuka kwenda kinyume na maendeleo huku tukijinasibu kwenda sambamba na malengo ya milenia. Hatari.
Nahisi mkuu bado hajui tatizo ama matatizo ama mikosi ama magonjwa yanayoidhuru nchi hii.
Jiulize tukiwafukuza wasiendelee na masomo ndiyo madarasa yatatosha?, ndiyo viwanda vinavyojengwa na kuuzwa na serikali ya ccm vitafufuka?,ndiyo mikataba mibovu inayoingiwa na serikali yetu kupitia viongozi itakuwa sawa?. Ndiyo wasomi wa Tanzania wataacha kujipa vyeo vya udokta na uprofesa kama wasanii?.
Kama huwezi kudumu na mtaji wa biashara Mungu huweka wigo usifanikiwe mpaka hapo akili yako itakapotulia na kuhimili ndipo unaanza kufanikiwa.
Hii ndiyo sababu umri wa kufanikiwa haueleweki wengine wanatajirika toka ujana hadi uzeeni wengine kinyume chake wengine hufa masikini.
Mkuu kama tunataka kusonga mbele imarisha mfumo wa elimu iliyo bora siyo bora elimu hapo hutasikia mtu analalamika ukosefu wa ajira huku anajiita msomi. Iwekee katiba ulinzi bora baada ya kuiunda upya ili ikitokea ukafanya mazuri asije mtu akakurithi na kuyabomoa yote mema uliyofanya kisa ukosefu wa kinga ktk katiba.
Leo Tanzania kila mtu anaamua atakavyo kwa kuwa katiba ni nzuri ila haina kinga mlinzi ndiyo maana yule mzanzibari alifuta uchaguzi peke yake.
Chonde mkuu rudi utafakari upya uendane na malengo ya milenia kwani nchi hii siyo kisiwa.
 
Tushatoka huko umechelewa, sasa tunakomaa na yule fisadi anayesaka kiki kwa nguvu kupitia mgongo wa dini!
 
Tushatoka huko umechelewa, sasa tunakomaa na yule fisadi anayesaka kiki kwa nguvu kupitia mgongo wa dini!
Tunahitaji kutetea haki na siyo kumtetea mtu na ikiwa mtu ana haki anaitafuta basi ataipata ndani ya haki tuiteteayo.
Sina nia mbaya na mtu bali nina nia mbaya na mtu anayeukataa ukweli.
Ikiwa huna mafanikio na umeoa basi mkeo aweza kuwa sehemu kubwa ya tatizo. Mpe mtoto wa kike elimu bora kwa ustawi wa jamii.
 
Back
Top Bottom