Rais Mwinyi ataka wataalam wa Kiswahili waandike sera na sheria kwa Kiswahili

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa wito kwa wataalamu wa lugha ya Kiswahili kutumia taaluma yao.

Amewaambia wataalamu hao wahakikishe sheria na sera za serikali zinakuwa katika lugha ya kiswahili ili kuwazesha wananchi kuzifahamu vyema.

Hali ilivyo hivi sasa baadhi ya sera na sheria zimeandikwa kwa lugha ya Kiingereza.
 
Huku bara wanakazana kurekebisha sheria! Kwa rugha zile zile za mabeberu.

Nilimsikia kiongozi mmoja akisema sheria lazima ziwalinde wanyonge. Zinakulindaje wakati ww unaetaka zikulinde huzijui.

Weka sheria na kanuni kwa kiswahili harafu uone wenye tutai km mianvuri watazungusha kesi za watu.
 
Mi nashangaa huku bara, kuna watu wana ma PHD lakini hayajasaidia wanyonge zaidi ya kuumiza.
Utasikia ana PHD ya sheria. lakini hawezi kuitafsiri sheria kwa kiswahili.

Ukienda china, nikichina ,kuanzia kula ,mpaka kujamba. Utasikia kipindi redioni eti...Tunu, namoja ya tunu za nchi hii nipamoja na kiswahili.

Eti rug'ha ya taifa nikiswahili, lakini Mahakama chombo muhimu cha kutoa haki kwa mtanzania wanatumia rug'ha ya mabeberu.
 
Back
Top Bottom