sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Mh Rais,na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi yetu, kwa tafrani hizi za utekaji hatupo salaam.
Wewe ndiye command in chief na pia ni comfort in chief, ukimya wako unaliweka Taifa njia Panda, huenda ndo maana wasio julikana wanahisi kuungwa mkono na serikali, hali inayo wafanya waitukanishe serikali yako kuwa haina mtandao mzuri wa ulinzi.
Iko wapi nguvu kubwa chini ya kamanda Sirro kama ilivyo tumika kule #MKIRU!!!
Umewajengea watendaji wako tendency ya kuwajibika mara wasikiapo sauti yako.
Sema neno sasa kukataa hali ya utekaji, onyesha una chukizwa na hofu iliyo tanda nchini ya #UTEKAJI, naamini ukisema hivyo kwa dhati ya moyo wako, mwisho wa utekaji utakuwa umefikia tamati.
Lakini pia wewe ni comforts in chief, mfariji mkuu wa wananchi mwenye kusimamia ustawi wa Taifa na wananchi wako .
Mara kwa mara umekuwa ukijitokeza kuwafariji wahanga wa matukio mbali mbali ,familiar zilizo athiriwa na majanga ya utekaji ni Watanzania pia, ni wapiga kura wako waonyeshe upo nao kwa kukemea matukio yanayo ichafua serikali yako.
Makundi haya yana haribu sifa na taswira ya serikali yako,ukizingatia wapo wanaojiita wanaharakati wa kukulinda, walioapa kuwaangamiza wakosoaji wako kwa kutumia jina lako.
Hii haikuweki kwenye sifa nzuri, zaidi ya kukuchafua.
Utawezaje kumlinda Rais anaye saidiwa na wananchi wake kuelekezwa mapungufu ya uongozi wake kwa kuumiza wananchi wasio na hatia.
#Viongozi wa dini, ninyi ni daraja la juu la kusimamia maadili, hatuwezi kuhubiri amani ilihali haki na wajibu wa kusimamia amani una kasoro.
Kwanini mna waogopa binadamu bila kukemea maovu 😢😢
Unganeni, toeni tamko kali ndani ya #CHRISTMAS hii kuonyesha chukizo la bwana kwa watu wake kabla hasira ya Mungu haijajidhihirisha ndani yetu.
Tuache kushinikiza makusanyo ya sadaka tu na kuliombea Taifa amani bila kutengeneza mazingira ya amani.
Amani ni tunda la haki, tumeshaichezea vya kutosha sasa tumekaribisha uhalifu wa kutekana.
Amani ni jukumu la kila mmoja, kwa kuwa mna wafuasi wengi hata watawala nao ni miongoni mwa wafuasi wenu semeni nao kwa hekima.
Hili ni jukumu lenu wote, si la Askofu Mwamakula au Askofu Bagonza ama sheik Ponda pekee yao. Viongozi wote wa dini mnapaswa kukemea hili.
Ikiwa mtatuacha tupotee, tukaamua kuyagomea makusanyiko yetu kwenye nyumba za ibada, mtamhubiria nani.
Tumerudi kwenye zama za mfalme Herode na Firauni, simameni kwa kutanguliza hofu ya Mungu, ili neno la bwana litamkwalo kwa mataifa lituponye na kuwaponya wenye mioyo migumu.
Tusijidanganye kuwanyamazisha wananchi kwa mujibu wa ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ndiyo wenye kutoa mamlaka na madaraka kwa serikali kutakuza uchumi.
Maridhiano, demokrasia na maendeleo havitengamani. Tusijidanganye kwa hali tete ya UTEKAJI tutakuza uchumi, hofu hufisha Taifa.