Rais Obama Katika Mashaka ya Mafua ya Nguruwe Baada Ya Mtu Aliyesalimiana naye Kufari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Obama Katika Mashaka ya Mafua ya Nguruwe Baada Ya Mtu Aliyesalimiana naye Kufari

Discussion in 'International Forum' started by Pdidy, Apr 29, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,613
  Likes Received: 5,783
  Trophy Points: 280
  Rais Obama Katika Mashaka ya Mafua ya Nguruwe Baada Ya Mtu Aliyesalimiana naye Kufariki
  [​IMG]
  Rais Obama akiwa na mwenyeji wake Rais wa Mexico Felipe Calderon katika ziara yake nchini humo wiki mbili zilizopita ( Picha: EPA)Monday, April 27, 2009 6:41 AM
  Rais Obama yupo kwenye mashaka makubwa ya kukumbwa na mafua ya nguruwe baada ya kugundulika kuwa mtu aliyepeana naye mkono wakati alipokuwa ziarani nchini Mexico alifariki siku moja baada ya kupeana naye mkono kwa ugonjwa wenye dalili kama za homa ya mafua ya nguruweMtafiti mmoja wa mambo ya kihistoria ambaye alipeana mkono na rais Obama alipokuwa nchini Mexico alifariki masaa 24 baadae kwa ugonjwa ambao ulihusishwa na homa ya mafua ya nguruwe.

  Ingawa mlipuko wa ugonjwa huo umeua zaidi ya watu 80 nchini Mexico katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, White House imesisitiza kwamba afya ya rais Obama haipo katika hatari yoyote.

  Watu 20 wamethibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo katika miji tofauti nchini Marekani ingawa hali zao sio mbaya.

  Washauri wa mambo ya afya wa rais Obama walikuwa katika tahadhari ya ugonjwa huo baada ya kugundua kuwa virusi vya mafua ya nguruwe viliibuka siku tatu kabla ya rais Obama kuanza ziara yake nchini Mexico.

  Washauri hao wa afya walianza kukuna vichwa baada ya kufahamishwa kuwa Felipe Solis mtafiti wa Akiolojia (archaeologist) ambaye alimpokea rais Obama katika nyumba ya makumbusho alifariki siku moja baadae.

  Kifo chake siku moja baada ya kupeana mikono na rais Obama kilitokana na ugonjwa wa pneumonia ulioambatana na dalili kama za homa ya mafua ya nguruwe.

  Ingawa hakuna chanjo ya kumlinda rais Obama na mlipuko wa mafua hayo ya nguruwe, afya ya rais huyo wa Marekani inafuatiliwa kwa ukaribu zaidi.

  Msemaji wa White House Robert Gibbs alisema: " Ziara ya rais Obama nchini Mexico haijaiweka afya yake kwenye hatari yoyote ile".

  "Muda ambao dalili za ugonjwa huo huanza kujionyesha baada ya kuambukziwa ni kati ya masaa 24 na 48 , lakini tangia tumerudi kutoka Mexico leo ni siku ya tisa, madaktari wamesema kuwa hayupo kwenye hatari yoyote ile".

  Rais Obama alikuwa nchini Mexico kwa ziara ya nusu siku kabla ya kuelekea nchini Trinidad and Tobago kwa ajili ya kilele cha mataifa ya Amerika.
   
 2. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hii habari ni ya uongo, wewe Pdiddy ni muongo, hujataja credible authority iliyosema kwamba yuko hatarini, na madaktari wamesema kinyume na ulivyosema wewe, na unajua, maana hata wewe umebandika kipande hiki:

  Msemaji wa White House Robert Gibbs alisema: " Ziara ya rais Obama nchini Mexico haijaiweka afya yake kwenye hatari yoyote ile"


  "Muda ambao dalili za ugonjwa huo huanza kujionyesha baada ya kuambukziwa ni kati ya masaa 24 na 48 , lakini tangia tumerudi kutoka Mexico leo ni siku ya tisa, madaktari wamesema kuwa hayupo kwenye hatari yoyote ile"
   
Loading...