Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Baada ya maswali mengi kuzagaa kuwa wastaafu wa CCM na serikali yake aidha wamemsusa JK au wamesoma alama za wakati na kuingia mitini, Raisi Mstaafu Mwinyi alionekana ITV taarifa ya saa mbili usiku akimnadi Jk na wagombea wengine wa ubunge wa Kawe na kata ya Mbweni kwa udiwani.
Lakini ukilinganisha na mahudhurio ya Chadema jana hapohapo Kawe utaona kwa uwazi ya kuwa kweli ushawishi wa Mzee Rukhsa sasa umefikia ukingoni kwani ni watu wachache walijitokeza na wengi wao ni watoto ambao hata hivyo hawatapiga kura. Mahudhurio hayo yalikuwa yanasononesha kabisa moyo na walikuwa kama wanaonekana ni wakiwa vile kwa kujua hatma ya CCM iko ukingoni musimu huu.
Ushauri wangu JK angelimwachia mzee wetu ale pensheni yake bila zengwe lolote kwa sababu hana mchango wowote ule kwenye kampeni za mwaka huu.