Rais Mwinyi ana hoja nzito. TRA na ZRB wabadilishane taarifa kudhibiti wakwepa kodi KMKM na TRA nao watumbuliwe

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,904
Raisi Mwinyi ana hoja nzito sana TRA na ZRB wabadilishane Taarifa na wafanya kazi pamoja kudhibiti wakwepa kodi

Mfano alitoa ni kuwa lita za mafuta milioni 50 zililetwa Tanzania bara toka Zanzibar mwenyewe mwenye Lita zake akasema hawezi lipa kodi Tanzania bars sababu zimetokea Zanzibar lakini kule nako hakulipa kumbe !!

TRA vizuri iwe inawapa takwimu ZRB za bidhaa zilizotoka bara kwenda Zanzibar na ZRB itoe takwimu za bidhaa zilizotoka Zanzibar kwenda bara na kama zililipiwa kodi upande husika au LA.Ripoti wasiishie tu kubadilishana copy ziende ofisi kama hazina za pande zote mbili

Huo mchezo unaonyesha umechezwa muda mrefu hasa kwa bidhaa za kutoka Zanzibar

Swala jingine ni je kikosi cha KMKM kazi yake nini hasa kuhusu hili swala LA lita milioni 50 kuondoka Zanzibar bila kulipiwa Kodi? Hayo ni magendo.Na ni kazi pia ya KMKM kudhibiti magendo nao napendekeza watumbuliwe

TRA nao je mtu akishasema Mimi ushuru ulilipwa Zanzibar inatosha kusema kwa mdomo tu hakuna verification yoyote ya kufanya kujihakikishia hilo ili kama hajalipa alipe? Swala LA hizo Lita 50 milioni TRA nako kuna watu wanatakiwa watumbuliwe .Mwinyi kamaliza ZRB kutumbua mpira uko Tanzania bara kuna watu TRA wanatakiwa kutumbuliwa
 
Hapo ni siasa tu na drama, written, edited and directed by them but watched and cheered by us!

Tatizo ni kuwa wao wana sera na system mbovu ya ulipaji kodi na utekelezaji wake. Utanunuaje TV au fridge kutoka ZNZ kwenda Dar la matumizi binafsi uambiwe ulipe kodi ya forodha wakati risiti ya manunuzi unayo? Kama muuzaji hajalipa kodi si wakamkamate yeye si wanamjua?

Hayo mafuta ( ya kula) yanalipiwa kodi ZNZ (ya kizanzibari) na huku yakija yanalipiwa kodi (difference), tatizo ni kuwa makusanyo yanaingia mifukoni mwa wakusanyaji kodi na hili sote tunajuwa. They need to fix this shit!
 
Kwa nchi zetu hizi za africa kuna viongozi aina ya Mwinyi utokea mara moja sana.

It’s a shame sio rahisi wa Tanzania angebadili sana fikra za wafanyakazi serikalini na hili ni tatizo kubwa.

Waafrica wanaaamini siasa ni sehemu ya kupiga deal ukiwaachia tu kama mama anavyofanya utosikia kelele za matatizo, na ukiwauzia watu wakifa huko raisi kawatuma, jeshi la polisi likikosea raisi kawatuma.

Sikuhizi mikutano ya katiba kila siku polisi wanaifungia na watu wanabebwa wala usikii anauwa demokrasia, yote watu wamerudi kula hela za watanzania maskini hiko tu ndio wanachotaka.
 
Bilashaka Saimia atafanya jambo hapa na natamani kusikia mahakama ya uhujumu uchumi ikimchukulia hatua na kumfungulia mashtaka mfanyabiashara husika.

Na Watanzania wanatamani kusikia takukuru imemkamata mfanya biashara huyo na ahojiwe pia asipewe dhamania.
 
Mwinyi tunamuhitaji sana huku bara kuliko wakati wowote, amalizie muda wake kule ahamie huku ni Rais Bora kabisa na anatufaa
 
Back
Top Bottom