Rais Mwinyi: Watu wanadhani kuweka kodi kubwa ndio pato kubwa kwa Serikali, kodi kubwa inapunguza wafanyabiashara

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,804
Leo Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ameitisha kikao na wafanyabiashara na kuongelea changamoto zinazoikabili sekta ya biashara Zanzibar na muelekeo wa kuzitatua. Kikao hiko kimehudhuriwa na wafanyabiashara pamoja na mawaziri wa serikali ya Zanzibar

Pamoja na mambo mengine, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema hatafuatilia wafanyabiashara waliokwepa kodi kipindi cha nyuma lakini kuanzia sasa wote walipe kodi.

Huu ukiwa utaratibu tofauti sana na aliotumia Rais wa Jamhuri, Dkt. John Magufuli alipoingia madarakani kwa kufukua makaburi ya makontena yaliyoingizwa kupitia bandari na wahusika kutakiwa kulipa tofauti ya kodi yote iliyoonekana kukwepwa kwenye awamu iliyotangulia. Wapo walioshindwa na kampuni zao kufa na wengine kuonja chungu ya gereza kwa makosa ya uhujumu uchumi.

========

MWINYI: Zipo tabia za kufanya mikutano mingi bila ufumbuzi, mimi katika utawala wangu tabia hiyo sitoitaka. Tunapokutana, ninapozungumza changamoto ikawekwa, mkachukua halafu mkawa hamjazifanyia kazi ni kupoteza muda na mimi nataka niwaambie watendaji wote serikalini kwamba nina ahadi na wananchi ya muda wa miaka mitano, sina muda wa kupoteza, lazima tufanye kazi hii kwa haraka, lazima tujitahidi kuondoa changamoto zote na zile ambazo zitakuwa ngumu kwenu, mimi nipo, nileteeni nitahahakisha tunazimaliza.

Lengo la mkutano huu nimeuitisha kwa madhumuni ya kuwahakikishieni wafanyabiashara kwamba serikali yangu itatoa msukumo mpya katika kutatua changamoto zinazokabili biashara Zanzibar.

Ahadi yangu kwenu ni kuondoa changamoto zote zinazokwamisha biashara hapa Zanzibar. Najua kuna changamoto ya kodi mathalan, mimi sio muumini wa masuala ya kuweka kodi kubwa kwa sababu watu wanadhani kuweka kodi kubwa ndio pato kubwa kwa serikali, ni kinyume chake.

Kodi kubwa inapunguza wafanyabiashara, watakaofanya biashara kwa kodi kubwa ni wachache lakini tukipunguza kodi watakaofanya biashara ile ni wengi. Lakini serikali haiishi kwenye kodi tu.

Tukiweka kodi ndogo maana yake kuna watu nje ya Zanzibar watakuja kufanya shopping hapa Zanzibar, hoteli zetu zitajaa, teksi zetu zitakuwa na wateja, migahawa yetu itajaa, hiyo itaongeza mzunguko wa fedha katika uchumi.

Uchumi wetu utaendeshwa na sekta binafsi, ahadi kwenu ni kwamba serikali itaweka mazingira rafiki ya kufanya biashara na tutaondoa urasimu, tutaondoa rushwa, tutaondoa vikwazo vyote vinavyosababishwa na utendaji katika serikali. Maono yangu ni kuifanya Zanzibar iwe kituo cha biashara katika ukanda wetu. Mwenyezi Mungu ametujaalia tupo katika jiografia nzuri sana, tuna uwezo wa kuwa kitovu cha biashara.
 
Huyu ndiye Rais anayeweza kutumia busara na hekima.

Siyo huyu Jiwe anayependa kuwakomesha wafanyibiashara kwa kuwalundikia kodi zisizoweza kulipika na hivyo kufilisika na kuikimbia nchi yetu na kwenda kuwekeza nchi za nje na serikali kukosa kodi na hivyo kuanza kufilisika
 
Back
Top Bottom