Zanzibar 2020 Rais Mteule wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi kuapishwa Novemba 2

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
785
1,000
Rais Mteule wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi Novemba 2, 2020 ataapishwa kuwa Rais wa awamu ya nane wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Sherehe hiyo itafanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. Dkt. Mwinyi alishinda baada ya kupata 76.27% ya kura zote halali.

7581301A-FBDF-419A-9E2C-A66873CA7DA2.jpeg
 

Compact

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
4,006
2,000
Aaagh! Katibu Mkuu Kiongozi usiandike tena kwa herufi kubwa (caps). Nimeshindwa kusoma.
 

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
10,381
2,000
Mwenyezi Mungu ampe hikma aivushe salama Znz.

Seif na Jussa wanakaribishwa pia.
Hivi atawezaje kutawala kwa amani moyoni katika hali ambayo Wazanzibar wengi namna hiyo wanauwawa na kuachiwa vilema vya maisha ili tu yeye awe rais?
 

Compact

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
4,006
2,000
Hongera sana Mh Mwinyi kuchaguliwa kuwa Rais mteule wa Zanzibar.

Ili kuleta umoja wa kitaifa, ukishaapishwa kuwa Rais, kwa mamlaka uliyonayo wasamehe viongozi wa upinzani na baadhi ya wafuasi wao walioshikiliwa.
 

MrFroasty

JF-Expert Member
Jun 23, 2009
958
500
Nimesoma kitu kimoja kati ya jamii za watu wa nyumbani yaani watanzania. Wengi ya wananchi hawana uelewa juu ya mfumo wa kidemokrasia. Nimegundua ni kama vile tumeingia kwenye mfumo wa vyama kwa shingo upande si kwa moyo wa dhati. Hili linaonekana wazi unapogundua wengi wakifurahia idadi kubwa ya wabunge kutoka chama kimoja.

Kwa mwenye akili zake timamu na anaefahamu umuhimu wa political balance katika taifa. Ushindi huu wa kishindo hata ungelipatakana kwa ACT / CDM / CUF bado kwa mwenye ufahamu wake ingekuwa vile vile ni pigo kwa taifa kwa maana ile ya kukosa political balance kwa uendeshaji wa vyombo vya kutunga sheria.

Nashauri asasi za kiraia zikapigania kwa nguvu zote kipengele cha kutoa elimu ya kiraia kikabadilishwa na kuruhusu wengine wajaribu kutoa elimu ili watu wafahamu umuhimu wa demokrasia. Tuna hatua kubwa tunahitaji kwenda ikiwa watu wanafuata vyama vya siasa kama vile timu za mpira au itikadi tuu. Nadhani hiki ndio chanzo cha watu kulazimisha ushindi.
 

mtanzania in exile

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
615
500
Hongera sana Mh Mwinyi kuchaguliwa kuwa Rais mteule wa Zanzibar.

Ili kuleta umoja wa kitaifa, ukishaapishwa kuwa Rais, kwa mamlaka uliyonayo wasamehe viongozi wa upinzani na baadhi ya wafuasi wao walioshikiliwa.
Awasamehe walioshikiliwa au walioshikiliwa ndio wamsamehe yeye? na vipi wale ambao wamepotea wasiojulikana walipo atatwambia wako wapi na walikuwa wapi? Vipi wale waliouliwa na vikozi vya ulinzi?

Vipi ndugu na jamaa za waliouliwa unataka nao baada ya siku chache tu toka kupoteza ndugu zao wamsamehe Mwinyi na group lake au ana mpango wa kuwarudishia uhai wao?

Ingelikuwa wewe jamaa yako au ndugu yako amepoteza maisha yake kweli ungelimsamehe kiongozi ambae alisababisha kifo chake?
 

Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,633
2,000
Hongera sana Mh Mwinyi kuchaguliwa kuwa Rais mteule wa Zanzibar.

Ili kuleta umoja wa kitaifa, ukishaapishwa kuwa Rais, kwa mamlaka uliyonayo wasamehe viongozi wa upinzani na baadhi ya wafuasi wao walioshikiliwa.
Wale si wakusamehewa

Asiwachekee kabisa kwani walidhamiria kuleta vurugu kubwa Zanzibar, na kumpora ushindi

Bila mamlaka kuwa imara pengine Dkt. Mwinyi asingekuwa Raisi mteule
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom