Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,467
- 40,973
Ujinga ni ugonjwa mbaya kuliko magonjwa yote. Kama ungejua kilichopo huko kwenye madini, usingeweza hata kuthubutu kuyataja. Utawala wa awamu hii umeua kabisa sustainability ya industry ya madini.Waswahili husema, "mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni".
Ni ukweli ulio wazi Sasa kuwa Rais Magufuli atakumbukwa na watanzania katika vizazi vingi vijanyo.
Kipindi chake cha uongozi kimekuwa na mambo mengi makubwa ambayo kiukweli yalihitaji ujasiri mkubwa kuyafanya.
Hakika Magufuli ni mtu mwenye uthubutu hata Kama akifeli baadhi ya mambo lakini watanzania wataiona nia yake njema.
Huu mkataba wa madini kusainiwa kwa mara ya kwanza Tanzania itanufaika na raslimali yake ya madini, hii inamfanya Magufuli kuingie kwenye vitabu vya kumbukumbu vya taifa hili hasa mtu atakapogusa nyanja ya madini. Huu ni ukweli ulio wazi japo Wana siasa wengi watapinga hili.
Vitosho na maneno mengi ya kukatisha tamaa mara kushitakiwa Miga n.k , laikini alisimamia msimamo wake hadi leo matokeo tumeyaona.
Itakapo tajwa kampuni mpya ya TWIGA moja kwa moja utamtaja Magufuli, ukitaja mabadiliko ya sheria za madini hapo lazima utamtaja Magufuli, chimbuko la mawazo ya kuanzishwa vitu hivi vyote ni yeye.
Hebu tuseme ukweli.
1; Wana Mwanza itawachukua miaka mingapi kumsahau Magufuli kwa uwepo la daraja la BUSISI? Waliwahi kuota kuwa wangekuwa na kitu Kama hiki?
Ujenzi wa Meli tano ziwa Victoria itawachukua miaka mingapi hadi kusahau.
2; Itatuchukua miaka mingapi hadi kusahau Tren ya Umeme SGR!!
Kila atakae iona hata Kama ni miaka 70 baadae jina la Magufuli litamjia kichwani.
3; Wananchi wa kigoma watamsahau vipi Magufuli kwa ujenzi wa mabarabara yanayounganisha mkoa wa kigoma na mikoa jirani, mkoa ambao Kama vile ulikuwa umesahaulika kabisa.
4; Tutakapoanza kutumia Umeme kutoka Bwawa la Nyerere tutamsahau vipi Magufuli watanzania.?
5; Utakapoona ndege za ATCL zikipasua anga atamsahau vipi Magufuli?
Hakika huyu ni shujaa wa taifa hili, wanasiasa watakataa kwasababu nawao pia wanahitaji kushika dola hivyo usitegemee kuwa watamuunga mkono Magufuli hata mara moja.
Lakini vitu anavyo vifanya vinajieleza.
Prof Lumumba hakuwa mnafiki aliposema " the Magufulification of Africa."
Licha ya mapungufu yake kiuongozi lakini hakika huyu ni kiongozi wa mfano wa kuingwa barani Africa.
Mzee Masha (Baba yake Masha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani) aliwahi kusema kuwa, wasukuma wana msemo unenao, 'ukitaka kujua mtu kama ataendelea kuwa tajiri au atafilisika hivi karibuni, hesabu idadi ya ndama walioko zizini, usiangalie mitamba inayokamuliwa'. Na kwenye madini, ukitaka kujua kama nchi itaendelea kutoa madini, angalia miradi ya utafiti madini inayoendelea.
Utawala wa awamu hii umesababisha makampuni yote zaidi ya 160 kuacha kufanya utafiti wa madini Tanzania kwa sababu Tanzania siyo mahali salama.
Hiyo Twiga unayoisema, ungekuwa una uelewa japo mdogo sana juu ya Business Intelligence ungejua ni nini Barrick wanafanya na wanataka. Ukweli ni kuwa Twiga ni kampuni ya muda mfupi maana hata Barrick wenyewe hawataki kutumia hata dola yao moja kufanya utafiti wa dhahabu Tanzania. Hela wanayoipata Tanzania, sasa hivi inatumika sana kutafiti kwenye mataifa mengine. Watakapoondoka Tanzania, itakuwa mwisho wa Twiga lakini Barrick itaendelea mahali pengine Duniani.
Sent using Jamii Forums mobile app