Alexism
JF-Expert Member
- Aug 14, 2011
- 3,423
- 2,046
WanaCCM bila shaka tumeona na kutambua kua Mwenyekiti wetu wa chama na Rais wa nchi hii sio tena halali yake kugombea nafasi anazo ziongoza kwa sasa. Ni ukweli usio pingika kua Mh. Magufuli amekosa ueledi ambao kweli wanaccm na watanzania tulidhani na kuamini kua anao. Mambo mengi yamefanyika katika kipindi hiki kidogo tangu ashike nafasi hizo ambayo kweli yanawakatisha tamaa wanaccm pamoja na watanzania kwa ujumla wetu. Ni vigumu mno kuendelea na mtu kama huyu maana anakiangamiza na chama na kuwafanya watu watuone CCM kua hatuna maana au malengo mazuri kwa ili Taifa.
Chonde chonde wanaccm awamu moja inatosha huyu mkuu ili tusipoteze uhalali wetu wa kuongoza nchi hii ya Tanzania .
MUNGU IBARIKI TANZANIA
KIDUMU CCM
Chonde chonde wanaccm awamu moja inatosha huyu mkuu ili tusipoteze uhalali wetu wa kuongoza nchi hii ya Tanzania .
MUNGU IBARIKI TANZANIA
KIDUMU CCM