Rais mstaafu Kikwete kwa hili umetukosea sana Watanzania

pantheraleo

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
690
841
Kauli yako katika clip hii ni kitisho kwa Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wetu Mheshimiwa Dokta Samia Suluhu Hassan.

Naomba nikukumbushe kwamba hayati Rais Dokta Magufuli alifanya kila jitihada kuhakikisha anakuweka mbali wewe na watu wako ili aweze kuongoza nchi vizuri. Alifanya kazi kubwa kurekebisha yale ambayo ama hukuyafanya katika awamu yako au yale ambayo ulifanya vibaya ikiwemo kupambana na rushwa, ufisadi na nidhamu katika utumishi wa umma. Naomba nikukumbushe pia kuwa ni wakati wa utawala wako kuna “mambo yaliharibika kweli kweli” lakini bado 2010 chama kikakupitisha na hakuna aliyekutisha kwamba linaweza kutokea jambo. Wizi wa mabilioni zaidi ya 130 wa EPA, ufisadi wa kila kona ya nchi, mikataba ya nchi kusaini mahotelini Ulaya, na mamia ya matukio mengine ya ufisadi mkubwa wa mali za umma. Haya yote yalikuendea mrama na wakati ule Dokta Slaa ilionekana wazi angekuwa alikuwa na nguvu mbele ya wananchi kuliko wewe. Lakini kina mzee Mkapa hawakusema kwamba “mambo yameharibika” hufai kugombea. Chama kilijua hutapata matokeo mazuri 2010 lakini bado kikachukua risk kukupitisha.

Leo tunamuongelea Samia ambaye katika muda wake wa miaka karibu miwili amekuwa na nguvu ya kusimamia miradi mikubwa aliyoacha JPM na kuhakikisha inaendeleea. Tunamuongelea Samia ambaye katika muda wake mfupi anakaribia kumaliza changamoto kama ya madarasa ambayo imedumu toka uhuru. Tunamuongelea Samia ambaye ameamua kukaa mbali na wewe na watu wako hata kwenye uchaguzi wa wajumbe wa NEC ambako majina ya watu uliopenyeza yalikatwa. JPM alikunanga na kukutenga waziwazi hata kutuma watu kukutukana na kufuta wabia wako kibiashara, Samia muungwana hafanyi hayo, basi tumia busara. Tunakusihi uache vitisho kwa Mheshimiwa Rais. Tunaamini vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na wabobezi wa siasa watakwambia kwa uwazi kuwa kauli hii haifai kuambiwa kiongozi mkuu wa nchi ambaye tayari katika muda mfupi ameonesha uwezo mkubwa katika uongozi.


Ndimi Luqman
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom