Rais Mwinyi aagiza Taasisi, Wizara kutoa ushirikiano kwa Vyombo vya Habari

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Hussein Mwinyi ameziagiza taasisi na maofisa uhusiano kukaa pamoja na kuangalia namna bora ya kutoa taarifa kwa vyombo vya habari tofauti na ilivyo sasa.

Pia ameziagiza wizara zote kuanza kutoa taarifa za shughuli zao kwa waandishi wa habari ili kuujulisha umma masuala mbalimbali yanayofanywa na Serikali.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Machi Mosi, 2021 wakati akifungua kongamano la kujadili matumizi ya sekta ya mawasiliano ya habari katika kuijenga Zanzibar mpya mjini Unguja

"Naagiza leo wakuu wa taasisi na maofisa uhusiano wote kaeni pamoja mwangalie namna nzuri ya kuwa mnatoa habari kwa waandishi wa habari ili umma ujue," amesema.

Amesema sekta ya habari ni kiungo muhimu kuchochea maendeleo na kuleta ustawi wa jamii.

Amesema kwa kipindi kifupi ambacho ameingia madarakakani amebaini kuna changamoto nyingi zinazowakumba wananchi lakini wanakosa njia bora za kuziwasilisha sehemu husika kwa kukosa muunganiko mzuri.

Awali mshauri wa vyombo vya habari, Suleiman Seif amesema sekta ya habari inakabiliwa na changamoto lukuki hivyo yapo mapendekezo kadhaa yanayotakiwa kuingizwa kwenye muswada wa sheria ya huduma za habari ya mwaka 1984.

"Kwenye muswada mahakama iweke wazi kwamba habari zinazofichwa kwa madai ya maslahi ya umma ndio habari za namna gani," amesema.

Amesema pia kuna jambo la baadhi ya taasisi kumlazimisha mwandishi wa habari ataje vyanzo vya habari yake jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Chanzo: Mwananchi
 
Anachokisema wa huku bara na yeye Mwinyi hua anaki copy fasta tu,ajaribu kua original.
 
Anachokisema wa huku bara na yeye Mwinyi hua anaki copy fasta tu,ajaribu kua original.
If everyone is thinking alike, then someone isn't thinking.

Kuna mmoja amewaza kisha akasema, na kuna mmoja amesikia mawazo ya mwenzake naye akayabeba na kuyasema jinsi yalivyo.
 
Back
Top Bottom