Joseph Mshinga
JF-Expert Member
- Aug 27, 2014
- 232
- 143
NAMNA WABUNGE WA VITI MAALUMU WANAVYOPATIKANA.
NA: Joseph Mshinga.
1.idadi yote ya wabunge wa viti maalumu katika bunge ni asilimia 40 ya viti vyote vya bunge katika majimbo yote(40% of all seats/constituencies ).
idadi ya viti vya ubunge ama majimbo kwa sasa ni 264.
40% ya 264 ni ngapi? unaweza kupiga kujua kutakuwa na jumla ya viti maalum wangapi.
FURSA YA CHAMA KUPATA WABUNGE VITI MAALUMU.
kwanza ili chama husika kiweze kupata wabunge wa viti maalumu ni sharti chama hicho kiwe na jumla ya kura zisizopungua asilimia 5 ya kura zote za wagombea wote wa ubunge wa chama hicho katika jumla ya kura zote za wabunge wa vyama vyote.
Hii bila kujalisha kama chama kimeshinda wabunge ama hakikushinda katika majimbo kiliyogombea. Hata kama chama kimeshindwa katika majimbo yote lakini kikafanikiwa kupata kura zinazofikia asilimia 5 ya kura zote za wabunge wa vyama vyote basi chama hicho kinapata fursa ya kuwa na wabunge wa viti maalumu.
kwa hiyo ieleweke wazi kuwa idadi ya wabunge walioshinda haitumiki kupata wabunge viti maalumu.
mbunge aliyeshinda kutoka jimbo la wapiga kura wachache mathalani majimbo ya Zanzibar atakuwa na kura chache pengine kuliko mtu aliyeshindwa katika jimbo la wapiga kura wengi kama majimbo ya mjini Dar es salaam.Hivyo huyu aliyeshindwa anaweza kuchangia zaidi kupatikana kwa mbunge wa viti maalumu kuliko aliyeshinda kwa mfano huu niliotoa.
na kwa vyovyote vile majimbo ya Zanzibar yanachangia asilimia ndogo sana katika viti maalumu. Mchango wa kura za viti maalumu katika majimbo yote ya Zanzibar yenye jumla ya wapiga kura laki 4 na ushehe ni mdogo kuliko mchango wa majimbo yote ya mkoa wa Shinyanga ulio na wapiga kura wapatao laki 7.
kwa hiyo hapa ni mchezo wa kupata kura nyingi zaidi na si kushinda viti vingi zaidi vya ubunge.
MGAWANYO WA HAO WABUNGE.
ili kupata kila chama kinapaswa kugawiwa wabunge wangapi inabidi asilimia ya kura za wabunge wote waliogombea katika kila chama dhidi ya kura zote za vyama vinavyostahili kupata wabunge viti maalumu ikokotolewe na hiyo itasaidi kujua kila chama kitapata asilimia ngapi kati ya hao wabunge wote(40% of 264). Idadi hiyo ipe jina la M.
kuna mazingira ambayo chama hakikusimamisha wagombea ubunge ama mgombea ubunge wake alipita bila kupingwa katika jimbo. Katika mazingira haya hakuna kura halali za mbunge kwa chama husika zilizopigwa na wapiga kura.
kwa hiyo ili kupata idadi ya kura zote zingatia mambo yafutayo.
1.Jumla ya kura zote za wagombea ubunge wa chama hicho katika maeneo kilichosimamisha wagombea ni sehemu ya kura zinazotumika. ziite jina la kura X.
2.Jumla ya kura zote za mgombea urais katika maeneo ambayo chama hicho hakikusimamisha mgombea ubunge zitahesabiwa kuwa ni kura za ubunge za chama hicho, Ziite jina la kura Y.
Mfano katika jimbo la Kinondoni ambapo Chadema haikusimamisha mgombea ubunge bali alisimamishwa wa CUF (UKAWA) basi kura za Edward Lowassa(mgombea Urais) katika Jimbo hili zitahesabiwa kama kura za mgombea ubunge wa chadema kwa swala la viti maalumu katika jimbo hili la kinondoni.
na hizo za mbunge wa CUF kinondoni zinaingia katika hesabu ya CUF. zile za mgombea wa CCM alieshindwa bwana IDD AZAN zinaingia katika hesabu ya CCM.
3.kama chama kimepita bila kupingwa katika jimbo. Maana yake uchaguzi haukufanyika kabisa kwa kuwa mgombea alikuwa mmoja tu na hivyo hakuna kura zilizopigwa. Kwa mazingira haya hapa kura za Rais hazitahusika. Kinachofanyika ni kukokotoa asilimia 51 ya wapiga kura wote walioandikishwa katika jimbo hilo bila kujali walijitokeza wote kupiga kura ama laa. (51% of registered voters in that constituency).Ziite jina la kura Z.
asilimia hizo zinahesabiwa kuwa ni kura halali za mgombea huyo aliyepita bila kupingwa ambazo zinapaswa kutumika wakati wa kukokotoa wabunge wa viti maalumu.
kwa kuwa mwaka huu hakuna mbunge aliyepita bila kupingwa basi kipengere cha 1 na 2 ndivyo vitatumika kukokotoa idadi ya vitu maalumu kwa kila chama.
hesabu ni kama hivi.
X + Y + Z= kura zote za ubunge za kila chama.
NB:
1.kama chama hakima mgombea urais Y= 0 kwenye mazingira ya Y.
2. kwa kuwa hakuna mbunge aliyepita bila kupingwa nchi nzima basi Z=0 kila mahali.
(a). Chadema=X+Y+Z= P1
(b). CUF=X+Y+Z=P2
(c). CCM=X+Y+Z=P3
kura zote walizopigiwa wabunge.
P1+P2+P3+P4+............+Pn=W (Jumla ya kura za wagombea ubunge wote toka vyama vyote vilivyosimamisha wagombea). W itatumika tu kujiridhisha kama chama kinastahili kupata wabunge viti maalumu na si vinginevyo.
hapa kuna kura za vyama ambavyo havitapata viti maalumu kama ACT, NRA, CHAUMA nk nazo zinaingizwa katima jumla ya kura zote zilizopigwa kwa wagombea wabunge wote.
lakini mgawanyo wa asilimia kwa vyama utahusisha tu vyama vyenye sifa ya kupata wabunge wa viti maalumu.
kwa hiyo chukua P1+P2+P3=Q. na utafute asilimia ya kila chama katika hivyo vitatu.
lakini sina uhakina kama CUF imefikisha asilimia 5 ya kura zote kwa maana ya P2.kwa kuwa wagombea wengi wametoka Zanzibar kuliko na wapiga kura wachache ama kura chache.(mpaka kujiridhisha kwa CUF).
(i). viti maalumu chadema.
(P1/Q x 100) x M= Viti maalumu chadema.
(ii). viti maalumu CUF.
( P2/Q x 100) x M=viti maalumu CUF.
(iii). viti maalumu CCM.
(P3/Q x 100) x M= viti maalumu CCM.
M ni jumla ya wabunge wote wa viti maalumu bungeni ambao ni (40/100 x 264).
NA: Joseph Mshinga
signature: 04/11/2015.