Rais Mwinyi: Watu wanadhani kuweka kodi kubwa ndio pato kubwa kwa Serikali, kodi kubwa inapunguza wafanyabiashara

Rais Mwinyi uko sahihi kabisa, Chukua hatua, Chukua Sheria za biashara na kanuni za jimbo la Texas Nchini Marekani na hamishia Zanzibar ndani ya mwaka moja tu utakataa wawekezaji na mitaji itakayoingia Zanzibar itakua haina idadi, usisubiri watumishi kukuletea changamoto kutoka kwa Wafanya biashara, kwani hao watumishi wenyewe hawajui tabia na lugha ya kibiashara. Mungu akuongoze na akupe hekima.
Mzee jazia nyama kuhusu Texas. Mh. Mwinyi yupo humu anakusoma.
 
Tatizo la serekali hizi ni kwamba HAKUNA MPANGO RASMI NA WA KUDUMU WA KIBIASHARA UNAOWEKWA KWENYE MFUMO RASMI AMBAO HATABADILIKA KWA 25 YEARS KILA KIONGOZI ANYEINGIA ANATEKENYA MFOMO NA KUWEKA ATAKAVYO YEYE HILI HUARIBU MALENGO NA GUARANTEE KWA INVESTA INVESTA HAPENDI SHAKINGS ZA KIPUUZI dr kitila hongera najua upo huku tengenezeni sera rafiki za wafanyabiashara na investor za muda mrefu unshaked kwanza baada ya hapo anza sasa kutangazia wawekezaji
 
Anazaliwa Baba tayari ni Balozi,

Uongozi upo kwenye bone narrow, Maisha yake yote ya utotoni Baba yupo kwenye Utawala, Baba anatundika Gloves yeye anaingia

Wenzangu na sie ukipata uteuzi ndio unaanza kujifunza kufunga tai kwa mara ya kwanza kwanini usione Binadam wenzio wote Kuku?
Nimesoma hii nikasema ni wewe kweli?...big up!!
 
Asante kwa busara na hekima
kuna kitu kinaitwa Equity and efficiency.
Equity, unachokifanya unaweka kodi kuwa kwa wafanya biashara, then hizo kodi zinazopatikana zinaingia kusaidia huduma za jamii, kutoa mikopo kwa wajisilia mali wadogo, kutoa elimu bure, kutoa huduma kwa jamii, na kujenga barabara, kutoa ruzuku na kulipa mishahara. Sio kitu kibaya nayo mbinu nzuri tu ya kiuchumi. Na mbinu hii hupunguza matabaka ya kiuchumi kwenye jamii. Fuatilia Tax double effect of Tax obama (rich man tax, capital gains, and inheritance duty)
 
Nikiongoz Mzuri Sana Ila shida regulation sina uhakika atafanikiwa kivile maana Znz kuna ZRB na TRA. Bad enough BOT ndio regulator Kwa bara na visiwani. Je anatoka vipi?
Soma vizuri ndugu juu ya kazi za BOT. Hiyo ni central bank ya Tanzania. Mambo ya fedha ni ya Muungano katika sarafu ingawa tuna wizara mbili za fedha ambazo BOT huwajibika nazo. Monetary Policies baina ya bara na Zanzibar hutumia interventions tofauti ndio maana wao wana mfumuko wao wa bei na bara wanareport peke yake. Zanzibar kwa hiyo wana semi autonomy inayowafanya wafanye maamuzi kwenye mambo yao yanyoihusu biashara ya Zanzibar
 
Anazaliwa Baba tayari ni Balozi,

Uongozi upo kwenye bone narrow, Maisha yake yote ya utotoni Baba yupo kwenye Utawala, Baba anatundika Gloves yeye anaingia

Wenzangu na sie ukipata uteuzi ndio unaanza kujifunza kufunga tai kwa mara ya kwanza kwanini usione Binadam wenzio wote Kuku?
 
Leo Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ameitisha kikao na wafanyabiashara na kuongelea changamoto zinazoikabili sekta ya biashara Zanzibar na muelekeo wa kuzitatua. Kikao hiko kimehudhuriwa na wafanyabiashara pamoja na mawaziri wa serikali ya Zanzibar

Pamoja na mambo mengine, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema hatafuatilia wafanyabiashara waliokwepa kodi kipindi cha nyuma lakini kuanzia sasa wote walipe kodi.

Huu ukiwa utaratibu tofauti sana na aliotumia Rais wa Jamhuri, Dkt. John Magufuli alipoingia madarakani kwa kufukua makaburi ya makontena yaliyoingizwa kupitia bandari na wahusika kutakiwa kulipa tofauti ya kodi yote iliyoonekana kukwepwa kwenye awamu iliyotangulia. Wapo walioshindwa na kampuni zao kufa na wengine kuonja chungu ya gereza kwa makosa ya uhujumu uchumi.

========

MWINYI: Zipo tabia za kufanya mikutano mingi bila ufumbuzi, mimi katika utawala wangu tabia hiyo sitoitaka. Tunapokutana, ninapozungumza changamoto ikawekwa, mkachukua halafu mkawa hamjazifanyia kazi ni kupoteza muda na mimi nataka niwaambie watendaji wote serikalini kwamba nina ahadi na wananchi ya muda wa miaka mitano, sina muda wa kupoteza, lazima tufanye kazi hii kwa haraka, lazima tujitahidi kuondoa changamoto zote na zile ambazo zitakuwa ngumu kwenu, mimi nipo, nileteeni nitahahakisha tunazimaliza.

Lengo la mkutano huu nimeuitisha kwa madhumuni ya kuwahakikishieni wafanyabiashara kwamba serikali yangu itatoa msukumo mpya katika kutatua changamoto zinazokabili biashara Zanzibar.

Ahadi yangu kwenu ni kuondoa changamoto zote zinazokwamisha biashara hapa Zanzibar. Najua kuna changamoto ya kodi mathalan, mimi sio muumini wa masuala ya kuweka kodi kubwa kwa sababu watu wanadhani kuweka kodi kubwa ndio pato kubwa kwa serikali, ni kinyume chake.

Kodi kubwa inapunguza wafanyabiashara, watakaofanya biashara kwa kodi kubwa ni wachache lakini tukipunguza kodi watakaofanya biashara ile ni wengi. Lakini serikali haiishi kwenye kodi tu.

Tukiweka kodi ndogo maana yake kuna watu nje ya Zanzibar watakuja kufanya shopping hapa Zanzibar, hoteli zetu zitajaa, teksi zetu zitakuwa na wateja, migahawa yetu itajaa, hiyo itaongeza mzunguko wa fedha katika uchumi.

Uchumi wetu utaendeshwa na sekta binafsi, ahadi kwenu ni kwamba serikali itaweka mazingira rafiki ya kufanya biashara na tutaondoa urasimu, tutaondoa rushwa, tutaondoa vikwazo vyote vinavyosababishwa na utendaji katika serikali. Maono yangu ni kuifanya Zanzibar iwe kituo cha biashara katika ukanda wetu. Mwenyezi Mungu ametujaalia tupo katika jiografia nzuri sana, tuna uwezo wa kuwa kitovu cha biashara.
Huyu jamaa kumbe anafikiri vizuri sana. Kama kwa Zenji inayotegemea utalii kwa asilimia kubwa, kukiwa na unafuu wa kodi kutavutia wateja na multiplier efect itakiwa kubwa. Amengalia mambo holistically, akienda hivi Zanzibar itasonga mbele kwa haraka sana.
 
Back
Top Bottom