Rais mwenye mawazo ya kuombaomba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais mwenye mawazo ya kuombaomba!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 2, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Sehemu ya hotuba ya Rais Kikwete inayothibitisha kuwa hana mawazo ya kuinua hali ya maisha ya watanzania bila ya kukinga mikono kwa nchi matajiri; asilimia 99 ya mambo anayotaka nchi matajiri zifanye kwa Afrika yanaweza kufanywa na Afrika wenyewe!

  Namnukuu:

  Mkutano wa G-20
  Ndugu Wananchi;
  Jambo la mwisho ambalo ningependa kuliongelea leo hii ni kuhusu msukusuko wa uchumi wa dunia na hasa mkutano wa Kundi la Nchi Ishirini Tajiri Duniani (G-20) ambao unategemewa kufanyika kesho tarehe 2 Aprili na kumazika tarehe 3 Aprili, 2009 mjini London, Uingereza. Mkutano huu umeitishwa kutafuta njia za pamoja za kukabili kudorora kwa uchumi duniani.

  Mataifa haya tajiri ishirini, ambayo yanamiliki asilimia 85 ya uchumi wa dunia ni pamoja na Marekani, Uingereza, China, Japan, Ujerumani, Ufaransa, Afrika ya Kusini, Australia, Uturuki, Brazil, Canada, Argentina, Mexico, Indonesia, India, Italy, Urusi, Korea Kusini, Umoja wa Nchi za Ulaya na Saudi Arabia.

  Ndugu Wananchi;
  Uchumi wa dunia sasa hivi unapita kwenye kipindi kigumu kuliko wakati wowote katika historia ya dunia. Hali hii isipodhibitiwa kwa haraka na kwa umakini itakuwa na athari kubwa ya kushusha viwango vya hali ya maisha ya watu katika nchi zote duniani tajiri na maskini. Matajiri watakuwa maskini na maskini watakuwa fukara zaidi.

  Kama nilivyosema katika hotuba zangu zilizopita, kiini cha kudorora huku kwa uchumi wa dunia ni machafuko na kuanguka kwa mfumo wa fedha wa kimataifa. Tatizo lilianzia nchini Marekani na kuenea katika mataifa tajiri ya Ulaya na Asia. Mabenki makubwa na madogo yameanguka na kufilisika. Viwanda vikubwa na vidogo pamoja makampuni makubwa na madogo yamefilisika na kufungwa. Mamilioni ya watu wamepoteza ajira na wanaendelea kupoteza ajira. Maelfu kwa maelfu ya watu wamepoteza nyumba zao za kuishi. Kwa ujumla, mamilioni ya watu katika mataifa tajiri wanaishi maisha ya mashaka. Wengi maisha yao yameanza kuporomoka.

  Nchi zetu hazihusiki na kuzuka mwa matatizo haya lakini, athari za kudorora kwa uchumi wa dunia zinatukumba sote. Tayari tunashuhudia kupungua kwa bei na mahitaji ya bidhaa za nchi zetu kwenye soko la dunia, kupungua kwa idadi ya watalii na kupungua kwa uwekezaji na vitega uchumi kutoka nje. Aidha, mapato ya fedha za kigeni na mapato ya Serikali nayo yanapungua. Mambo haya hatimaye yatasababisha kushuka kwa uchumi wa nchi zetu, watu kupoteza ajira na kipato na hali za maisha za watu katika nchi zetu kuporomoka.

  Kunahitajika hatua thabiti zichukuliwe na hatua hizo ziwahusishe na kunufaisha wadau wote. Nchi tajiri duniani zinao wajibu mkubwa zaidi. Kwanza, zina wajibu wa kuhakikisha kuwa wanadhibiti hali ili uchumi wa nchi zao usiendelee kudorora. Pia zinao wajibu wa kuzisaidia nchi kama zetu ziweze kukabiliana na athari za kudorora kwa uchumi wa dunia. Nchi tajiri zimekuwa zinachukua hatua za kunusuru uchumi wa nchi zao na bado wanaendelea. Bahati mbaya nchi zetu maskini ambazo hazina uwezo wa kuwa na mipango kama hiyo, pamoja na ukweli kwamba nazo pia zinaihitaji sana, bado hazijasaidiwa.

  Ndugu Wananchi;
  Mkutano wa kesho wa Mataifa 20 Tajiri Duniani umeitishwa kujadili hatua zaidi za kuchukua kuzuia mambo yasiwe mabaya zaidi na kufanya uchumi ukue. Pia wanakusudia kuzungumzia njia za kuepuka maatizo kama haya yasitokee tena duniani. Katika mkutano wa kesho pia watazungumzia namna ya kuzisaidia nchi maskini za Afrika na zile zinazoendelea ziweze kujihami na kukabiliana na athari za matatizo ya uchumi wa dunia.

  Katika mkutano wao wa kwanza, uliofanyika Washington, Marekani, jambo hili halikufanyika. Wakati ule nikiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), nilimwandikia Rais George Bush wa Marekani, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano ule, kumuomba wayaangalie maslahi ya Afrika, lakini hatukufanikiwa. Tulipata ahadi kuwa katika mkutano utakaofuata jambo hilo litazingatiwa.

  Tunamshukuru Waziri Mkuu wa Uingereza, Bw. Gordon Brown kwa kutimiza ahadi yake aliyonipatia kuhusu kujali maslahi ya Afrika pamoja na kutoa fursa ya ushiriki na sauti ya Afrika kuwepo katika mkutano huu wa pili. Kwa nia ya kupata maoni ya Waafrika hasa kuhusu matakwa na matarajio ya Afrika katika mkutano wa G-20, Waziri Mkuu wa Uingereza, tarehe 16 Machi, 2009 aliitisha mkutano maalum baina yake na viongozi kadhaa wa Afrika mjini London, Uingereza. Mkutano huo uliohusisha viongozi wa nchi za Tanzania, Liberia, Afrika Kusini, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Botswana, Misri, na Cape Verde ulikuwa na manufaa makubwa.

  Ndugu Wananchi,
  Nilitumia nafasi hiyo kuwasilisha maoni na mapendekezo ya mkutano wa pamoja wa Mawaziri wa Fedha, Magavana wa Benki Kuu za Afrika na Shirika la Fedha Duniani (IMF) uliofanyika hapa Dar es Salaam kuanzia tarehe 10 hadi 11 Machi, 2009. Mapendekezo hayo yalikuwa msingi wa mazungumzo yetu katika mkutano wetu na Bw. Gordon Brown.

  Kwa muhtasari, matarajio ya Afrika katika mkutano wa G-20 ni kwa Afrika kusaidiwa kujikinga na kukabili madhara ya kudorora kwa uchumi wa dunia. Miongoni mwa mambo ambayo tuliyasisitiza ni haja ya kuanzishwa mfuko maalum ambapo fedha zake zitatumika kuzisaidia nchi za Afrika kuchukua hatua za kunusuru uchumi wao kama wafanyavyo mataifa tajiri.

  Kwa maneno mengine tuliunga mkono pendekezo la Benki ya Dunia na kutaka Mkutano wa G-20 ukubali kwamba asilimia 0.7 ya fedha walizotumia kugharamia mipango yao ya kuchochea uchumi wao (stimulus packages) zitengwe kwa ajili ya kusaidia kuchochea kukua kwa uchumi kwa nchi za Afrika. Pili, tulisitiza kuwa nchi tajiri zisipunguze misaada ya maendeleo kwa nchi maskini. Badala yake misaada hiyo iongezwe kama walivyoahidi kwenye mikutano ya Monterrey, Gleneagles na kwingineko.

  Tatu, tulisema kwamba tunatarajia pia misaada kwa Afrika, na uwekezaji kutoka nje vitaelekezwa katika kujenga na kuboresha miundombinu, kuleta mapinduzi katika kilimo, kukuza biashara miongoni mwa nchi za Kiafrika na baina yake na nchi nyingine za dunia na kusaidia zaidi makundi katika jamii ambayo yanahitaji msaada zaidi (vulnerable groups).

  Nne, kwamba nchi tajiri duniani pamoja na Taasisi za Kimataifa za Fedha Duniani zilegeze masharti na kupunguza urasimu wa kupata fedha za misaada na mikopo kwa kutambua kwamba hiki ni kipindi kugumu na cha dharura. Aidha, masharti ya kukopa kutoka vyombo vingine vya fedha yalegezwe pia.

  Tano, kwamba nchi tajiri zisaidie nchi za Afrika kujenga mitaji ya vyombo vya fedha vya kikanda kama vile Benki ya Maendeleo ya Afrika. Na, la sita, kwamba, nchi tajiri zitakubaliana kuruhusu uwazi katika mabenki yao na taasisi zao za fedha ili kuwezesha nchi za Kiafrika kufuatilia na kurudishiwa fedha, majumba na rasilimali zilizoporwa kutoka katika bara letu na kuhifadhiwa kisirisiri katika mabenki ya nchi tajiri.

  Ndugu Wananchi,
  Tunamshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu Gordon Brown kwa kuyapokea mapendekezo haya ya Afrika kwa moyo mkunjufu na kuahidi kuyafikisha na kusaidia kuyatetea katika kikao hicho. Pia tunamshukuru amepokea rai ya Afrika ya kuwakilishwa kwenye mkutano huo kwa kumwalika Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Meles Zenawi, ambaye atatuwakilisha kwa kofia yake ya Uenyekiti wa NEPAD.

  Ndugu Wananchi;
  Mkutano huu wa G-20 ni muhimu sana kwani unalo jukumu la kihistoria la kuuokoa uchumi wa dunia. Kwa msemo wa Kiswahili tungeweza kusema kuwa kazi ya mkutano huu ni ya kufa na kupona. Mkutano ukifanikiwa, sote tumenusurika. Ukishindwa sote tutakuwa mashakani na tunaweza kuangamia. Tuwatakie viongozi wa G-20 heri na fanaka tele katika mazungumzo yao. Hatima ya maisha na ustawi wa dunia na watu wake uko mikononi mwao.  My TAKE:

  TUMELAANIWA, TUMEROGWA NA KWA HAKIKA HATUNA NAFASI YA KUFANIKIWA! - Tanzania inafanya nini kustimulate uchumi wake?
   
 2. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,181
  Likes Received: 663
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo..!
  Je mambo hayataenda bila kupitisha bakuli kwa wajomba?
   
 3. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Tanzania ina wenyewe, kama sisiem ilivyo na wenyewe, wanaomba kwa mkono wa kulia wanagawiana kwa mkono kushoto.

  Jitihada ni jinsi ya kuhakikisha tunakata mikono yote miwili. Rasilimali zipo kibao, mkulu kazi yake kuzunguka na mkebe tu, hadi anatutia aibu watanzania kote duniani, yule rais wa afrika ya mashariki, "msafiri".
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kama ni hivyo, kwa nini hatukumuweka Rais Mgogo?

  Malecela angelitafuta sana kwani jamaa zake wenye uzoefu wa kutembeza bakuli wangelimpa mwanga mkubwa wa what to do ili bakuli lijae. Tungelitengeneza wizara ya Ombaomba ambayo ingelikuwa karibu sana na HAZINA na Wizara ya Fedha. Hii Mshauri wake mzuri angelitufaa ni MATONYA, hata RA mwenyewe angelichangia badala ya kufisadi.

  Hebu fikiri Rais wetu kwenye mkutano wa G20, anafika hapo na bakuli lake na kulala chini na bakuli juu. Haki ya nani angelikusanya hela nyingi sana.... Hata mie ningelichangia maana kumuona Rais wa watu yuko tayari kujidhalilisha kwa ajili ya watu wake, Mgogo huyo angelistahili hongera kubwa.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,551
  Likes Received: 18,226
  Trophy Points: 280
  MMKJ, haya sasa ni maneno ya kukata tamaa.'hajujalogwa bali ni viongozi wetu. Kwa kauli "KWA HAKIKA HATUNA NAFASI YA KUFANIKIWA!" hili swali l"Tanzania inafanya nini kustimulate uchumi wake?" limekuja kufanya nini?.
  Bado tuna nafasi ya kufanikiwa tukikubali mabadiliko.
   
 6. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mimi naisoma mtu hali hii kama mgonjwa mnyonge..aliyeadhirika fikra and much more!

  It doesnt show any strong will to fight..Hakuna character! Ndio! We need some push toka kwa rafiki zetu etc but kuji prisent kama tumenyongoyea na kufanya watanzania kuamini mitizamo kama hii haitunvunjiii utu wetu bali mpaka kinga ya mwili...Kauli imefifia sana...!

  No No its not like that!!! Its too much!
   
 7. K

  Kaka Mdogo Member

  #7
  Apr 2, 2009
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jamani Rais wetu kachoka. nafikiri angekuwa muungwana angeachia tu madaraka baada ya miaka mitano, kwa sababu kachoka na kakosa mwelekeo. Hivi hii dhana ya kwamba sisi ni maskini inatoka wapiiiiiii????? Yaani hatuwezi kuuza utajiri wetu bali umaskini. Yaani nimeangalia speech ya rais jana nikatamani kulia. Rais anaongea kama vile anaongea na watoto wa chekechea. Anaongea mambo ya kuomba misaada kama vile ni jambo la kawaida sana. Anaongelea issue ya umeme na kwamba asilimia 14 tu ya watanzania ndio inayopata huduma ya umeme, na wala haongelei mikakati ya hata kufikia asilimia 50. aibuuu!! kwanini asimuige Obama akaja na sera ya YES, WE CAN!!
   
 8. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  The inability of our president to even make an effort with self reliance amazes me.I feel humiliated by the way he sucks up to rich nations who have developed through HARD WORK!
   
 9. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  MMKJJ

  Naomba unitoe kwa wale waliolaaniwa na kurogwa, imani hiyo sina!

  Sidhani kama unauhakika kuwa hatuna nafasi ya kufanikiwa.

  Sasa kama tumelaaniwa na kurogwa kuna haja gani ya kustimulate urogaji na laana?

  Hiyo stimulation ya uchumi si ndio itawaongezea nguvu warogaji na hata kuongeza laana!

  Laana tupu kufikiri na hata kupayuka kuwa 'hatuna nafasi ya kufanikiwa'

  Amani
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Apr 2, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Wazungu hawana wajibu wa kutusaidia sisi Miafrika. Na wala hatujarogwa wala kulaaniwa. Ni kwamba Miafrika Ndivyo Tulivyo. Nani anabisha?
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Apr 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  mtu aliyerogwa hajui kuwa karogwa hadi aende kwa mganga wa kienyeji. Atajaribu kutumia teknolojia ya wazungu ndipo mwisho atatambua kinachohitajika ni "mitishamba". There is no rational or conventional way of explaining whatever bs is going on with the Tanzanian leadership. None whatsoever. Except some kind of witchcraft or superstition beliefs!
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hatukurogwa wala kulaaniwa, simpo, hatuna akili! na hii ni sababu ya kudumazwa kimawazo tulikofanyiwa wakati tunalazimishwa kuwa wajamaa wa kuiga, mitaala ya shule (ingawa zilikuwa bure) ilikuwa mibovu, kuimbishwa ngonjera za siasa, kulimishwa, kufagilishwa, kuchezeshwa halaiki, haya ndio matunda yake.

  Ndio kwanza tunaanza kufunguwa macho, ilituchukuwa miaka mingi ya kufungwa macho na waIngereza waliopewa jukumu la kuiongoza Tanganyika, tukafikiri tukidai kujiongoza tutakuwa tumepata ufunuzi, lilikuwa wazo zuri kweli, tukapewa uongozi, kilichotokea? tukafungwa macho na masikio na fikra na utawala uliotulazimisha tuingie kwenye ujamaa kwa kutumia kila njia chafu, kuanzia za kinadharia, kisaikolojia mpaka za kimabavu. Ikashindikana kabisa, hapo iliposhindikana. tayari wa Tanzania hoi, elimu duni, kula duni, kuvaa duni, kwa kifupi kila kitu nyang'a nyang'a!

  Raisi huyu wa sasa ndio umeona ametutowa kutoka kwenye tegemezi kutoka kwa wahisani la zaidi ya asilimia 60 ya bajeti yetu kufikia 40 na mwakani 30, kapiga hatuwa kubwa katika kuonyesha kuwa anaweza kututowa kwenye uomba omba na kwa hilo inabidi tumsifu.

  Mzee Mwinyi kipindi chake na mabadiliko ya kisiasa duniani ndio tukaanza kupata ahueni, tukapewa RUKSA ya kuweza kufanya tupendacho na tutakacho. Ni muda mfupi sana wa kuwa na akili zetu wenyewe za kutosha kuliendesha Taifa. Wengi wetu bado wana kasumba za uongozi wa wakati tuliofungwa ki akili, siwalaumu, ndio, kila siku zinavyokwenda tunaona mabadiliko ya nyakati na tunaanza kujulimbikizia viakili, tunaanza kusoma kwa kufuata mitaala tuipendayo, kama ile ya serikali hatuitaki. Kama nchi itafananishwa na binadam basi sisi bado tu watoto wachanga kwa sasa. Tusikate tamaa, tutakuwa, na akili tutapata kila tukuwapo.
   
 13. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Na nchi nyingine za Afrika ambazo hazikufuata siasa ya Ujamaa kama unavyodai ni nini tatizo lao???
   
 14. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ukweli unabaki kuwa, hii Financial crisis inayoikumba dunia hivi sasa inaumiza/itaumiza sana nchi zote duniani. Ina fifisha matumaini mengi ambayo nchi zote ilikuwa imejiwekea. Mapato ya nchi yatashuka, na hivyo mapato ya kila mtu yatakuwa matatani. Hivyo kila nchi ni lazima ikajiweka sawa kukabiliana na matatizo haya, bila kusubiri msaada wa mwenzake (zaidi ya kupeana mikakati inayofaa). Kwa maana, hao wenzako unaowasubiri wakusaidie, wao pia wanataka kutatua matatizo yao (wana shida ya pesa). Kama hawakuwa wakikusaidia wakati wakiwa na uwezo, inakuwaje leo wakiwa na shida ya pesa unadhani wana uwezo zaidi wa kukusaidia?

  Nchi kama Tanzania, inaweza kuanza sasa kufikiria vyanzo vipya vya mapato. Vyanzo hivyo ni lazima vianzie ndani ya nchi, kwa kuboresha uwekezaji wa ndani na kubana matumizi yasiyo ya lazima.

  Nionavyo mimi, kipindi hiki sio cha kuweka bakuli juu na kuomba misaada kutoka kwa wahisani (watakuchukia na kukucheka). Ni kipindi cha kufanya reforms za namna ya kufanya kila jambo linalohitaji pesa. Mambo ambayo serikali inaweza kuyafanya ni kama:

  1. Kupunguza ukubwa wa Wizara zake
  2. Kupunguza semina, warsha, kongamano na mengine yasiyo na tija za haraka kwa maendeleo ya nchi
  3. Kupunguza matumizi ya ununuzi wa magari, safari za nje (kufanya nini kama hawana cha kukusaidia?), n.k.
  4. Kuhimiza uzalishaji wa mazao ya chakula zaidi ya yale ya biashara. Dunia inapokuwa katika shida kama hizi, mazao ya biashara ndio yanayokuwa na tija zaidi. Rais amezungumzia uhaba wa chakula duniani. Kilimo cha chakula kikihimizwa inavyotakiwa, kinaweza kuwa njia ya ukombozi wa nchi kama zetu ambazo zina ardhi nzuri. Uwekezaji wa kufa na kupona kwenye kilimo ndio njia inayofaa sasa.
  5. Kuhimiza wananchi kufunga mikanda na kutumia kidogo walichonacho kwa uangalifu.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Apr 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo unasema ni utoto tu, tukikua tutaacha!?
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Apr 2, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni moja tu. Nalo ni Miafrika Ndivyo Tulivyo! Wengi wanaokataa ukweli huu wanakataa kwa sababu ya majivuno tu lakini hawana ubavu wa kubadilisha mazingira yaliyopo Afrika. Tukibadilishana nchi sasa hivi, kwa mfano, Watanzania wote wahamie Uingereza na Wingereza wote wahamie Tanzania....guess what? Baada ya miaka michache tu tutaanza kudai waturudishie nchi yetu na wao warudi kwao. Huu ni ukweli na wengi wetu tunaujua lakini tunaukana tu.
   
 17. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #17
  Apr 2, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45

  MMKJJ,

  Ina maana umeshafanya madogoli na kuona kuwa tumerogwa/wamerogwa? just-a-jest

  Yes the Bs is inexplainable, na nimefurahi kuona it is the Leadership and not the populace! Manake kweli tungehitaji stimulus kwenda kutafuta 'mitishamba!'

  This is Stimulating by itself.

  Thanx
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Apr 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Jana nilikuwa nazungumza na Ole Naiko wakati wa mkutano wa Waipa kuhisiana na hilo, hasa upande wa kuvutia na ku-retain wawekezaji, aliniambia kuwa hadi hivi sasa serikali haijawa na plan yoyote tangible ya kukabiliana na yanayoendelea duniani katika anga za kiuchumi
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Apr 2, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Lini tumewahi kuwa na mipango yoyote ya kukabiliana na hali ngumu na uduni wa maisha? When? We've always been in a recession...
   
 20. U

  Utatu JF-Expert Member

  #20
  Apr 2, 2009
  Joined: Dec 31, 2008
  Messages: 436
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60


  MM,

  Hili swali JK alishaulizwa pale kwenye ule mkutano wa IMF dar. Akatapatapa. Hadi leo hii hajafikiria jibu lake ni nini. Usitegemee kitu chochote kutoka kwake. Huu ni uchovu uliozidi kipimo. Usanii utamuishia 2010.
   
Loading...