Rais mstaafu TLS - Mfumo wa Haki Jinai Tanzania uundwe upya, haki ipatikane

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,293
24,173
Dr. Rugemeleza A.K Nshala, rais mstaafu wa Tanganyika Law Society TLS amesema mfumo wa Jinai Haki ( Criminal Justice System) wa nchini Tanzania unahitaji mabadiliko makubwa kwa kufumuliwa na uundwe upya ili kulinda haki za raia na watu .


Azungumzia mazito kuhusu

  • Nolle prosequi / kufutiwa mashtaka bila kuelezwa sababu za msingi zaidi ya ofisi ya DPP kusema imeamua kutoendelea na mashtaka
  • Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka DPP
  • Makubaliano kati ya raia na kitu kinachotisha kikubwa yaani raia asiishitaki serikali akiachiwa pia asidai fidia
  • Marekebisho ya sheria yanahitajika ili mahakama iweze kusikiliza haki ya dhamana na ikiwa inafaa mahakama ipewe mamlaka ya kumuachia mtuhumiwa wakati Polisi na waendesha mashtaka wakiwa wanaendelea kusaka ushahidi
  • Watuhumiwa wengi wanaozea ndani ya mahabusu gerezani kwa muda mrefu wakati inadaiwa vyombo vinaendelea na upelelezi
  • Mtuhumiwa siyo mhalifu mpaka hapo atakapo pata haki yake kwa kuhukumiwa na Mahakama.
  • Hii ya mtuhumiwa kuhukumiwa na Polisi, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka au kiongozi yeyote ni uvunjifu wa haki za raia na katiba.
  • Wenye jukumu la kurekebisha mfumo huu Jinai Haki, ni serikali iliyopo madarakani kwa kutumia wataalamu wake na bahati kuna wasomi bobezi waliopo ofisini , ni kama Mwanasheria Mkuu Jaji Dr. Feleshi, Waziri wa Sheria Prof. Palamagamba na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Wadau wengine kama TLS, Kituo cha Haki za Binadamu, Vyombo vya Habari na wananchi ni kupaza sauti na kupigia kelele mfumo huu mbovu wa Haki Jinai uliopo sasa hivi.
  • Polisi hawawezi kulaumiwa, wao Polisi hawana jukumu lolote bali kupiga saluti na kutekeleza amri na sheria hii mbovu inayoendesha Mfumo Haki Jamii ( Criminal Justice System) kama wanavyoelekezwa na viongozi wanaowaongoza jeshini na wanasiasa serikalini.
  • Watanzania tuamke toka dhamira zetu zilizo mfu, tupiganie haki hii wote kabisa bila kujali vyeo vyetu, vyama vya kisiasa, itikadi n.k

Rugemeleza Nshala, holds Doctor of Juridical Studies (S.J.D) from the Ivy league Harvard Law School. He holds a Bachelors of Laws Degree (LL.B) from the University of Dar es Salaam, Tanzania (his home country), which he obtained in 1993; the Masters of Laws Degree (LL.M) from Harvard Law School and Masters of Environmental Management (MEM) from Yale School of Forestry and Environmental Studies that he obtained in 1997 and 2007, respectively. Source : Harvard African Development Conference
 
Katiba Mpya ndio maana inapigiwa kelele, itakuja kutibu hayo yote aliyoainisha hapo juu, siasa imeharibu sana muhimili wetu wa mahakama, inatakiwa pawepo na utaratibu mpya kuanzia uteuzi wa majaji/hakimu, utendaji wao, DPP uteuzi wake na mamlaka yake yachekiwe, tuanze upya kama taifa linaloheshimu misingi ya haki za raia wake.
 
Wewe ulikuwa Rais wa Tls,kwani unachokieleza hukukiona wakati ukiwa Rais?

Anajinasibu kuwa mwanataaluma sasa wakati aliakua ametulia tuliiiii.... tena wala sidhani kama aliwahi kuipitia hiyo sheria hadi alipoguswa mzee wetu Rugemalila.

Uzuri ni kwamba alijua sheria itawahusu kina fulani tuu kumbe sheria haichagui.

Ni fundisho kubwa hilo kwa wanataaluma wetu sio wa sheria tuu hata wengine
 
Katiba Mpya ndio maana inapigiwa kelele, itakuja kutibu hayo yote aliyoainisha hapo juu, siasa imeharibu sana muhimili wetu wa mahakama, inatakiwa pawepo na utaratibu mpya kuanzia uteuzi wa majaji/hakimu, utendaji wao, DPP uteuzi wake na mamlaka yake yachekiwe, tuanze upya kama taifa linaloheshimu misingi ya haki za raia wake.

Kusipokuwako umakini hata hiyo katiba mpya inayopiganiwa na wanaotaka kushika dola inaweza kuja na ikawa mbovu zaidi ya katiba iliyopo
 
Anajinasibu kuwa mwanataaluma sasa wakati aliakua ametulia tuliiiii.... tena wala sidhani kama aliwahi kuipitia hiyo sheria hadi alipoguswa mzee wetu Rugemalila.

Uzuri ni kwamba alijua sheria itawahusu kina fulani tuu kumbe sheria haichagui.

Ni fundisho kubwa hilo kwa wanataaluma wetu sio wa sheria tuu hata wengine
Wewe ni mwehu,hao TLS wana mamlaka gani ya kubadili mfumo mzima wa Sheria mbovu za katiba mbovu ya CCM?
 
