Rais Putin atoa amri ya jeshi lake kuondoka Syria Mara moja

Ubavu

JF-Expert Member
Jun 19, 2012
2,790
3,254
Rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa amri kwa wanajeshi walioko Syria kurejea nyumbani mara moja kwa sababu tayari wametekeleza asilimia kubwa ya malengo yao.

Akizungumza katika ikulu ya Kremlin Putin, alisema

''Tayari tumeshakamilisha asilimia kubwa ya madhumuni yetu nchini Syria kwa hivyo kuanzia jumanne (kesho) ningependa asilimia kubwa ya jeshi letu kurejea nyumbani.'' alisema bwana Putin.

Tangazo hilo lake limewaacha wachanganuzi wengi wamepigwa na mshangao kwani hakukuwa na dalili zozote za kuwepo kwa tukio kama hilo.

Aidha Putin ametangaza hilo katika siku ambayo mazungumzo ya amani yameanza upya mjini Geneva Uswisi.

Urusi ni mshirika wa karibu sana wa rais wa Syria Bashar al-Assad.

Ikulu ya Kremlin inasema kuwa rais Bashar al-Assad alifahamishwa kuhusu hatua hiyo.

Itakumbukwa kuwa kuingia kwa majeshi ya Urusi katika vita vya Syria vilibadili kabisa taswira ya vita hivyo.

Kwa wakati huo waasi walionekana kuwa walikuwa wanaelekea kuishinda nguvu jeshi la Syria kinyume na hali ilivyo sasa ambapo majeshi watiifu kwa rais Assad wameanza hata kuteka maeneo yaliyokuwa chini ya waasi.

Rais Putin hata hivyo amesema kuwa kambi ya kijeshi ya Hmeimim na bandari ya Tartus itasalia chini ya jeshi la Urusi.

Huku akisisitiza kuwa zitalindwa ''kwa hewa ardhini na hata baharini''

Source BBC world.

Nadhani mmeona jinsi mwanaume anavyofanya kazi. Sio america ambao mpaka kesho bado wanaangaika Iraq na Afghanistan..
 
Kwa nchi ya Urusi kuondoa sehemu kubwa ya majeshi yake huko Syria ni jambo jema na ni katika kusaidia mazungumzo ya amani yafanikiwe pia.. Wachambuzi wa masuala ya kivita hebu tusaidieni hivi hatua hii haiwezi ikawapa waasi nguvu ya kujipanga upya?. Kama ni kweli kwa yanayo semwa na baadhi ya wadau kuwa Us walikuwa nyuma ya hawa waasi tunaweza kusema kuwa American ndio wameshindwa katika uwanja wa vita?..

Baadhi wamesema Urusi imeweza kufanikisha kujaribu silaha zao, sasa je vita vilivyo kuwa vikipiganwa Syria vinatosha kuthibitisha au vilikidhi haja ya Urusi katika kufanyia majaribio hayo ya silaha...

.Tusaidieni kwa mnaojua masuala haya ya vita, nini maoni yenu.Nnatanguliza shukrani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom