#COVID19 Rais Museveni atangaza amri ya kutotoka nje kwa siku 14

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametagaza masharti zaidi ya kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona wiki mbili baada ya kupiga marufuku usafiri wa Umma.

Katika hotuba yake kwa taifa iliyopeperushwa moja kwa moja kwenye televisheni usiku wa Jumatatu Bw. Museveni amepiga marufuku usafiri wa kutumia magari binafsi na boda boda kuanzia saa nne usiku.

Mtu yeyote anayehitaji huduma za dharura za kiafya kama vile kujifungua au kufanyiwa upasuaji anatakiwa kupata idhini kutoka kwa maafisa wa serikali katika ngazi ya Wilaya kabla ya kutoka nyumbani

Wauzaji bidhaa za chakula sokoni watahitajika kuondoka maeneo yao ya biashara hadi pale serikali itakapokamilisha kushughulikia maeneo mapya ya wao kuuzia bidhaa zao .

Rais Museveni pia ameahidi msaada wa chakula kwa watu ambao hawafanyi kazi kutokana na vikwazo vya kukabiliana na covid-19 na hawana uwezo wa kujipatia bidhaa hiyo muhimu.

Bw. Museveni pia ametoa agizo kwa polisi kuwakamata wanasiasa watakaotoa misaada ya chakula kwa jamii na kushtakiwa kwa ''jaribio la mauaji ''

Uganda kufikia sasa imethibitisha kuwa na wagonjwa 33 wa corona na maafisa wanatarajia idadi hiyo kuongezeka.

Magari binafsi yatazuiwa kuingia barabarani baada ya maelekezo ya awali kutaka magari kubeba abiria watatu pekee kukiukwa, na baadhi ya watu kutumia magari binafsi kuwasafirisha wengine na kuongeza hatari ya kusambaa kwa virusi hivyo. Limeandika gazeti la New vision la Uganda.

''Isipokuwa kwa ndege za mizigo, malori, magari aina ya pickups na treni, kuanzia siku ya Jumanne tarehe 31 mwezi Machi saa moja, amri ya kutotoka nje itatekelezwa katika nchi yote ya Uganda'' Meseveni aliesema.

Alisema kuwa siku 14 zitatumika kubaini na kuwafuatilia na kuwatenga wale wote waliokaribiana na watu waliothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Museveni ameamuru pia kufungwa kwa maduka makubwa, njia tao, maduka ya vifaa, biashara zisizo za chakula, saluni, nyumba za kulala wageni na karakana za magari kwa siku 14, maeneo amayo amesema hukusanya watu wengi, limeeleza gazeti la Daily Monitor la Uganda.

Amri hiyo haihusu hospitali, maeneo yanayotoa huduma za kitabibu na mashirika yanayojihusisha na masuala ya afya.
 
M7 is
1585646318146.png
, he is well informed that
 
Agawe chakula kwa wananchi sio kujivunia mamlaka ya kutangaza tu! Awajibike pia
 
Back
Top Bottom