Rais Mutharika: Amewataka wafuasi wake kupuuza matokeo yanayosambazwa na vyombo vya habari

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Ijapokuwa tume ya uchaguzi ya Malawi MEC bado haujatangaza matokeo ya uchaguzi wa urais uliorudiwa , ishara za mapema zinaonesha kwamba rais Peter Mutharika yuko nyuma ya mpinzani wake mkuu Lazarus Chakwera.

Kulingana na mgombea mwenza Atupele Muluzi, ambaye alisema kwamba ametumwa na Mutharika kuzungumza na vyombo vya habari, rais amewataka wafuasi wake kupuuza ripoti zinazosema ameshindwa katika uchaguzi huo, akisema wanapaswa kusubiri matokeo rasmi ya tume ya uchaguzi ya MEC.

Atupele Muluzi ni mwana wa rais wa zamani Bakili Muluzi na kiongozi wa chama kidogo cha upinzani United Democratic Party DPP.

Muluzi amedai kwamba takriban wachunguzi 15 waliotumiwa na DPP/UDP katika maeneo ya upinzani wametoweka na wengine kuhofiwa kufariki baada ya kushambuliwa na wafuasi wa upinzani.

Matokeo ya wilaya zote 28, yaliotiwa saini na maafisa pamoja na wawakilishi wa wilaya yanaonesha kwamba rais Mutharika yuko nyuma ya Lazarus Chakwera ambaye anaongoza chama cha upinzani cha Malawi Congress party na kinawakilisha muungano wa Tonse unaoshirikisha vyama vinane vya upinzani.

Chombo cha habari cha serikali kinasema upinzani unaongoza
Upinzani nchini Malawi unaelekea kupata ushindi katika kura ya uchaguzi wa urais inayofanyiwa marudio baada ya matokeo yake kufutiliwa mbali kufuatia madai mengi ya udanganyifu.

Matokeo rasmi ya uchaguzi huo uliofanyika siku ya Jumanne hayajatangazwa na tume ya uchaguzi ya Malawi.

lakini chombo cha habari cha serikali MBC kinasema kwamba kiongozi wa upinzani Lazarus Chakwera alikuwa anaongoza na asilimia 59 ya kura zilizohesabiwa siku ya Jumatano.
Rais Peter Mutharika , ambaye anawania muhula wa pili ana asilimia 38 ya kura zilizohesabiwa, kinasema.

Mgombea wa tatu ambaye hakuonekana kama mgombea mkuu Peter Kuwani anasemekana kujiapatia asilimia 2 ya kura hizo.

Mwaka uliopita, Malawi ilikuwa nchi ya pili barani Afrika kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais kufuatia madai ya udanganyifu, baada ya Kenya 2017.
Mwandishi wa BBC katika eneo la kusini mwa Afrika, Andrew Harding anasema sio jambo la kawaida na kwa wengi linavutia - Mahakama iliingilia kati na kubadilisha matokeo katika eneo ambalo wizi wa kura ni suala la nyeti.

Muongozo wa uchaguzi wa Malawi
Lazarus Chakwera (Kulia) anampinga rais Peter Mutharika (Kushoto)


Maelezo ya picha,
Lazarus Chakwera (Kulia) anampinga rais Peter Mutharika (Kushoto)

Wafuasi wa bwana Chakwera tayari wameanza kusherehekea kile wanachoamini ni ushindi wa kihistoria - katika kile kinachoaminika kuwa tukio la kwanza katika eneo la sahara kwamba uchaguzi uliokumbwa na udanganyifu umebadilishwa na upinzani kuibuka na ushindi ukichukua madaraka kwa njia ya kidemokrasia.
Pongezi pia zimetolewa na viongozi wa upinzani katika mataifa ya Afrika ya kusini.

"Maisha mapya kwa Malawi!," alisema kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Nelson Chamisa.

"Mungu ameipatia Malawi Mcha Mungu'', aliongezea akitaja historia ya Chakwera kama kiongozi wa dini.
''Ndugu yangu, rafiki yangu na kiongozi ameshinda uchaguzi wa Malawi. Niliwasiliana naye kwa simu na kusherehekea ushindi wake'', alituma ujumbe wa twitter kiongozi wa zamani wa chama cha upinzani cha DA Mmusi Maimane.
Subira iliojaa wasiwasi

Mwandishi wa BBC anasema taasisi za kidemokrasia nchini Malawi huenda zikakabiliwa na shinikizo kali katika saa chache na siku zijazo.
Taifa hilo lilikuwa limegawanyika kabla ya uchaguzi huo wa marudio huku kukiwa na maandamano makubwa ya kupinga serikali.
Kiongozi mkuu wa serikali amedaiwa kusema kwamba uchaguzi unaibiwa.

Watu walipiga kura siku ya Jumanne


Maelezo ya picha,
Watu walipiga kura siku ya Jumanne licha ya hofu ya corona
Akizungumza siku ya Jumanne baada ya kupiga kura kusini mwa Malawi, bwana Mutharika alidai kumekuwa na ghasia katika maeneo ya upinzani, kilisema chombo cha habari cha Reuters.

''Inasikitisha. katibu wetu mkuu amepigwa . wale wanaosababisha ghasia hawana la kufanya '', Reuters ilimnukuu rais akisema.
''Ni vipi sasa kwamba uchaguzi huu utakuwa wa haki na huru''?, aliuliza.
Hatahaivyo ripoti hizo hazijathibitishwa.

Akipiga kura yake kiongozi wa upinzani Chakwera alisema kwamba ana imani na tume ya uchaguzi kufanya kile kilicho cha haki.
''Naamini kwamba hatua ya raia wa Malawi kutafuta haki inajibiwa hii leo. Na naamini haki yao itaheshimiwa'', aliongezea.
Yeyote yule atakayeibuka mshindi atalazimika kupona mgawanyiko uliotokea pamoja na kukabiliana na masuala muhimu ya ufisadi, umasikini na ukosefu wa ajira.

Kwanini kulikuwa na uchaguzi?

Kura ya marudio ya uchaguzi wa Mei 2019 iliagizwa na mahakama ya kikatiba nchini Malawi mwezi Februari baada ya majaji kubaini udanganyifu mwingi.
Uchaguzi huo ulimfanya rais Mutharika kupata ushindi mwembamba wa kura 159,000 ambazo ni asilimia 38.6 ya kura zilizopigwa . Bwana Chakwera alikuwa wa pili na asilimia 35.4.

Bwana Chakwera na mgombea aliyekuwa katika nafasi ya tatu walihoji kwamba uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki.
Malalamishi yao yalishirikisha madai kwamba nakala za kuhesabu kura hizo zilifutwa na kuongezewa idadi ya kura kwa kutumia wino wa kusahihisha makosa.
Hali ya switafahamu kuhusu matokeo hayo ilizua miezi kadhaa ya wasiwasi na maandamano, yaliobadilika na kuwa ghasia kati ya wafuasi wa upinzani na maafisa wa polisi kote nchini.

Uamuzi wa mwezi februari wa kufuta matokeo hayo ya uchaguzi uliwafanya watu kusherehekea , lakini bwana Mutharika alitaja uamuzi huo kama'' mabadiliko ambayo yanaadhimisha mwanzo wa mwisho wa demokrasia nchini humo.

Mwezi uliopita, mwenyekiti wa zamani wa tume ya uchaguzi nchini Malawi Jane Ansah alijiuzulu kufuatia miezi kadhaa ya shinikizo ya waandamanaji ambao walimkosoa kwa jinsi alivyosimamia uchaguzi huo.

Kura mpya inajiri wakati ambapo kuna hofu kubwa kati ya serikali na mahakama za taifa hilo.
Pia kumekuwa na wasiwasi kuhusu mkakati na usalama wa kufanya uchaguzi katikati ya mlipuko wa virusi vya corona.
 
Naona waananza mchakato wa kutaka kupigana ila sisi hatuta pokea wakimbizi huku kwetu.
 
Jecha Yupo Njiani Naamini Iwapo Hawata Kuwa Makini
Yale Ya Manchester United Vs Bayern Munich Yanakwenda Kutokea.
Yaani Hajaamini
 
Hili ni pigo kubwa sana kwa Tanzania, Malawi wanatufanya tuonekane taifa la wajinga sana wasioweza hata kusimamia uchaguzi wao wenyewe.

Ktk Tanzania chama kinachotawala eti ndicho kinaandaa na kusimamia uchaguzi, sisi ni bure ni hakuna mfano. Viva The Nyasaland.
 
"As I urge this nation to go into soul-searching and self-reflection, I ask all Malawians to move on peacefully. We are at the moment waiting for the Malawi Electoral Commission to announce the
results of the Election.
Much as I find this Election unacceptable, but for the sake of peace, & for the love of our country, which is larger than us all, I wish to ask all Malawians to be peaceful when the results are announced." Peter Arthur Mutharika

IMG_20200627_192036.jpg
IMG_20200627_195911.jpg
IMG_20200627_195914.jpg
IMG_20200627_195909.jpg
IMG_20200627_192029.jpg
IMG_20200627_200710.jpg
 
Final national results for the Malawi fresh election

Registered voters 6,859,570
Total votes 4,445,699
Voter turn out 1.9%
Valid votes 4,388,376
Null & void 56,323 (1.9%)

Dr. Chakwera - 2,604,043 (58.57%)
Peter Dominic Driver Kuwani - 32,456
Prof. Arthur Peter Mutharika - 1,751,377

I wish to congratulate the President-elect of the Republic of Malawi, H.E. Lazarus Chakwera for his resounding and well-deserved victory.
#MalawiDecides2020
 
Back
Top Bottom