Rais Paul Kagame wa Rwanda, akagua gwaride la Jeshi la Tanzania (JWTZ)

Huyo anayekagua askari wa JWTZ ni Chief of Staff wa Majeshi ya Rwanda.

best.jpg
 
11072720_706425619468415_6496588163067173375_n.jpg

Rais wa Rwanda Mhe.Paul Kagame akikagua gwaride la heshima.alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Mhe.Rais Kagame yupo nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Ukanda wa Kati kuhusu Uwekezaji na Viwanda unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Sijawahi kujua hii kitu, huwa wanakagua nini? Mavazi au kitu gani? Maana huwa sielewi vizuri hii kitu labda ipewe jina lingine. Maoni yangu
 
Hizo ni protocol za raisi yeyote apokelewapo.CHADEMA kama hamlijui hata hilo huko ikulu mtafanyaje hamjui hata kiongozi wa nchi huwa anapokelewaje.

Na nyie siku hizi naona mbowe akienda mbali anapokelewa na kagwaride ka mabouncer wa billicanas club mnawaita red brigade
Hahahaaa
 
Kagame ni head of state. Kupigiwa mizinga ni itifski.na kukagua gwaride ni itifaki pia. ikizingstiwa Pk ni mjeshi.
 
Bado tunawavalisha askari wetu OVERZIZED UNIFORMS na VIATU VYA MITUMBA

Hivi hatuna bunduki zingien zaidi ya hizo?

Mkuu bunduki aina nyingine zipo. Hizo walizonazo pamoja na uwezo wake wa kutumika kama bunduki, lakini ni muafaka kwa gwaride. Maana wangeonekana na SMG, ungesema hazitoshi wabebe vifaru.
 
Jk hana chuki na kagama na warwanda wake, watanzania hatuna chuki nao pia, lakini kuna maraia humu yenyewe yana chuki ya kudumu na kagame na ukweli hayo maraia sio watanzania kabisa.
 
..tatu, amemaliza sintofahamu iliokuwepo kati yake na Kagame. Sasa Rwanda imerejea tena na kuwa fully committed kutumia reli na bandari za Tanzania. Leo Raisi Kagame amezindua treni ya mizigo ya Rwanda toka bandari ya Dsm.

..nne, Coalition of the Willing au CoW, imezikwa rasmi leo Dsm kwa ziara hii ya Raisi Kagame ambaye amepokelewa kwa heshima za kijeshi hapa Dsm.

Hahahaha. Mnajikomba tuu baada ya mambo kutokwenda kama mlivyotaka.

Mlitaka uadui kati ya nchi hizi mkasahau kuwa kati ya nchi na nchi kinacho matter siyo urafiki bali ni interests.

Natumaini wale wote wanaitumia hii forum kutaka kuleta uadui kati ya nchi hizi mbili kwa manufaa yao or just for fun watakoma once and for all.

Kama hawamtaki Kagame waingie msituni wamwondoe na siyo kutumia mgongo wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom