Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 414
Rais Yoweri Museveni ameapishwa kwa mara ya sita mfululizo kuliongoza taifa hilo hadi mwaka 2026 katika sherehe zilizofanyika Uwanja wa Kololo nchini humo.
Museveni amekuwa kiongozi wa nchi hiyo tangu mwaka 1986. Sherehe za uapisho zimehudhuriiwa na viongozi takriban 11 wa mataifa mbalimbali barani Afrika wakiwamo Samia Suluhu wa Tanzania, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Évariste Ndayishimiye wa Burundi, Mohamed Abdullahi Mohamed wa Somalia na Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe.
Museveni alitangazwa mshindi katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2021 dhidi ya mpinzani wake Robert Kyagulanyi 'Bobi Wine' baada ya kujinyakulia kura milioni 5.85 au asilimia 58.64 ya kura zote.