Rais na tangazo la ushuru/ TRA

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Kuna tangazo moja nimekuwa nikiliona kwenye TV ambalo linamuonesha rais Kikwete akiwasisitiza wananchi ili wanaponunua vitu waombe risiti ili kutoinyima serikali mapato. Tangazo hilo pia linahusisha utumiaji wa mashine mpya za TRA za ushuru.

Najiuliza kama kweli lile ni tangazo au ni hotuba ya rais maana naona rais wa nchi ni mtu mkubwa sana kuhusika kwenye matangazo ya biashara. Nadhani wapo watu wengi sana ambao wangeweza kuhusika kwenye tangazo hilo na sio rais wa nchi.

Nawasilisha.
 
Mpwa umechukua kabisa maneno yangu yaani inatisha na kusikitisha umaarufu na hadhi ya Rais inapoporomoka hadi kufikia kwenye matangazo, tena ukiangalia sana kwa jicho la pili lile tangazo ni la biashara kama thread moja ilivyowahi kuripoti hapa kuhusu bei halisi ya zile mashine! Nilijiuliza hivi, je inawezekana kweli Kamishna or Mkurugenzi wa TRA atumike kwenye matangazo, jibu likawa hapana labda afisa uhusiano! sasa iweje RAIS? au nae amekua afisa uhusiano wa Nchi? Mmmh ya Ngoswe.....
 
Ile naona wemechukua hotuba yake na kuiingiza ktk tangazo. Kodi ni muhimu kwani inaongeza pato la taifa hivyo raisi kuhamasisha sio suala la ajabu, binafsi sioni tatizo kabisa.
 
Ile naona wemechukua hotuba yake na kuiingiza ktk tangazo. Kodi ni muhimu kwani inaongeza pato la taifa hivyo raisi kuhamasisha sio suala la ajabu, binafsi sioni tatizo kabisa.
hawa kufikiria vizuri ,rais wetu hana mvuto kodi zita pungua...siku ya uchaguzi igunga alisema watu wajitokeze kupiga kura lakini idadi ndio ikapungua kuliko 2010
 
huu ni uchochezi... yaan ionekane kuwa huyo prezdaa anasura ya kwavutia wafanyabiashara, na kuwashawishi wape kodi... ni udhalilishaji na dharau za wazi kabisa kwa wana-Magamba.. hivi si mwenyekiti wa Magamba-taifa yule...? (me 4gotten bhana...).
 
Rais anayeweza kupiga picha na 50cent na Teddy Kalonga anapoonekana kwenye tangazo la TRA naona ni mafanikio makubwa kwake!
 
Usikute ana % yake kwenye vile vidude ambavyo unakuta vianuzwa mpaka 2mill wakati bei halisi sio iyo
Yale yale ya akina Shimbo matrekta ya kuuza 3mil wanauza mpaka 6mil sorry I mean power tiller.
Nimegundua kufikia hali kama ya Misri sio jambo la ajabu ni vitu kama ivi ndo vinachochea
Personally I dont feel proud kulipa kodi as I know iyo Kodi inakuwa mis-used big time
 
Rais wetu anashabikia kuuza sura bila kujali matokeo yake. Kwenye kuhimiza ulipaji wa kodi yupo, na tabasam kuubwa ! Kuzindua majina mapya kwenye makampuni yanayo badili majina kukwepa kodi yupo. Maskini yupoyupo tu. Hajaambiwa sura ishapoteza mvuto?
 
Watoke zao, mie nahamasisha watu waache kudai risiti ili angalau wapate percent ya chini, kwani kodi tunayoichangia hapa inatumiwa vibaya na serikali.
Wananchi wanavyopiga kelele kuhusu safari zisizo na tija za rais, posho na magari ya kifahari, mnawaona kama wanampigia mbuzi gitaa, watoto wenu wanasoma nje ya nchi, kutibiwa nje ya nchi, walala hoi mnaowaomba wadai risiti hawana madawa hospitalini, shuleni hamna walimu wa kutosha.

Mimi sidai risiti ndo kwanza namuomba muhindi ile 18% ya kodi anipunguzie niile mwenyewe, kuliko baba Riz1 aende nayo USA kupiga picha na 50cent.
 
Wao kama wamekua wezi wa hizi kodi zetu yaafa sisi tusidai risiti ili serikali yao legelege izidi kuanguka
 
Kuna tangazo moja nimekuwa nikiliona kwenye TV ambalo linamuonesha rais Kikwete akiwasisitiza wananchi ili wanaponunua vitu waombe risiti ili kutoinyima serikali mapato. Tangazo hilo pia linahusisha utumiaji wa mashine mpya za TRA za ushuru.

Najiuliza kama kweli lile ni tangazo au ni hotuba ya rais maana naona rais wa nchi ni mtu mkubwa sana kuhusika kwenye matangazo ya biashara. Nadhani wapo watu wengi sana ambao wangeweza kuhusika kwenye tangazo hilo na sio rais wa nchi.
 
kuna Bwana mmoja amejinyonga akaacha kajiujumbe ! " namchukia fulani ....., naona BORA nifanye uamuzi huu ili nisimuone tena"
 
Mr. Everywhere, ni hulka

hujiulizi kwa nini Ben Mkapa alikuwa haonekani sana kama ilivyo kwa J.K
 
Ile naona wemechukua hotuba yake na kuiingiza ktk tangazo. Kodi ni muhimu kwani inaongeza pato la taifa hivyo raisi kuhamasisha sio suala la ajabu, binafsi sioni tatizo kabisa.

Tatizo anaimiza kodi ila wanazifuja angekuwa anasimamia vizur hakuna shida. Yan ni kama analia njaa kuwa kodi mnampa kidogo.
 
Back
Top Bottom