Rais Mwinyi atoa onyo kwa watakaopandisha bei ya bidhaa Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amewanasihi wafanyabiashara kuacha kutumia mgogoro wa Urusi na Ukraine kama kisingizio cha kupandisha bei za bidhaa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Dk. Mwinyi alieleza hayo jana katika risala maalum aliyoitoa yenye lengo la kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa mwaka 1443 hijria, aliyoitoa kupitia vyombo vya habari.

Alisema serikali hatua haitosita kuwachukulia kali wafanyabiashara kinyume na maagizo inayoyatoa, kwani amepata taarifa kwamba bidhaa nyingi zitakazouzwa kwa kipindi cha mwezi wa Ramadhani zimeingizwa nchini kabla kuibuka kwa mgogoro wa Urusi na Ukraine.

Dk. Mwinyi aliwahakikishia wafanyabiashara na wananchi kuwa Serikali itaendelea kufuatilia mwenendo wa uchumi wa dunia na gharama za kufanya biashara duniani, ili kuhakikisha kwamba bei za bidhaa zinazouzwa kwenye maduka ya jumla na rejareja zinaakisi gharama na uwezo wa kipato cha wananchi.

Aliwahimiza wakuu wa taasisi zinazoshughulika na biashara, mikoa, masheha, wahakikishe wanafuatilia wakuu wa wilaya na kwa karibu mwenendo wa bei za bidhaa katika maeneo yao ya utawala na kuwachukulia hatua za kisheria wanaojaribu kukiuka sheria na maagizo ya serikali.

Alisema kuwa wakati wa Ramadhani ukikaribishwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa dunia bado haiko katika hali ya kawaida, kama ilivyokuwa kabla ya kuzuka kwa janga la UVIKO 19, mwishoni mwa mwaka 2019.

Aliongeza kuwa pamoja na kuendelea kuwepo kwa changamoto zilizoambatana na maradhi hayo, hivi karibuni mgororo wa vita baina ya Taifa la Urusi na Ukraine umeibua taharuki mpya kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii duniani kote.

Alieleza kuwa kwa kuzingatia hali ya uchumi nchini pamoja na uchumi wa dunia kwa jumla amekuwa akiitisha vikao na watendaji wa taasisi mbali mbali za Serikali kwa lengo la kujadili maendeleo ya biashara nchini ambapo amekuwa akitoa maagizo na maelekezo yenye lengo la kudhibiti hali ya upandaji wa bei za vyakula, mafuta ya petroli na bidhaa nyengine muhimu.

Dk. Mwinyi alisema kuwa kwa kipindi cha mwezi wa Ramadhani, serikali imepunguza viwango vya kodi kwa bidhaa muhimu ambapo yaliyofanywa yamezingatia maslahi maamuzi katika suala hilo ya wananchi na wafanyabiashara ambapo serikali imeweka bei elekezi.

Chanzo: Zanzibar Leo
badilisha title. Unadai ametoa onyo kisha content unasema amewasihi-begged.....??
 
Ukweli ni kwamba haijalishi kama ametoa onyo au amewasihi, bei hazitashuka kwa sababu hizo. Uchumi haubadilishwi kwa maonyo au kusihi wafanyabiashara.
badilisha title. Unadai ametoa onyo kisha content unasema amewasihi-begged.....??
 
Sasa huyu Tunaemuita Rais wa JAMHURI ya muungano wa TANZANIA 🇹🇿 ni tanzania ipi sasa
 
Huu wimbo kila mwaka unaimbwa imekuwa kama routine. Impact yake haionekani. Isitoshe urais wa Zanzibar na Ramadhan vina uhusiano gani?
Rais moja ya kazi zake NI kuuendeleza Mila thilka na Urithi WA Nchi yake RAMAZAN NI ktk utamaduni wetu thilka yetu na ishara ya Nchi yetu
Hivyo Basi ikisha Mfungo Rais anakwagua gwaride na ana hutubia Baraza la IDI
Iko hivyo ukitaka usitake ukipenda usipende ukifurahi ukinuna

Na jengine nikwambie RAIS WA ZANZIBAR kuna siku mbili huwa ana toka full scoter yaani migari na mipikipiki kama yote
MAPINDUZI DAY na
EID DAY

Endelea kumeza viwembeeee
 
Huyu wa bara sioni hata kitu kimoja alichofanikiwa. Muhimu kuangalia vitendo / matendo na kauli zake zimejaa taarabu, visingizio, mipasho.

Toka aingie haya ni matokeo ya utawala wake:-

Mfumuko wa bei, kuongozeka matatizo umeme, maji, mbolea madawa ya kulevya, kuwafungulia wauza sembe, kuanzisha tozo, kuchukua mikopo kwa mambo yasiyo na tija.

Teuzi, tenguzi, ufisadi, na mafisadi kurudishwa rasmi kuongoza CCM na serikali, gharama za chakula, ujenzi, usafiri kuongezeka, nidhamu serikalini kushuka, udini.

Mafanikio yake mengine ni masoko kuchomwa moto usiku, ajali za magari za kutisha kila siku, polisi kuongeza uporaji wa mali za raia na kuua raia, machinga, mama ntilie kufukuzwa bila kuwapa alternative, uwiano wa kitoto na upendeleo wa wazi wa vyeo, pesa, ajira kwa watu wa Zanzibar.

Mkakati wa kuwafukuza wamasai na kuuza eneo lao la Loliondo kwa majangiri wa UAE kuwinda na kuua wanyama muhimu, nyara za serikali, urithi wa Watanzania na vizazi vijavyo., Kasi ya kujenga na kuendeleza miradi ya kimkakati imepungua sana. Ukiritimba, rushwa, kucheleweshwa vimerudi kwa kasi Bandarini, kemikali zinatiririka huko Mara ndani Ziwa watu mifugo na samaki wanaumwa na kufariki, tume inakuja na sababu / majibu ya ajabu ajabu, Rais yuko kimya.

Kwa vitendo na kauli zake naonekana hajali maisha ya Watanzania wengi hana uwezo wala malengo, maono, mikakati, nia ya ukweli / dhati, uthubutu wowote na nchi hii zaidi ya kutawala for the sake of kutawala.
Dah.....kwa kifupi Sir 100 kashindwa udereva....2025hrs tumkatae.....imetosha 🤭
 
Back
Top Bottom