Rais Paul Kagame amekanusha kwamba Serikali yake ilimteka Paul Rusesabagina ambaye ni nyota wa filamu ya Hotel Rwanda

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,406
2,000
Rais Paul Kagame wa Rwanda Jumapili amekanusha kwamba serikali yake ilimteka Paul Rusesabagina ambaye sasa anashikiliwa nchini humo kwa makosa ya ugaidi na mengineyo.

Rusesabagina ni maarufu duniani kutokana na alivyoonyeshwa katika filamu ya Hotel Rwanda kama shujaa aliyesaidia kuokoa maisha ya mamia ya watu wakati wa mauaji ya halaiki nchini humo.

Katika mkutano na wanahabari kwa njia ya mtandao kutoka mji mkuu wa Rwanda, Kigali, Rais Kagame hakusema wazi namna Rusesabagina alivyokamatwa, lakini alisema kwamba walimfanyia mbinu ya kusafiri kwenda Rwanda kabla ya kukamatwa kwake.

Alisema si kweli kwamba Resusebagina alitekwa na maafisa wa Rwanda nje ya nchi hiyo. Kigali ilitangaza kumshikilia Resesabagina Agosti 1, na kumwonyesha kwa umma akiwa amefungwa pingu.

Kumekuwa na habari tofauti kwamba Rususebagina alikamatwa na maafisa wa Rwanda katika uwanja mmoja wa ndege nje ya Ubelgiji ambako amekuwa akiishi kwa miaka kadhaa sasa.

Idara ya uchunguzi wa makosa ya jinai ya Rwanda imeeleza kwamba Rusesabagina anakabiliwa na mashitaka kadhaa ikijumuisha ya ugaidi, kufadhili ugaidi, uhaini, utekaji na mauaji.

Rwanda imemshutumu Rusesabagina kwa kushiriki katika mashambulizi ya waasi wa National Liberation Front – FLN – kusini mwa Rwanda katika mpaka na Burundi hapo mwaka 2018. Paul Rusesabagina ana uraia wa Ubelgiji lakini alikuwa na hati halali za kuishi Marekani hadi alipokamatwa.

Rais Kagame pia amezungumzia maandamano yaliotokea wiki iliyopita mbele ya ubalozi wa Rwanda mjini Kinshasa nchini DRC, wale waliopanga maandamano hayo walikuwa nyuma ya mpango mpana wa kuharibu uhusiano mzuri wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wiki iliyopita mbele ya ubalozi wa Rwanda mjini Kinshasa kulitokea maandamano makubwa yakishinikiza kwamba balozi wa Rwanda nchini humo Vincent Karega arejeshwe Rwanda kutokana na sababu ambazo hazikufafanuliwa. “Hivi vita ambavyo vimekuwa vikitokea vina historia yake, kupotosha ukweli kwa kurahisisha mambo huku wakisema kila kitu kinasababishwa na Rwanda, lakini hilo ni wazi na ni rahisi kulielewa, wanafanya hivi ili kupata nafasi ya kuficha nafasi yao kwenye matatizo ambayo yamekuwa yakitokea na jinsi walivyohusika kwenye matatizo hayo” alisema rais Kagame.

Kagame pia amezungumzia uhusiano wa Rwanda na mataifa ya Uganda na Burundi ambayo kwa miaka ya hivi karibuni yamekuwa mahasimu wakubwa wa Rwanda “uhusiano wetu na Burundi na Uganda bado una doa kidogo bado unahitaji kazi zaidi za kufanya ili uweze kuboreka na watu waishi vyema, kwa upande wa Burundi nadhani mmekuwa mkifuatilia sisi tulifanya kila liwezakanalo ili kwenda na wakati tuliofikia,lakini ilionekana kwamba wenzetu wa Burundi ni kama hawakuitikia” aliongeza rais huyo.

VoaSwahili
 
Mr Putin

JF-Expert Member
Feb 13, 2019
243
250
Imejulikana jamaa kajileta mwenyewe kwenye zile harakati zake za kutafutia support waasi wake:iko hivi: akiwa marekani ka pigiwa simu kua Rais wa Zamibia Lungu anamhitaji ili wa zungumzia issue ya support na yale aliyo yasema huko mahamani msemaji wa kundi lake Calixte Sankara kuhusu tuhuma za kupewa support na Rais huyo wa Zambia Lungu nchini Rwanda. Jamaa kaona hiyo bahati sana na aka chukua ndege to dubai ili akutane huko na wajumbe wa Rais Lungu na kweli wa kakutana kwenye hotel ,wakapiga story na kupumzika kidogo jamaa akiwa so excited to meet Mr President.

Akaambiwa kuna jet iko airport imeshafika kuwachukua kuelekea Lusaka na safari ikaanza kwenda Lusaka,walipofika kaunde airport wa kafikia lounge ya kifahari wakingojea Mr President ku approve mukutano. Basi bana wakawa wanapiga wine kidogo kidogo!akaja mtu akiwa na simu ikiwa inaita na akasema Rais Lungu amepiga simu na ikawekwa loudspeaker !

Jamaa Rusesabagina akasikia mwenyewe! Mr President akasema now niko kampala it's better you come right now to kampala ili tuzungumze issue yote hapa tukiwa na Rais M7,itakua vizuri zaidi and see how we can help you to achieve you goal!. Jamaa kasema woow!! This is good opportunity! This time am going to overthrow kagame.

Basi bana jet ikapandwa tena na furaha juu! Na wine ilikuwa imepanda kidogo kichwani ndio safari ikaanza na kagiza kalikua kametanda kidogo, na akaona asinzie at least 20 minutes ili afike ile wine ikiwa imepungua kichwani. Jamaa kuja kuzinduka kaona jamaa wa 2 mmoja mbele na mwingine nyuma na akawa hivi🤤!!na akaambiwa hivi:Urakaza neza kugihugu cyane cya mavuko!!! (Karibu sana katika nchi yako ya kuzaliwa!! )Jamaa tena akawa hivi 🤤!! Akaomba maji ya kunywa akapewa maji ameandikwa INYANGE INDUSTRIES. hapo akajua kua ameingizwa cha KIKE.🤣🤣🤣 Kushuka kaona gari inje imeandikwa RIB (Rwanda Investigation bureau) pingu na maneno haya: you are under arrested now.

Mjinga kabisa!! Na hapo kimetumika kitu kinaitwa Tricky not kidnap .jamaa wako vizuri ku deal na international issues
 
blackcornshman

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
4,199
2,000
Imejulikana jamaa kajileta mwenyewe kwenye zile harakati zake za kutafutia support waasi wake:iko hivi: akiwa marekani ka pigiwa simu kua Rais wa Zamibia Lungu anamhitaji ili wa zungumzia issue ya support na yale aliyo yasema huko mahamani msemaji wa kundi lake Calixte Sankara kuhusu tuhuma za kupewa support na Rais huyo wa Zambia Lungu nchini Rwanda. Jamaa kaona hiyo bahati sana na aka chukua ndege to dubai ili akutane huko na wajumbe wa Rais Lungu na kweli wa kakutana kwenye hotel ,wakapiga story na kupumzika kidogo jamaa akiwa so excited to meet Mr President. Akaambiwa kuna jet iko airport imeshafika kuwachukua kuelekea Lusaka na safari ikaanza kwenda Lusaka,walipofika kaunde airport wa kafikia lounge ya kifahari wakingojea Mr President ku approve mukutano. Basi bana wakawa wanapiga wine kidogo kidogo!akaja mtu akiwa na simu ikiwa inaita na akasema Rais Lungu amepiga simu na ikawekwa loudspeaker ! Jamaa Rusesabagina akasikia mwenyewe! Mr President akasema now niko kampala it's better you come right now to kampala ili tuzungumze issue yote hapa tukiwa na Rais M7,itakua vizuri zaidi and see how we can help you to achieve you goal!. Jamaa kasema woow!! This is good opportunity! This time am going to overthrow kagame.

Basi bana jet ikapandwa tena na furaha juu! Na wine ilikua imepanda kidogo kichwani ndio safari ikaanza na kagiza kalikua kametanda kidogo, na akaona asinzie at least 20 minutes ili afike ile wine ikiwa imepungua kichwani. Jamaa kuja kuzinduka kaona jamaa wa 2 mmoja mbele na mwingine nyuma na akawa hivi🤤!!na akaambiwa hivi:Urakaza neza kugihugu cyane cya mavuko!!! (Karibu sana katika nchi yako ya kuzaliwa!! )Jamaa tena akawa hivi 🤤!! Akaomba maji ya kunywa akapewa maji ameandikwa INYANGE INDUSTRIES. hapo akajua kua ameingizwa cha KIKE.🤣🤣🤣 Kushuka kaona gari inje imeandikwa RIB (Rwanda Investigation bureau) pingu na maneno haya: you are under arrested now.

Mjinga kabisa!! Na hapo kimetumika kitu kinaitwa Tricky not kidnap .jamaa wako vizuri ku deal na international issues
Kama kweli vile.
 
kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,239
2,000
Hakika kagame ni gaidi la kimataifa na mtu laghai na muongo he is a big fraude kwa jinsi anavyojipambanua kama kiongozi bora. Ni mtu mkabila mkubwa na mnafiki haijawahi kutokea. Ana wivu na kisasi cha ajabu. As long as yeye na genge lake la ukaburu wa kitutsi wanaongoza rwanda eneo la maziwa makuu hasa majimbo ya kivu congo amani itakua ndoto.

La kusikitisha wazungu wanamuunga mkono kutokana na unafiki wake. Hebu fikiri raia wa ubeljiji anayeishi marekani kihalali anatekwa na kurudishwa Rwanda ila ubeljiji na marekani hawajatamka kitu kwa kua mtu huyo ni mwafrika mhutu au tuseme mbantu mwenye asili ya rwanda. Hii kitu lazima ikome haki iwe kwa kila mwananchi rwanda sio haki kwa watutsi tu.
 
LOVE U JF

JF-Expert Member
Dec 9, 2015
1,900
2,000
Imejulikana jamaa kajileta mwenyewe kwenye zile harakati zake za kutafutia support waasi wake:iko hivi: akiwa marekani ka pigiwa simu kua Rais wa Zamibia Lungu anamhitaji ili wa zungumzia issue ya support na yale aliyo yasema huko mahamani msemaji wa kundi lake Calixte Sankara kuhusu tuhuma za kupewa support na Rais huyo wa Zambia Lungu nchini Rwanda. Jamaa kaona hiyo bahati sana na aka chukua ndege to dubai ili akutane huko na wajumbe wa Rais Lungu na kweli wa kakutana kwenye hotel ,wakapiga story na kupumzika kidogo jamaa akiwa so excited to meet Mr President. Akaambiwa kuna jet iko airport imeshafika kuwachukua kuelekea Lusaka na safari ikaanza kwenda Lusaka,walipofika kaunde airport wa kafikia lounge ya kifahari wakingojea Mr President ku approve mukutano. Basi bana wakawa wanapiga wine kidogo kidogo!akaja mtu akiwa na simu ikiwa inaita na akasema Rais Lungu amepiga simu na ikawekwa loudspeaker ! Jamaa Rusesabagina akasikia mwenyewe! Mr President akasema now niko kampala it's better you come right now to kampala ili tuzungumze issue yote hapa tukiwa na Rais M7,itakua vizuri zaidi and see how we can help you to achieve you goal!. Jamaa kasema woow!! This is good opportunity! This time am going to overthrow kagame.

Basi bana jet ikapandwa tena na furaha juu! Na wine ilikua imepanda kidogo kichwani ndio safari ikaanza na kagiza kalikua kametanda kidogo, na akaona asinzie at least 20 minutes ili afike ile wine ikiwa imepungua kichwani. Jamaa kuja kuzinduka kaona jamaa wa 2 mmoja mbele na mwingine nyuma na akawa hivi!!na akaambiwa hivi:Urakaza neza kugihugu cyane cya mavuko!!! (Karibu sana katika nchi yako ya kuzaliwa!! )Jamaa tena akawa hivi !! Akaomba maji ya kunywa akapewa maji ameandikwa INYANGE INDUSTRIES. hapo akajua kua ameingizwa cha KIKE. Kushuka kaona gari inje imeandikwa RIB (Rwanda Investigation bureau) pingu na maneno haya: you are under arrested now.

Mjinga kabisa!! Na hapo kimetumika kitu kinaitwa Tricky not kidnap .jamaa wako vizuri ku deal na international issues
Aisee umetisha jomba
 
Mr Putin

JF-Expert Member
Feb 13, 2019
243
250
Hakika kagame ni gaidi la kimataifa na mtu laghai na muongo he is a big fraude kwa jinsi anavyojipambanua kama kiongozi bora. Ni mtu mkabila mkubwa na mnafiki haijawahi kutokea. Ana wivu na kisasi cha ajabu. As long as yeye na genge lake la ukaburu wa kitutsi wanaongoza rwanda eneo la maziwa makuu hasa majimbo ya kivu congo amani itakua ndoto.

La kusikitisha wazungu wanamuunga mkono kutokana na unafiki wake. Hebu fikiri raia wa ubeljiji anayeishi marekani kihalali anatekwa na kurudishwa rwanda ila ubeljiji na marekani hawajatamka kitu kwa kua mtu huyo ni mwafrika mhutu au tuseme mbantu mwenye asili ya rwanda. Hii kitu lazima ikome haki iwe kwa kila mwananchi rwanda sio haki kwa watutsi tu.

Hayo ya kwako na chuki ya binafsi!
Kwahiyo Sankara mbona alifuatwa na yuko gerezani ni mhutu? Ideology za ukabila kama zako ndio kagame hataki. Vingine mhalifu ni mhalifu tu hanaga kabila.
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
153,236
2,000
Kwahiyo alijiteka mwenyewe akajifunga pingu na kujisafirisha hadi Rwanda kisha akajikabidhi kwa askari
 
Mr Putin

JF-Expert Member
Feb 13, 2019
243
250
Hakika kagame ni gaidi la kimataifa na mtu laghai na muongo he is a big fraude kwa jinsi anavyojipambanua kama kiongozi bora. Ni mtu mkabila mkubwa na mnafiki haijawahi kutokea. Ana wivu na kisasi cha ajabu. As long as yeye na genge lake la ukaburu wa kitutsi wanaongoza rwanda eneo la maziwa makuu hasa majimbo ya kivu congo amani itakua ndoto.
La kusikitisha wazungu wanamuunga mkono kutokana na unafiki wake. Hebu fikiri raia wa ubeljiji anayeishi marekani kihalali anatekwa na kurudishwa rwanda ila ubeljiji na marekani hawajatamka kitu kwa kua mtu huyo ni mwafrika mhutu au tuseme mbantu mwenye asili ya rwanda. Hii kitu lazima ikome haki iwe kwa kila mwananchi rwanda sio haki kwa watutsi tu.
Alafu ujue sheria za Rwanda ziko strictly !,ukiiba hela ya Uuma unakwenda jela Mali zako zinauzwa na case ya rushwa inakua attached kwenye CV yako ndani ya Systems zote utakapo omba kazi myaka ijayo wataona kua ulifungwa kwa case ya rushwa. Sio kama hapa unahamishwa na kula bata huko huko! Swali? Kayumba nyamwasa mhutu?
 
Mr Putin

JF-Expert Member
Feb 13, 2019
243
250
Kwahiyo alijiteka mwenyewe akajifunga pingu na kujisafirisha hadi Rwanda kisha akajikabidhi kwa askari
Kwanza jua international laws zikoje kumshika muhalifu ambae yuko inje ya nchi! Na je akiwa na uraia wa nchi nyingine inakuaje? Inakuaje mtu kutekwa kisheria za kimataifa? What si Kidnapping ? Airports zote wakisema alitoka kihalali. Sema mbwa kaonehwa mfupa na yeye kafuata. Na Zambia na watu wake kwenye hizo halakati zake za kutaftia waasi wake support ndio walimsaliti.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom