Rais Museveni kufanya ziara ya kikazi Tanzania. Atakabidhi Shule iliyojengwa kwa ufadhili wake Wilayani Chato

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni anatarajiwa kuwasili Tanzania kwa ziara ya Kitaifa kuanzia Novemba 27, 2021, na atapokelewa na Rais Samia Suluhu Hassan

Mbali na Marais hao kufanya mazungumzo, pia watashiriki ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda

Rais Museveni atatembelea Bandari ya Dar na kukagua mradi unaoendelea wa SGR. Vilevile, ataenda Wilayani Chato, Mkoani Geita ambapo ataikabidhi rasmi Serikali ya Tanzania Shule ya Msingi iliyojengwa kwa ufadhili wake

7230DC5A-F232-4BBE-9AA9-D9AAC3B1C62F.jpeg
 
Mseveni siyo jirani, dikteta. Madikteta wanafahamiana na kusaidia a popote walipo. Ndo maana hiyo haikujengwa songea wa Mtwara kwa mashangazi 'zao'. Ikapelekwa mulemule.
Samia anayemtembelea na kumpokea ni dikteta?
 
Si chadema wanasema Magufuli alifunga nchi na kuharibu mahusiano na majirani?
Kumbe majirani hao hao walitujengea hadi shule!
Chadema wao utawaonea ,waliosambaza uongo huo na chadema kuunga tera ni wana CCM wenzenu wakiongozwa na team msoga ,na makamba ambao tumekuja gundua hawakuwa na hawajawai kumpenda magufuli tangia aingie madarakani, na ukute ata watu waliookotwa baharini kwenye viroba ni wao ndo wali plan ili wananchi mchukie kiongozi wao, ni swala la muda tu tutajua kilakitu.
 
Umenena vyema mkuu
 
Mseveni siyo jirani ni dikteta. Madikteta wanafahamiana na kusaidiana popote walipo. Ndo maana hiyo shule haikujengwa Songea wala Mtwara kwa mashangazi 'zao'. Ikapelekwa mulemule.
Ukiondoa madikteta waongoza nchi kuna madikteta waongoza vyama
 
Mseveni siyo jirani ni dikteta. Madikteta wanafahamiana na kusaidiana popote walipo. Ndo maana hiyo shule haikujengwa Songea wala Mtwara kwa mashangazi 'zao'. Ikapelekwa mulemule.
Zimwi likujuwalo mkuu
 
Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni anatarajiwa kuwasili Tanzania kwa ziara ya Kitaifa kuanzia Novemba 27, 2021, na atapokelewa na Rais Samia Suluhu Hassan

Mbali na Marais hao kufanya mazungumzo, pia watashiriki ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda

Rais Museveni atatembelea Bandari ya Dar na kukagua mradi unaoendelea wa SGR. Vilevile, ataenda Wilayani Chato, Mkoani Geita ambapo ataikabidhi rasmi Serikali ya Tanzania Shule ya Msingi iliyojengwa kwa ufadhili wake

View attachment 2024364
Ndege wa rangi moja
 
Back
Top Bottom