Rais na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii

Lamisa Danish

JF-Expert Member
Nov 17, 2019
285
626
Kwako Mama yetu Mh Rais,

Mm nikiwa kama Shabiki yako namba moja,mkereketwa wako Kindaki Ndaki na mpiga debe wako niliejitolea kukusemea,kukutetea na kukuunga mkono Juhudi zako zote za kuliletea maendeleo taifa letu,Nina haya machache kwako nikiomba uyatupie jicho.
Kwanza

Wafanyakazi wa Nchi hii wanajituma sana ktk kufanya kazi ili kujikimu wao na familia zao,wakati huohuo wakisaidia kulijenga taifa kupitia kodi zao wanazokatwa kabla hata ya kuchukua mishahara yao.

Wamekuwa pia wakilipa kodi kila wakinunua bidhaa mbalimbali madukani,masokoni, kwenye vyombo vya usafiri nk.

Ikiwa yote hayo hayatoshi bado na sasa hivi Wafanyakazi wamekuwa wakilipa TOZO kwenye miamala yao wanayoifanya wanapohamisha fedha kwenda kwa ndugu zao na jamaa zao mbalimbali waliopo vijijini.

Wamekuwa wakifanya haya yote kwa moyo mmoja,bila kujali vipato wanavyopata ktk mishahara hiyo midogo isiyokidhi mahitaji,ila wameendelea kuwa watiifu wakitii mamlaka bila shuruti ukizingatia serekali ya awamu ya tano haikufanya nyongeza yeyote ktk awamu yake.

Pamoja na yote hayo ya kiwango kidogo cha mishahara ukilinganisha na mifumuko ya bei ya bidhaa mbalimbali nchini,TOZO,ulipaji wa kodi kwa wakati nk nk bado kuna suala LA mifuko ya Jamii kama vile NSSF,PSPF nk nk huko pia fedha zinakwenda kutoka kwenye mshahara wa huyu mfanyakazi.

HOJA YANGU ni kwamba nashauri hii mifuko ianzishe Mikopo kwa wafanyakazi ili hii mikopo iwasaidie kufanya mambo yao kama UJENZI wa Nyumba,Kufungua biashara ili kupunguza ukali wa maisha nk nk.

Kwa mfano,Mfanyakazi akiwa amechangia Million 30 aruhusiwe kukopa robo or nusu ya fedha zake ili aweze kufanya mambo yake ingali akiwa na nguvu sababu mnakuja kumpa MTU hela zake uzeeni ameshachoka na hana anachoweza kukifanya sababu nguvu zimeshamuishia na hela zenyewe nyingi.

Huyu MTU hawezi tena kufanya biashara,wala lolote na hapo ndipo wengine huitwa baby na kujikuta pesa zake zinatapanywa ilihali ujanani aliishi kwa tabu.

Faida ya kufanya hivi ni kwamba Hawa wafanyakazi wakishapewa hii mikopo wataizungusha na kuongeza mzunguko wa fedha kuisadia serikali katika suala LA uhaba wa ajira uliopo sasa.

Jambo LA Pili Mh Rais,ni kwa Hawa Wazee waliostaafu or walioacha kazi kwa namna moja ama nyingine wasicheleweshewe kupewa fedha zao,unakuta MTU amefanya kazi ana kadi ya Uanachama siku anataka apewe pesa yake anatakiwa alete barua ya Muajiri kuthibitisha Uajiriwa wake.

Sasa unajiuliza hizo fedha zilizopo kama michango zilikuwa zikilipwa na nani?na imekuwaje wakizipokea kama hawajui huyu MTU ameajiriwa ama Laa?

So Mh Rais Mama yetu kipenzi tunakuomba utupie Jicho hii mifuko ya Jamii Urasimu ni Mwingi pasipo sababu zozote za msingi.

Ni hayo tu Wasalaam
 
Una hoja nzuri sana ya mtu mwenye akili na busara ILA kwa watu kama akina Jenister Mhagama ambao ndio watoa maamuzi hakuna litakalo fanyika.
Kama wanataka kurudisha fedha mtaani kwa njia isiyo na madhara yeyote nadhani hii ni mojawapo.

Serikali iwape watu pesa zao ni haki yao na jasho lao,kuwazungusha bila sababu za msingi hadi wengine wanapoteza maisha bila kuzipata ni wizi kama wizi mwingine wowote.

