Rais Mwinyi: Hatutaki masihara kwenye vita dhidi ya ubadhirifu, rushwa na wizi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema nguvu inayotumika kupambana na wabadhirifu wa mali za umma visiwani humo si nguvu ya soda na mapambano hayo ndio kwanza yameanza.

Kadhalika, amesema wizi, ubadhirifu wa mali za umma ni mambo aliyoyavalia njuga na hataki masihara na kusisitiza kuwa ataendelea kuondoa muhali ili wale wote wanaohusika au waliohusika kwenye ubadhirifu wachukuliwe hatua.

Dk Mwinyi aliyasema hayo jana Ikulu mjini Zanzibar wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa vyombo vya habari Tanzania kuhusu siku zake 100 madarakani.

“Mimi wale wenye makosa makubwa ndio nawataka kwa hivyo nimeshatoa maagizo kabisa kwenye vyombo vyote kwamba hakuna mdogo, hakuna mkubwa lakini hususani hawa wakubwa…kwa hivyo ni vyema tukapeleka nguvu kubwa kwenye watu tunaowadai pesa nyingi na hili litafanywa hivyo ili tuondokane na kutumia rasilimali zaidi ya kile tunachokidai,” alisema Dk Mwinyi.

Rais Mwinyi alizungumzia mambo 10 yaliyofanyika ukiwemo uwajibikaji na utawala bora na kusisitiza kuwa nguvu inayotumika kupambana na wabadhirifu wa mali za umma.

“Vita dhidi ya rushwa, ubadhirifu, wizi wa mali ya umma nimelivalia nguja, hatutaki masihara kwenye hili, nilisema wakati kampeni kuwa nitaondoa muhali hapa Zanzibar na kweli nimeondoa, kwa sababu nimechukua hatua kila penye kasoro, wengine walisema ni nguvu ya soda, lakini ndio kwanza nimeanza mtasikia mengi vita ya rushwa ni suala la kudumu,” alisema Dk Mwinyi.

Alisema kulikuwa kuna ubadhirifu mkubwa na hivi karibuni zaidi ya watumishi 80 walisimamishwa kazi baada ya kuthibitika walihusika kucheza na mitandao ya serikali ya mapato na wengine kula rushwa.

“Kuna watu wamesharudisha fedha, nimeambiwa na ZAECA katika orodha yao kuna watu wamerudisha fedha nilichowaambia ni kwamba, mtu aliyerudisha fedha kama ni kwa makubaliano arudishe halafu asishitakiwe basi angalau afukuzwe kazi. Huwezi kuwa na mwizi akarudisha basi aendelee, atakuibia tena,” alisema Dk Mwinyi.

Alisema Wazanzibari wasiwe na wasiwasi kwa kuwa watu wote waliochukua fedha za serikali watazirudisha na bado kuna kesi za fedha nyingi ZAECA na nyingine zipo mahakamani.

Kuhusu uadilifu na uwajibikaji wa watumishi wa umma, alisema kila aliye katika utumishi wa umma lazima awe mwadilifu na kuwa wale wote walioiba mali za umma watazirejesha na kwamba wapo walioanza kuzirejesha.

“Kwenye makosa yote ni sawa madogo na makubwa lakini nimeviagiza vyombo vyote kuweka nguvu zaidi kwenye makosa makubwa kwa tuelekeze nguvu huko kwa sababu wakati mwingine unaweka mkazo kwenye kosa dogo mtu anadaiwa shilingi elfu ishirini wakati kuna wengine wana kesi za mabilioni, lazima tuweke mkazo kwenye kesi kubwa ambazo hata gharama za kuziendesha zinawiana au fedha tunazodai ni kubwa zaidi,” alisema Dk Mwinyi.

Alisema vita dhi ya maovu katika jamii ukiwemo udhalilishaji ni kubwa na akaomba wananchi kushiriki kwa sababu bila ushirika ni ngumu kupigana vita hiyo mwenyewe.

Aligusia pia maslahi ya watumishi wa umma na kusema serikali iko mbioni kuongeza maslahi ya wafanyakazi wakati kwa kuwa wale wa kima cha chini walishaongezewa maslahi hayo kwenye serikali ya awamu iliyopita.
 
Kuna lile swali aliloulizwa kuhusu Maalim seif,alijibu nini ?maana nilipitwa na hiyo sehemu.
 
Wabadhirifu wa mali za umma na ufisadi nchi hii wote huwa wanatokea "CCM", hicho chama ndio Chuo Kikuu cha ufisadi na ujambazi.

Nasema uongo ndugu zanguuuu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom