Rais na Mwenyekiti wangu, usisubiri mpaka uharibifu wa Spika Ndugai ukuchafue

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Imefikia hatua Spika anamkosoa kila lililo jema na kukubali yasiyofaa. Ukosoaji wa namna hii si afya kwa ustawi wa nchi yetu.

Tabia hii ameanza kuonesha katika hiki cha awamu ya sita. Mbona Rais Magufuli alikuwa anafanya yanayofanywa na awamu hii lakini hakuwahi kukosoa?

Ukosoaji wa aina ya Ndugai ni moja wa ufa hatari sana katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi. Ukiachana na nchi chache sana duniani ambazo zina uchumi imara wa kujiendesha zenyewe, nchi nyingi zinategemea mikopo ili kukamilisha ujenzi.

Spika licha ya kujua umuhimu wa mikopo yenye riba nafuu na masharti rahisi lakini bado anaona mikopo hiyo haifai. Bila kutoa njia mbadala wa kuongeza mapato ya ndani anapinga mikopo nafuu. Je, maendeleo yatakujaje?

Yawezekana Spika kaona siku zake za kukalia kiti cha uspika zimeisha au ana nia na lengo tofauti la kumkwamisha Rais na Mwenyekiti wake.

Rais na Mwenyekiti wangu, nguvu na uwezo wa kumtoa Spika unao, fanya sasa kabla uharibifu wa Spika haujaota mizizi itakayokuwa migumu kuing'oa.

Update:
Kwa kinachoendelea sasa ndicho kipimo halisi cha nguvu na uwezo wa Rais wa JMT na Mwenyekiti wa CCM Taifa. Tuendelee kuwa waadilifu na wazalendo kwa nchi yetu.

Ikitokea Spika akaondoka kwa njia yoyote ile iwe kujiuzulu, kupitia azimio la bunge au kuvuliwa uanachama atambue kwamba alikuwa na uhuru wa kutoa maoni lakini hakuwa na uhuru wa kupotosha. Tumesikia taarifa na ufafanuzi wa kisomi kutoka mamlaka ya udhamini wa mikopo na madeni ya serikali yaani BOT kwamba deni la taifa ni himilivu hivyo kauli ya kupigwa mnada nchi ni upotoshaji
 
Imefikia hatua Spika anamkosoa kila lililo jema na kukubali yasiyofaa. Ukosoaji wa namna hii si afya kwa ustawi wa nchi yetu.

Tabia hii ameanza kuonesha katika hiki cha awamu ya sita. Mbona Rais Magufuli alikuwa anafanya yanayofanywa na awamu hii lakini hakuwahi kukosoa?

Ukosoaji wa aina ya Ndugai ni moja wa ufa hatari sana katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi. Ukiachana na nchi chache sana duniani ambazo zina uchumi imara wa kujiendesha zenyewe, nchi nyingi zinategemea mikopo ili kukamilisha ujenzi.

Spika licha ya kujua umuhimu wa mikopo yenye riba nafuu na masharti rahisi lakini bado anaona mikopo hiyo haifai. Bila kutoa njia mbadala wa kuongeza mapato ya ndani anapinga mikopo nafuu. Je, maendeleo yatakujaje?

Yawezekana Spika kaona siku zake za kukalia kiti cha uspika zimeisha au ana nia na lengo tofauti la kumkwamisha Rais na Mwenyekiti wake.

Rais na Mwenyekiti wangu, nguvu na uwezo wa kumtoa Spika unao, fanya sasa kabla uharibifu wa Spika haujaota mizizi itakayokuwa migumu kuing'oa
Hata Mzee Samwel Six aliikosoa sana serikali ya Kikwete. Ndugai anatumia haki yake ya kutoa maoni kama ambavyo kina Bulembo wanatumia.
 
Serikali yenye akili husisitiza uzalishaji wa ndani ili iweze kuuza nje na kupata fedha za kigeni. Wanaompotosha mama kwa kopa kopaa kopaaaa kopaaaaaa kopaaaa@aaaaaaaq, sijui wana maana gani.
Tukope kwa tahadhari na kwa viwango.
 
Mnacheza ngoma ya CCM! CCM mtu hawezi kuongea bila kujua Mkiti anataka nini, Ndugai ni mjumbe wa kamati kuu ya chama, na ni spika, anaaccess ya moja kwa moja na Rais, na sidhani kama inapita wiki moja bila kuongea na Rais! Unadhani anajiongelea tu bila kujua nini anafanya/wanafanya?
 
2025 tutashuhudia mengi. Naona Samia nae kaonyesha misuli yake. Kasema ataendelea kukopa. Ila sasa kama wanakopa hizi tozo zetu zinafanya kazi gani ?Au ndo zinawalipa allowances za safari zao.

Si walisema zinajenga nchi...😁
 
CCM na wanachama wao.
Wachokiwaza wao ni kufukuza wanachama wezao kwa sababu wana mtazamo tofauti
 
Waliokuwa wakitupeleka vizuri ni awamu ya 5. Ni ngumu kumeza ukweli lakini walikuwa wakituambia ukweli. Uchumi wa kujidanganya kwa mikopo ya hovyo na kutumia hovyo ni kujidanganya ya hali ya juu sana.
Serikali iliyonyang'anya fedha za watu toka kwenye akaunti binafsi Kwa nguvu na kuteka Hadi wafanyabiashara ilifanya uzuri Kwa hayo?
 
Back
Top Bottom