Wazee wamechoka wanahitaji kupumzika lakini bado wamekuwa wakipigwa danadana.
 
Tulikuwa tunaelekea huko....Rais wa wanyonge akatuona watumishi ni mabeberu. Akaunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii ukawa mmoja. Ushindani wa kibiashara na kihuduma ukafa. Akachukua matrilioni ya mafedha....wastaafu wakalia.
Mama Rais Samia aingilie kati hili nadhani litaboost boost hela mtaani hali imekuwa ngumu.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Umesema vema sana katika hili...najiuliza hivi kwanini serikali isiwafanyie wepesi wastaafu jamani...idadi ya vitu vinavyohitajika ili kupata hela ni nyingi..ila pia nimegundua vibgine vinaongezwa na wafanyakazi husika ili kuleta ugumu. Mimi nashauri wafanyakazi wote wa mifuko ya jamii wawe wanafanyiwa assessment na wanaowahudumia. Mambo ya Opras anayosema Raisi kweli hayafanyi kazi.

Swala liwe..kila anaehudumiwa lazima atoe mrejesho mara baada ya huduma..tena bila muhusika kujua. Na afisa rasilimali watu..aubde tume ya kufanya anaylysis hoja na yule mwenye kiwango kisichovumilika..afutwe kazi au ashushwe vitengo.

Sema tatizo afisa rasilimali watu wengi waliweka ndugu zao au watu waluwapa hongo ili wapate kazi...sijui kama watakuwa fair..ila ukweli secta hii haitaisha malalamiko kama wafanyakazi hawatabanwa watoe huduma kwa weledi
 
Hoja ni nzuri sana hususan kipengele cha kuruhusu mwanachama wa mfuko wa jamii husika kukopa angalau nusu ya pesa aliyohidhi katika mfuko huo ila kwa kuwa wanye mamlaka wanalipiwa hadi hela ya mboga majumbani mwao na walipa kodi hawatazingatia ushauri huu.
Laana iwe juu yao na vizazi vyao hata cha saba.
 
Umesema vema sana katika hili...najiuliza hivi kwanini serikali isiwafanyie wepesi wastaafu jamani...idadi ya vitu vinavyohitajika ili kupata hela ni nyingi..ila pia nimegundua vibgine vinaongezwa na wafanyakazi husika ili kuleta ugumu. Mimi nashauri wafanyakazi wote wa mifuko ya jamii wawe wanafanyiwa assessment na wanaowahudumia. Mambo ya Opras anayosema Raisi kweli hayafanyi kazi. Swala liwe..kila anaehudumiwa lazima atoe mrejesho mara baada ya huduma..tena bila muhusika kujua. Na afisa rasilimali watu..aubde tume ya kufanya anaylysis hoja na yule mwenye kiwango kisichovumilika..afutwe kazi au ashushwe vitengo. Sema tatizo afisa rasilimali watu wengi waliweka ndugu zao au watu waluwapa hongo ili wapate kazi...sijui kama watakuwa fair..ila ukweli secta hii haitaisha malalamiko kama wafanyakazi hawatabanwa watoe huduma kwa weledi
Umeshibisha Uzi kwa kuongeza nyama za kutosha Mkuu,nakuunga mkono kwa yote uliyoandika hapa

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Hoja ni nzuri sana hususan kipengele cha kuruhusu mwanachama wa mfuko wa jamii husika kukopa angalau nusu ya pesa aliyohidhi katika mfuko huo ila kwa kuwa wanye mamlaka wanalipiwa hadi hela ya mboga majumbani mwao na walipa kodi hawatazingatia ushauri huu.
Laana iwe juu yao na vizazi vyao hata cha saba.
Ni kweli bora wakopeshe tu coz unakuta hao hao NSSF wanaikopesha serikali inajenga majengo makubwa yasiyo rudisha pesa Leo wala kesho.

Hilo suala LA ujenzi ni LA serikali ambayo inachukua kodi,badala ya kuwainua wenye pesa zao ambao ni walalahoi pesa zinaenda kupewa tajiri tena anaezifanyia majukumu ambayo alipaswa kuyafanya kupitia kodi.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli bora wakopeshe tu coz unakuta hao hao NSSF wanaikopesha serikali inajenga majengo makubwa yasiyo rudisha pesa Leo wala kesho.

