samirnasri
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 1,388
- 213
Kuna tangazo moja nimekuwa nikiliona kwenye TV ambalo linamuonesha rais Kikwete akiwasisitiza wananchi ili wanaponunua vitu waombe risiti ili kutoinyima serikali mapato. Tangazo hilo pia linahusisha utumiaji wa mashine mpya za TRA za ushuru.
Najiuliza kama kweli lile ni tangazo au ni hotuba ya rais maana naona rais wa nchi ni mtu mkubwa sana kuhusika kwenye matangazo ya biashara. Nadhani wapo watu wengi sana ambao wangeweza kuhusika kwenye tangazo hilo na sio rais wa nchi.
Nawasilisha.