RAIS NI KIONGOZI WA WATU,LAZIMA TUMKOSOE

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,685
1,111
Hatuna nia mbaya na serikali, kwa kuwa tunaipenda Tanzania tunaipenda na serikali yetu pia,ndiyo maana tunaionya na kuikemea pale inapokosea kwa kuwa jukumu la serikali liko mikononi mwetu sisi wananchi ambao tumeiweka madarakani.

Kichekesho ni pale tuliyempa dhamana anapotaka kuwatisha maboss wake ambao ni wananchi. Pamoja na mapungufu ya katiba ya JMT ya mwaka 1977 hakuna sehemu inayompa rais haki ya kuwa juu ya sheria, ndiyo maana kwa kuthibitisha hilo bunge lina uwezo wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais.

Hatukumchagua mtumishi wetu mkuu kwa lengo la kuwatisha wananchi wake,kama kuna wanaomshauri vibaya wanampoteza,nimsihi tu arudi kwenye katiba ambao ndiyo msahafu wa nchi na asimamie hapo. Nchi haiendeshwi kwa matakwa binafsi ndiyo maana tuna katiba,tuna sheria na kanuni zinazotuongoza.

Nachelea kusemea hili kutokana na tabia inayotaka kujengeka ya kuwatishia wapiga kura ambao ndiyo wananchi waliokupa dhamana,kitendo cha kuziambia taasisi binafsi kuwa zisifikirie kuwa zina freedom to that extent ni kuwakosea waliokupa nafasi hiyo wakitegemea utumishi uliotukuka toka kwako. Waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari ni Watanzania wenzako,wana haki katika nchi yao kama wewe ulivyo na haki,kuwatishia si jambo la busara kwa kuwa wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.

Hatuwezi kufikia malengo ya uchumi wa kati ikiwa nchi imegawanyika vipande vipande bila kuwa na mshikamano wa kitaifa. Mshikamano na umoja ndiyo nguzo kuu ya amani ndani ya taifa hili,tunawezaje kujenga mnara wa Babel Ikiwa wajengaji tunaongea lugha tofauti?

Tujisahihishe tulipokosea turudi kwenye misingi yenye kuheshimu utawala wa sheria bila kujali nani ni nani. Jukumu la ujenzi wa taifa ni la kila mmoja,tukizingatia sheria na kusimamia matakwa ya katiba nchi itasonga mbele.
 
Back
Top Bottom