Hilo suala LA ujenzi ni LA serikali ambayo inachukua kodi,badala ya kuwainua wenye pesa zao ambao ni walalahoi pesa zinaenda kupewa tajiri tena anaezifanyia majukumu ambayo alipaswa kuyafanya kupitia kodi.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
Hizi pesa inafaa sana ziwanufaishe waajiriwa.
Nimewahi ona sehemu fulani ambapo taasisi binafsi imeanzisha kitu kama mfuko wa jamii. Kila mfanyakazi anakatwa angalau sh. 100,000 kwa mwezi na kuwekwa kwenye akaunti ya mfuko huo. Faida aliyonayo mwajiriwa ni fursa ya kukopa hadi mara tatu ya kiasi alichoweka kwenye mfuko. Mfano mtu aliyefanya kazi kwa mwaka mzima na kuweka sh. 1,200,000 ana fursa ya kukopeshwa sh. 3,600,000 ambayo riba yake ni asilimia 10 tu ambayo ni sh.360,000. Kifupi pale maisha yanasonga vizuri sana na watu wanatoboa ndani ya mwaka tu kwani wengi wana fursa ya kukopa angalau milioni 30.
Sasa watu wanaochangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii (NSSF, PSPF) waruhusiwe kukopa japo nusu tu ya pesa waliyoweka pale maana unakuta mtu kaweka milioni 30 kwa mfano ila maisha yake ni magumu sana kana kwamba hana hata senti kwenye mifuko hiyo.
 
Hivi kama umefanya kazi ya mkataba sehemu na baadae ukavunja mkataba kabla ya hatavmwaka mmoja, mafao yako unaruhusiwa kwenda kuchukua uliyoweka unaweza kuyapata kwa wakati??
 
Sasa watu wanaochangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii (NSSF, PSPF) waruhusiwe kukopa japo nusu tu ya pesa waliyoweka pale maana unakuta mtu kaweka milioni 30 kwa mfano ila maisha yake ni magumu sana kana kwamba hana hata senti kwenye mifuko hiyo.[/QUOTE]

Hapa ndipo penye tatizo na mm,lengo LA kufanya kazi ni ili kuboresha maisha yako,sasa kama unafanya kazi halafu maisha hayaboreki kuna maana gani??

Wanakuja kukupa pesa Uzeeni ilhali uko dhoofli hali ili zikusaidie nn??

Wanaokuja kuzitapanya hata hawajanisaidia chochote wakati nahangaika na shida zangu Ujanani.

Tuangalie namna ya kubalance hizi pesa ili ziwe na tija kwa walengwa.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Hivi kama umefanya kazi ya mkataba sehemu na baadae ukavunja mkataba kabla ya hatavmwaka mmoja, mafao yako unaruhusiwa kwenda kuchukua uliyoweka unaweza kuyapata kwa wakati??
Si kuna sheria ile walitaka kupitisha kuwa mpaka ufikie miaka 55 ya kustaafu ndio utapewa pesa yako.

Yaani kama uliajiriwa ukafanya kazi miaka kumi ukaacha na hujafikisha miaka hiyo 55 sijui 60 hupewi pesa yako ufike umri huo.

Kwa sasa nadhani unapewa ila ndio kwa kuzungushwa saaana,kama ulikuwa na shida na hiyo pesa kwa wakati Fulani unaweza kuimaliza hiyo shida kabla hujaipata hiyo fedha.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kitu ambacho hujui hiyo mifuko inatunza namba, ila fedha halisi hazipo. Kama wanashindwa kuwalipa wastaafu kwa muda ambao ni wachache kila mwaka itakua wakopeshe watu. Hamna pesa hapo na haitotokea wafanye hivyo kama tu FAO la kujitoa liliwashinda.
 
Kwako Mama yetu Mh Rais,

Mm nikiwa kama Shabiki yako namba moja,mkereketwa wako Kindaki Ndaki na mpiga debe wako niliejitolea kukusemea,kukutetea na kukuunga mkono Juhudi zako zote za kuliletea maendeleo taifa letu,Nina haya machache kwako nikiomba uyatupie jicho.
Kwanza

Wafanyakazi wa Nchi hii wanajituma sana ktk kufanya kazi ili kujikimu wao na familia zao,wakati huohuo wakisaidia kulijenga taifa kupitia kodi zao wanazokatwa kabla hata ya kuchukua mishahara yao.

Wamekuwa pia wakilipa kodi kila wakinunua bidhaa mbalimbali madukani,masokoni, kwenye vyombo vya usafiri nk.

Ikiwa yote hayo hayatoshi bado na sasa hivi Wafanyakazi wamekuwa wakilipa TOZO kwenye miamala yao wanayoifanya wanapohamisha fedha kwenda kwa ndugu zao na jamaa zao mbalimbali waliopo vijijini.

Wamekuwa wakifanya haya yote kwa moyo mmoja,bila kujali vipato wanavyopata ktk mishahara hiyo midogo isiyokidhi mahitaji,ila wameendelea kuwa watiifu wakitii mamlaka bila shuruti ukizingatia serekali ya awamu ya tano haikufanya nyongeza yeyote ktk awamu yake.

Pamoja na yote hayo ya kiwango kidogo cha mishahara ukilinganisha na mifumuko ya bei ya bidhaa mbalimbali nchini,TOZO,ulipaji wa kodi kwa wakati nk nk bado kuna suala LA mifuko ya Jamii kama vile NSSF,PSPF nk nk huko pia fedha zinakwenda kutoka kwenye mshahara wa huyu mfanyakazi.

HOJA YANGU ni kwamba nashauri hii mifuko ianzishe Mikopo kwa wafanyakazi ili hii mikopo iwasaidie kufanya mambo yao kama UJENZI wa Nyumba,Kufungua biashara ili kupunguza ukali wa maisha nk nk.

Kwa mfano,Mfanyakazi akiwa amechangia Million 30 aruhusiwe kukopa robo or nusu ya fedha zake ili aweze kufanya mambo yake ingali akiwa na nguvu sababu mnakuja kumpa MTU hela zake uzeeni ameshachoka na hana anachoweza kukifanya sababu nguvu zimeshamuishia na hela zenyewe nyingi.

Huyu MTU hawezi tena kufanya biashara,wala lolote na hapo ndipo wengine huitwa baby na kujikuta pesa zake zinatapanywa ilihali ujanani aliishi kwa tabu.

Faida ya kufanya hivi ni kwamba Hawa wafanyakazi wakishapewa hii mikopo wataizungusha na kuongeza mzunguko wa fedha kuisadia serikali katika suala LA uhaba wa ajira uliopo sasa.

Jambo LA Pili Mh Rais,ni kwa Hawa Wazee waliostaafu or walioacha kazi kwa namna moja ama nyingine wasicheleweshewe kupewa fedha zao,unakuta MTU amefanya kazi ana kadi ya Uanachama siku anataka apewe pesa yake anatakiwa alete barua ya Muajiri kuthibitisha Uajiriwa wake.

Sasa unajiuliza hizo fedha zilizopo kama michango zilikuwa zikilipwa na nani?na imekuwaje wakizipokea kama hawajui huyu MTU ameajiriwa ama Laa?

So Mh Rais Mama yetu kipenzi tunakuomba utupie Jicho hii mifuko ya Jamii Urasimu ni Mwingi pasipo sababu zozote za msingi.

Ni hayo tu Wasalaam
Arudishe FAO LA KUJITOA.Hata hivyo wao ndo walilutengeneza tatizo hawawezi kulitatua.CCM out wakati ukifika.
 
Mkuu KUFIKISHA milioni 30 kwenye mfuko wa hifadhi si kazi ndogo...majority wa watz hizo Ela wanafikisha kwa mbinde sana..landa useme akifikisha milioni Tano au kumi
 
Ccm ni laana..hawaezi ruhusu..mana hizo ndio hela za kununulia wapinzani na za kuhonga wapiga kura kipindi cha uchaguzi..na pia ndio za posho kwa polisi ili wawapige mabomu mkitaka kulinda kura zenu.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kitu ambacho hujui hiyo mifuko inatunza namba, ila fedha halisi hazipo. Kama wanashindwa kuwalipa wastaafu kwa muda ambao ni wachache kila mwaka itakua wakopeshe watu. Hamna pesa hapo na haitotokea wafanye hivyo kama tu FAO la kujitoa liliwashinda.
Kama wanatunza namba hizo fedha wanazokata zinapelekwa wapi?mana ni kila mwezi wanakata pesa kwenye mishahara yetu.

Back
Top Bottom