Rais mtaafu Kikwete akitoa ushauri wa jinsi ya kuongoza nchi atatoa ushauri huu?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,205
12,702
Wakati wa uongozi wake aliwahi sema kuwa watu wasimuandame kuwa anasafiri sana. Alisema kuwa huko watu wanapesa sana hivyo ni muhimu atoke akahemee.

So kama JK akiombwa ushauri wa kuongoza nchi bila shaka ushauri wa kutoka na kuomba kwa kila anayeonekana ana pesa utakuwa ni wa kwanza kabisa kutoa.

Pengine si vibaya kusafiri na kuomba pesa huku na kule hasa kwa kipindi hiki cha mdororo. Mficha maradhi. Lakini tukumbuke Nyerere alivyosema kuwa nchi maskini haiwezi kuendelea kwa kutegemea misaada kutoka nchi za kigeni. Mtegemea cha nduguye.

Kama nchi tukae tuumize vichwa kuondokana na aibu hii.
 
Mleta mada ungemshauri kwanza Lisu anaeishi kwa misaada ya wanaume huko ubelgiji. Wao (mabeberu) waliiba rasilimali zetu toka enzi za ukoloni kwa njia hii, na sisi tunazirudisha kwa njia ile. Tatizo liko wapi?
 
Ustawi wa Nchi yetu "Tanzania'' hautakuja kama miujiza ila nikwajuhudi na ubunifu wetu sisi wenyewe Watanzania kujikomboa.

Viongozi wetu sio malaika wanatoka miongoni mwetu hivyo tisiwategemee sana ila tujitizame na tutikize wajibu wetu kikamilifu.
 
Mleta mada ungemshauri kwanza Lisu anaeishi kwa misaada ya wanaume huko ubelgiji. Wao (mabeberu) waliiba rasilimali zetu toka enzi za ukoloni kwa njia hii, na sisi tunazirudisha kwa njia ile. Tatizo liko wapi?
Wakoloni hawakuiba kitu cha kutufanya kuwa masikini. Ardhi bado ipo, madini bado yapo tena mengi tu, maji bado yapo, gesi bado ipo. Viongozi wa Africa hadi leo wakiiba wanasingizia wakoloni ndiyo wameiba. Ishu ya kitoto sana.
 
Kuna jamaa mmoja anataka kuturudisha kwenye ukoloni kupitia mgongo wa beberu amu stedamu. Bahati nzuri watanzania tumeshtuka.
 
Wakati wa uongozi wake aliwahi sema kuwa watu wasimuandame kuwa anasafiri sana. Alisema kuwa huko watu wanapesa sana hivyo ni muhimu atoke akahemee.

So kama JK akiombwa ushauri wa kuongoza nchi bila shaka ushauri wa kutoka na kuomba kwa kila anayeonekana ana pesa utakuwa ni wa kwanza kabisa kutoa.

Pengine si vibaya kusafiri na kuomba pesa huku na kule hasa kwa kipindi hiki cha mdororo. Mficha maradhi. Lakini tukumbuke Nyerere alivyosema kuwa nchi maskini haiwezi kuendelea kwa kutegemea misaada kutoka nchi za kigeni. Mtegemea cha nduguye.

Kama nchi tukae tuumize vichwa kuondokana na aibu hii.
Mkuu Likoni Pikitusi, Lycaon pictus , sio kila ziara ni kwenda kuhemea!. Ziara nyingine ni kuhudhuria mikutano muhimu inayohitaji resprentation ya head of state.

Safari nyingine ni muhimu sana kwa rais wetu kupata kitu kinachoitwa exposure na ziara nyingine ni just recreational na ku refresh akili inatulia ina relax ina refresh akirejea anakuwa more energetic!.
P
 
Mama aka relax akirudi awe imara kuamua kwa facts sio kuogopa kivuli wanamtisha bure mili kutimiza yao...mfano kesi Mbowe ni kubumba wanatumia kodi zetu vibaya....awe maamuzi magumu yeye mkubwa zaidi Sirro ....Msuya hata Mabeyo..
 
Wakati wa uongozi wake aliwahi sema kuwa watu wasimuandame kuwa anasafiri sana. Alisema kuwa huko watu wanapesa sana hivyo ni muhimu atoke akahemee.

So kama JK akiombwa ushauri wa kuongoza nchi bila shaka ushauri wa kutoka na kuomba kwa kila anayeonekana ana pesa utakuwa ni wa kwanza kabisa kutoa.

Pengine si vibaya kusafiri na kuomba pesa huku na kule hasa kwa kipindi hiki cha mdororo. Mficha maradhi. Lakini tukumbuke Nyerere alivyosema kuwa nchi maskini haiwezi kuendelea kwa kutegemea misaada kutoka nchi za kigeni. Mtegemea cha nduguye.

Kama nchi tukae tuumize vichwa kuondokana na aibu hii.
Tatizo ni kwamba tumejiwekea mindset kwamba bila wao hatuendi! Hivi inakuwaje nchi kama yetu yenye almost kila kitu tunaendelea kutegemea misaada 60 yrs after uhuru? Tunsfikiria mafanikio yapatikane overnight?! Inabidi tukaze mikanda tuondoe dhana potofu ya kufikiria kwamba hatuwezi na kuwaruhusu wafikirie kwa niaba yetu. We can if we decide to!
 
Back
Top Bottom