Kusipokuwako umakini hata hiyo katiba mpya inayopiganiwa na wanaotaka kushika dola inaweza kuja na ikawa mbovu zaidi ya katiba iliyopo
"Kusipokuwepo umakini".... inayopiganiwa na "wanaotaka kushika dola" naona umejaribu kutafuta weakness but sadly hujaipata, ukaamua kujishikiza kwenye kupiga ramli tu.

Usimchukie mtu kwa maoni yake, na haijalishi kayatoa wapi, na lini, ni haki yake kikatiba, kumtaka afunge mdomo ni udikteta wa kike.
 
Alipokuwa na nafasi ya kimadaraka kwanini hakushauri wala kufanya chochote kuhusu hiyo 'criminal justice reform' anayoihubiri leo?

Viongozi wa nchi hii wamejaa unafiki nafiki na umbayuwayu.

-Kaveli-
 
21 Mar 2021
RAIS WA TLS ATOA TAMKO KWA RAIS WA TANZANIA SAMIA SULUHU, WALIOFUNGULIWA KESI ZA KUBAMBIKIWA WAPEWE HAKI, SERIKALI IWE WAZI
Kwa niaba ya baraza la uongozi la TLS, Dr. R Nshala
 
Hivi mnasema alikuwa wapi sasa huyu mama yeye kipindi kile anapinga COVID-19 na chanjo vile vile yeye alikuwa wapi.

Mbona leo ametambua uwepo wa COVID-19 na chanjo amedungwa, kama huo sio unafiki ni nini. Na nyie pia acheni unafiki.
 
20 November 2020

101 : MFUMO WA JINAI HAKI
Ijue kwa kina sheria ya mfumo wa haki jinai nchini Tanzania, ili ufahamu hazi zako, za ndugu yako, jirani, jukumu la mjumbe maana wanaweza kuwa mashahidi wako au mashaidi wa Jamhuri



Utu wa mtu ni msingi katika mwenendo
  • Ukamataji / arrest ufanyike kwa njia ya sheria
  • Mtuhimiwa aoneshwe RB , warrant of arrest au hakimu / jaji atoe amri na mkamataji ajitambulishe
  • Upekuzi
  • Wapekuzi wakaguliwe
  • Wapekuzi hawastahili kubeba mabegi, mifuko na kuingia nayo ndani ya eneo la upekuzi kuzuia bangi au kete za madawa ya kulevya kupachikwa kijanja
  • Kufikishwa polisi
  • N.k
Source : ITV TANZANIA
 
Jamhuri (Serikali) hubeba mashtaka yote kwa niaba yetu, sababu ni nini? Majibu yapatikana hapa chini toka kwa wakili msomi

Sn.1 Ep.5 Sheria za Jinai



Kwanini Jamhuri ni sehemu muhimu katika kesi za jinai, yaani umeumizwa au kuibiwa lakini anayeshitaki ni Jamhuri na wewe mhanga (mlalamikaji) huwa ni shahidi
Source : Hope Channel Kenya
 
Sheria haziwezi kubadirishwa mpoka kuwe na critical event kwenye jamii. Kesi kama hii ya Mbowe inaweza saidia sababu Jamii inaamini Mbowe anaonewa sio kama ya mzee luge ambaye jamii ilikuwa inaamini ni mwizi.
 
Bado tuna sheria nyingi kandamizi kwa mfano ile inayomruhusu DPP kufuta kesi bila kutoa maelezo/sababu yoyote, ile ya mtu kushinda kesi kisha asidai fidia kwa usumbufu na uonevu aliopata.

Dhamana iwe ni haki ya mtuhumiwa kwa tuhuma yoyote ile, kwa mfano hapo Kenya kuna Gavana ana tuhuma ya mauaji lakini yeye na wenzake wako nje kwa dhamana na kesi inaendelea.

Nchini Uganda, kuna kipindi Bobby Wine alitiwa nguvuni akituhumiwa kwa kosa la uhaini kufuatia msafara wa rais Museveni kupigwa mawe na mashabiki wake kz mwa Uganda lakini walipewa dhamana hadi akaruhusiwa na mahakama kusafiri kwenda Marekani kutibiwa kufuatia kipigo alichopata kutoka kwa watu wa usalama wa Uganda na aliporejea aliendelea na kesi na kushinda.

Nchini Tanzania kuna msururu wa tuhuma nyingi ambazo eti mtuhumiwa haruhusiwi kupewa dhamana hii sio haki na ni uonevu uliopitiliza na eti hata usipotiwa hatiani pia hauna haki ya kudai fidia..!!!

Fikiria, unamfungulia mtu kesi ya uhujumu uchumi kwa unavyofikiria wewe wakati kumbe sio uhujumu uchumi na baada ya kusota gerezani miaka mitano anaachiliwa huru na hawezi kudai fidia yoyote kisha nchi inadai eti inafuata utawala wa sheria. Hovyo sana.
 
Wewe ulikuwa Rais wa Tls,kwani unachokieleza hukukiona wakati ukiwa Rais?
Ndio matatizo ya kuishia darasa la 3C!!

Kwani kuwa Rais wa TLS ndio kunampa fursa/mamlaka ya kubadili mfumo? Kama ungekuwa umeishia japo darasa la saba, ungeweza kuiona paragrafu iliyoandikwa kuwa, "Mwenye jukumu la kuweza kubadili mfumo huu ni serikali iliyopo madarakani kwa kutumia wataalamu wake wabobevu"

Wakati unaambiwa usiwe mtoro wa shule, ulikuwa unaona kama wanaokusisitiza kusoma ni wajinga
 
Back
Top Bottom