Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,087
- 6,568
Kama kuna eneo ambalo Watanzania wanakupongeza Rais JPM basi ni kuwa mkweli. Na jana ukiwa Kagera umekiri kuwa kweli huwa unakosea kuchagua viongozi.
Hilo la kule Ubungo la watoto wa shule kukaa chini, kusomea kwenye madarasa mabovu tena kuna RC, DC, Mkurugenzi na Mbunge wote wana CCM kweli limekuchefua, na sio jambo zuri.
Ila Mh Rais kwa kuwa umekiri kuwa huwa unakosea kuchagua viongozi sometimes, basi tambua sio hao tu wa Dar es Salaam uliokosea kuchagua maana wapo wengi.
Ukizunguka Tanzania kero kubwa ni hiyo. Uhaba wa vyumba vya madarasa huku viongozi uliowachagua wanakusanya kodi, ukosefu wa maji na huduma za afya ndio balaaa. Kwa ufupi Mh Rais ungekuwa unafuatilia kero za wananchi kupitia mitandao ya kijamii, ungepata ukweli kuwa 60% ya viongozi uliowachagua wanakuangusha na ulikosea kuwachagua. Maana hata utawala bora wengi ni bure kabisa.