singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
UKIKUTA kiongozi wa nchi anapenda kurandaranda kwenye miji mikuu ya mataifa ya ughaibuni, fahamu kwamba mtawala huyo hana ajenda ya maendeleo kwa wananchi wake, maana kwake sera za kimataifa ndilo liwazo lake, badala ya ustawi wa taifa kwa mikono yake.
Hapendi kusikia kilio cha “wasio nacho”, siku zote ana mzio (allergy) na jasho la wadunda kazi wa nchi yake, wenye kupanda bila kuvuna, kuwekeza jasho lao pasipo kupata kutokana na mfumo katili wa uchumi. Bali yeye huvutiwa na manukato ya ughaibuni, akaziba masikio kwa waliao nyumbani akiwaita “wavivu wa kufikiri”, na eti waliolaaniwa kwa ufukara wa kutengenezewa.
Ukiondoa Serikali za Awamu ya Kwanza chini ya Mwalimu Julius Nyerere, na ya pili chini ya Rais Ali Hassan Mwinyi, Serikali za Awamu mbili zilizofuata ziliongozwa na marais “watalii” “kiguu na njia”, wenye mitizamo ya “majuu” badala ya matatizo ya nchi, huku wakikaribisha nyang’au wa kimataifa kushambulia na kupora uchumi wa nchi kwa dhana potofu ya uwekezaji (usiojali) na uhusiano wa kimataifa.
Na hili la utamaduni ulioanza kujengeka, wa kuchagua kiongozi wa nchi kutokana na Mawaziri wa Mambo ya Nje, imeonesha dhahiri kwamba viongozi wa sampuli hiyo siku zote akili yao iko nje ya nchi zaidi kuliko kuwa ndani ya nchi na kwa wananchi wao.
Hawana muda na raia; ziara zao vijijini hufanana na za “flying doctors” – madaktari chonjo; misafara yao yenye ulinzi mkubwa, huenda kasi ya radi wasipate fursa ya kuongea na wanaowaongoza njiani, wakihofia “usalama” wao katikati ya wananchi wanaodai kuwaongoza, wakati hizo ni mbwembwe na makeke yenye gharama kubwa kwa wananchi na uchumi wa nchi.
Mbona Mwalimu Nyerere, alichanganyika kirahisi na wananchi shambani, akiwafundisha kilimo bora na bado hakudhurika?. Mbona Rais John Pombe Magufuli leo anaweza kusimama njiani akahutubia wananchi bila hofu ya usalama?.
Ni serikali hizi mbili za mwisho (Awamu ya Tatu na Awamu ya Nne) zilizouza uchumi wa nchi kwa pamoja na kuua uzalendo, maadili na utamaduni wa taifa kwa kasi ya kutisha kwa ubepari wa kimataifa chini ya utandawazi (utandawizi) usiodhibitiwa wala kuratibiwa.
Ni awamu hizi mbili zilizoiingiza nchi katika mikataba hatari ya kimataifa kiwango cha kukaribisha ukoloni nchini kwa mshangao wa nchi nyingi za kiafrika, kama tutakavyoona hivi punde katika makala haya.
Wale wanaojaribu kumtupia madongo, Rais John Pombe Magufuli kwa kutogeuka “mtalii” ili aanze kurandaranda nje ya nchi akitumbua jasho la watu wake, badala ya kuumia nao pamoja katika “kutumbua majipu” waliyotuletea, wanatumika na ubeberu kutaka kumwondoa kipenzi huyu wa watu kwenye reli ya ukombozi wetu; na hao wakafie mbali.
Nchi yetu ambayo hapo mwanzo ilijipambanua na harakati za ukombozi dhidi ya ukoloni mamboleo, ubeberu wa kisiasa na kiuchumi, sasa imeishiwa pumzi dhidi ya vita hizo kutokana na kuongozwa na mawakala wa maovu hayo.
Hebu tujikumbushe ilivyokuwa na namna leo “Yerusalemu” ya ukombozi wa Afrika inavyoteketea chini ya viongozi wasaliti, mawakala wa ubeberu wa kimataifa
Mei 25, 1963, mjini Addis Ababa, Viongozi wa nchi 13 za Afrika walioanzisha Umoja wa nchi huru za Afrika (OAU) siku hiyo, walikuwa na kazi ngumu kuchagua kipi kipewe kipaumbele na umoja huo; kati ya vita vya ukombozi wa kisiasa dhidi ya ukoloni mkongwe, na vita vya ukombozi dhidi ya ubeberu wa kiuchumi wa nchi za Magharibi.
Ni Rais wa kwanza wa Ghana na mwanaharakati wa mapambano barani Afrika, Kwame Nkrumah, aliyetegua kitendawili hiki kwa tamko lake maarufu kwamba, “Utafuteni kwanza ufalme wa kisiasa na mengine yote mtazidishiwa”.
Kwa kibwagizo hicho, OAU ilianza harakati kwa kujikita zaidi katika Vita vya Ukombozi wa kisiasa barani Afrika badala ya ukombozi wa kiuchumi. Nkrumah akasema, Ghana iongoze harakati hizo na Makao Makuu ya ukombozi yawe Accra, Ghana; lakini Julius K. Nyerere wa Tanzania akapinga, akasema, Makao Makuu yawe Dar es Salaam, karibu na kichwa cha udhalimu – Afrika Kusini ya Makaburu, ili iwe rahisi kuutokomeza ubaguzi wa rangi. Nyerere akashinda, Makao Makuu ya harakati za kupigania uhuru barani yakawa Dar es Salaam.
Ile dhana ya Nkrumah kwamba ukijikomboa kisiasa utakuwa pia umejikomboa kiuchumi haikufanya kazi, wala haijafanya kazi hadi leo. Afrika sasa yote ni huru, lakini hakuna hata nchi moja ya Kiafrika iliyo huru kiuchumi; zote ni masikini, zinazidi kuwa masikini kuliko hata kabla ya enzi za uhuru.
Kati ya nchi 42 masikini sana duniani (LDCs), 28 zinatoka bara la Afrika ambazo zimebebeshwa na nchi tajiri deni la zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 40 ambalo halilipiki. Tanzania pekee ina deni linalozidi dola bilioni nane.
Hali hii ya umasikini imezidi kuongezeka kutokana kwamba, viongozi wengi walioongoza harakati za kuleta uhuru hawakufanya hivyo kwa lengo kamili la kuondoa ukoloni na utegemezi; walichotaka ni kuchukua nafasi ya wakoloni na kubakia ndani ya mfumo wa kikoloni.
Kwa mfano, kulikuwa na sababu gani kwa nchi huru zilizotawaliwa na Mwingereza, kuendelea kuwa wanachama wa Jumuiya ya Madola chini ya Malkia wa Uingereza? Au zile zilizotawaliwa na Wafaransa (Francphone States), kuwa wanachama wa nchi zinazoongea Kifaransa? Ni kwa kiasi gani Umoja wa Mataifa (UN) ni wa manufaa kwa mataifa yote, kama si kwa madhumuni na kwa manufaa ya mataifa makubwa ya Ulaya yaliyouunda baada ya vita ya Pili ya Dunia ya kupigania makoloni?.
Baada ya vita vya ukombozi kumalizika na Afrika yote kukombolewa, ni dhahiri kwamba, kwa kuzingatia madhumuni ya kuanzishwa kwake, OAU haikuwa na kazi tena; na kwa kweli chombo hiki kiligeuka kuwa kikao cha malumbano na ukinzani tu, kiasi kwamba maazimio yaliyofikiwa yalisahaulika mara tu viongozi wa nchi wanachama waliporejea kwenye miji mikuu ya nchi zao.
Ni kwa sababu hii kwamba mwaka 2002, OAU ilibadili madhumuni yake na jina, kutoka harakati za ukombozi wa kisiasa kuwa harakati za ukombozi wa kiuchumi na kuitwa “Umoja wa Afrika” – AU. Je, AU itaweza kumaliza matatizo ya kiuchumi yanayozikabili nchi za Afrika?.Kupata jibu la swali hili, hatuna budi kuangalia jinsi Afrika inavyoonekana machoni mwa nchi tajiri zilizoitawala.
Afrika inaundwa na nchi 53 zinazojiita mataifa huru. Bara hili limeingia karne ya 21 likiwa mhanga mwenye makovu wa ajali kuu mbili: Kwanza, ni biashara ya utumwa iliyojenga dhana kwa mataifa ya nje kwamba Mwafrika ni mtu wa kutumikishwa daima; hana utamaduni wala asili ya kutamani kwa kuwa utamaduni wa mdogo hauna mvuto kwa mkubwa. Pili, ni ukoloni mkongwe wenye kudhalilisha na kunyanyasa utu na ubinadamu.
Historia imetuonyesha kwamba, mkoloni sio tu hukalia na kupora nchi, bali hukalia na kupora kila kitu mpaka roho ya mtawaliwa. Na katika kujaribu kumfanya mtawaliwa huyo kuwa mali yake na mtumwa milele, humjeruhi na kumlemaza roho na mwili kwa kupotosha utamaduni wake, kiasi cha kuuteketeza kumfanya (mtawaliwa) ajione kama mtu asiye na asili wala historia.
Ni viongozi wachache mno wa harakati za mwanzo za huru walioingia uwanjani wakilielewa hili. Wengi hawakuelewa kuwa uhuru maana yake ni kufanya kazi na kujitegemea. Uhuru pia ni njia ya maisha huru ya watu katika juhudi za kuishi, na kuendelea kuishi kama taifa huru lenye mifumo yake huru kisiasa, mila na desturi, dini, mifumo ya imani na mfumo wa utoaji haki.
Raia Mwema