Rais Mwinyi hongera sana kuchaguliwa lakini mulika idara zako za Serikali hasa Elimu na Ardhi

pasi padinde

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
282
299
Shikamoo kiongozi,

Wakristo zanzibar wanapata shida sana naomba hili ulimulike kwasababu ya mambo ya dini.

Mfano ukitaka kujenga shule na wewe ni mkristo yaani utazungushwa mpaka miaka miwili mpaka mitano kwa kigezo kwamba wakristo wamekuja kuanzisha shule ili wawabadilishe watoto wa kiislamu wawe wa kristo na inafika mpaka wizarani kuna kuwa na urasimu usio na miguu wala kichwa.

Kuhusu ardhi hakuna mtu atakupa ushirikiano ukianzia ngazi ya chini mpaka juu na hasa kama unataka pengine ujenge kanisa.

Kuna watu wanalalamika sana naomba ulitazame hili.
 
Umekuja na mtumbwi juzi tu kuanzia mwezi wa 10 kwaio huyajui.... Hakuna aliezuiliwa kuanzisha shule Zanziba kwa kuwa eti ni ya kikristo.... Kuna international schools ambazo ni wazungu wanamiliki, kuna shule ya kikristo inaitwa ST. Francis Zanzibar kama hujui.

Kuhusu kujenga kanisa, Makanisa madogo madogo yamejaa yakutosha, kuna moja inajengwa Jumbi inaonekana haijapata watu wa kutosha kuchangia ujenzi.

Sababu ya kutokuwepo shule nyingi za kikristo ni very simple logic. 90+ ya wazanzibari ni waislam, watapeleka watoto wao shule aidha za kiislam ama ambazo hazina mlengo wa dini, wakristo nao pia wanapeleka watoto wao shule zilizokuwa hazina mlengo wa dini sasa kujenga school specific for wakiristo doesnt make sense hasa ukizingatia kuwa wakiristo wenyewe hawazipi kipaumbele na wanapeleka watoto wao huko kwengine.
 
Wewe acha hayo nimeonyeshwa nyaraka kwakweli wakristo wanaumizwa sana zanzibar

St Fransis mpaka walijenga ukuta kila uchwao wanarushiwa mawe na wakalazimishwa wajenfe msikiti ndani ili watoto wa kislam wawe wanasali huku eneo ni la Roman Catholic. Hivi mashule ya kiislam yana eneo la kusali wa kristo?

Pili ukienda pale ardhi kila shule ya kikristo wanalazimisha iwe na kitu kinaitwa lizi je mashule ya kiislamu wanayo?

Ukiona makanisa ya kikristo zanzibar mengi yamejengwa kibishi kwa kusema liwalo na liwe baada ya msoto mkubwa wa kuzungushwa.
 
Umekuja na mtumbwi juzi tu kuanzia mwezi wa 10 kwaio huyajui.... Hakuna aliezuiliwa kuanzisha shule Zanziba kwa kuwa eti ni ya kikristo.... Kuna international schools ambazo ni wazungu wanamiliki, kuna shule ya kikristo inaitwa ST. Francis Zanzibar kama hujui...
Waislamu wengi hao hao hawapendi shule za kiislamu kwasababu hakuna content yeyote ya kielimu na wanakimbilia mashule ya kikristo
 
Wewe acha hayo nimeonyeshwa nyaraka kwakweli wakristo wanaumizwa sana zanzibar...
Hayo yakurushiwa mawe naona ndio nakusikia wewe. Shule ya kiislam ijenge kanisa ndani la dhehebu gani? hao wanaosali humo kina nani kama shule haina wakiristo?

Hakuna kanisa lilojengwa kiubishi Zanzibar, ukiona limejengwa ujue lina baraka za serikali.

Mgeni haruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar. Hata mahoteli wanalipia Lease, tena haijaalishi mmiliki nani
 
Hayo yakurushiwa mawe naona ndio nakusikia wewe. Shule ya kiislam ijenge kanisa ndani la dhehebu gani? hao wanaosali humo kina nani kama shule haina wakiristo?...
Ina maana sisi wa Tanganyika tukija Zanzibar tunakuwa wageni?
 
Hata tanzania bara wakristo romankatolik wamepewa viwanja vikubwa sana kujenga makanisa tofauti na waisalamu angalia kanisa msimbazi dar eneo lake ni kubwa sana hakuna hata eneo kama hilo wanalo waislam na sio msimbazi dar pekee nenda dodoma ukianza kuingia kutoka dar unapokelewa na maeneo makubwa ya makanisa na mashule zina uwanja mkubwa mpaka unaingia mjini tanzania nzima makanisa yametawala ardhi zenye eneo kubwa sana kuliko waislamu
 
Ili umiliki ardhi, unatakiwa uwe na kitambulisho cha mzanzibari. Maana yake, wewe ni kama foreigner Zanzibar. Utalipia ardhi kama anavyolipia mtaliana.
Hapo kuna haja gani ya muungano kwanini tusiuvunje tubaki na mataifa mawili?
 
Back
Top Bottom