Rais Mstaafu Kikwete aliwahi kulalamika kutengwa na majirani zetu, siyo wa kuwaamini sana

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,174
27,217
Mimi binafsi Kuna mengi ambayo nimefurahi hasa kwenye ziara ya Mama huko Kenya, ikiwemo kuwauzia gesi maana tutapata faida kubwa.

Kikwete anahesabika moja ya maraisi wapole,wenye busara na diplomasia ya Hali ya juu. Lakini pamoja na yote hayo Mh. Kikwete aliwahi kupata shuruba ya Hawa majirani hasa Kenya tu kwa sababu ya kuwakatalia baadhi ya mambo yao waliokuwa wakihitaji.

Kikwete kwa haiba aliyonayo na alivyokuwa akisemwa kuwa anachekacheka basi isingekuwa ngumu kwake kukataa hayo mambo, Ila hadi anadiriki kukataa tafsiri yake Kuna vitu alivyiona.

Mama Samia Mimi ni mfuasi wako, hivyo pamoja na Huo ujirani mwema Kuna vitu inabidi kuvikataa katakata, Wala ukwepeshe.

Kwenye kikao wanakubaliana wakatae kusani ila nyuma ya pazia Kenya anaenda kusaini, mfano ni: EPA
Ilifikia kipindi wakawa wanafanya meetings za EAC bila hata kumjulisha Mh. Kikwete.

Hivyo Mama nakuomba usifurahie Sana maneno yao matamu bali Pima maslahi ya watanzania.

Chini ni habari ya kipindi hicho 2013 Kikwete akilalamikia Hawa majirani zetu.

Zaidi soma > Hotuba ya Rais Kikwete, Bungeni Dodoma - Novemba 07, 2013

Eac.jpg
 
Jirani 254 ni wakora sana toka enzi za mwl Nyerere. Walijimilikisha mali za jumuia ya Afrika Mashariki wakati jumuiya inavunjika mara ya kwanza, usitegemee watakuwa watu wema kwetu kama tunavyodhani.

Kama kuna mtu alikuwa mvumilivu kidlomasia alikuwa Mwl. Nyerere, ila kuna wakati mipaka ya nchi zetu mbili ilifungwa kabisa; wakati wa JK wakaunda kundi lao la "muungano wa walio tayari".

Hawa ni watu wa ndimi mbili na they are not dependable and reliable. Suala la Uhuru kuvutia wawekezaji toka kokote ikiwamo East Africa amekuwa akiimba mdomoni ila kwa vitendo ukifika kwao mizengwe iliyopo, Rostam kasikika leo akizungumzia namna anapigwa sound kwa miaka 4.

Tunarejea juzijuzi hapa walikataa mahindi ya Tanzania eti yana sumu kuvu; baada ya muda imethibitika hayana sumu kuvu na hapajawahi kuwa na apology kwa ku-paint picha mbaya juu ya Tanzania.

Mwaka jana wakazuia vitunguu, carrots, nyanya, ginger ati wanaweza kulima wao wenyewe ndani, then hasara imepatikana kwa wafanyabiashara wadogo, mara Rais wao anajirudi tena.

Mwaka jana wakazuia Watanzania tusiingie nchini kwao kwa kuwa "tuna corona"; ila ndege zao au magari yao kuja huku sawa tu. Tulipo-reciprocate wakamtuma Balozi wao haraka haraka na akasema, unajua sisi ni ndugu.

Ni jirani mwenye hila na mkora sana na tuna wajibu kuishi nae kwa akili ila tujue tu wakati wowote anaweza kutugeuka.

Tuingie nao mikataba kwa tahadhari sana.
 
Mimi binafsi Kuna mengi ambayo nimefurahi hasa kwenye ziara ya Mama huko Kenya, ikiwemo kuwauzia gesi maana tutapata faida kubwa.

Kikwete anahesabika moja ya maraisi wapole,wenye busara na diplomasia ya Hali ya juu. Lakini pamoja na yote hayo Mh. Kikwete aliwahi kupata shuruba ya Hawa majirani hasa Kenya tu kwa sababu ya kuwakatalia baadhi ya mambo yao waliokuwa wakihitaji.

Kikwete kwa haiba aliyonayo na alivyokuwa akisemwa kuwa anachekacheka basi isingekuwa ngumu kwake kukataa hayo mambo, Ila hadi anadiriki kukataa tafsiri yake Kuna vitu alivyiona.

Mama Samia Mimi ni mfuasi wako, hivyo pamoja na Huo ujirani mwema Kuna vitu inabidi kuvikataa katakata, Wala ukwepeshe.

Kwenye kikao wanakubaliana wakatae kusani ila nyuma ya pazia Kenya anaenda kusaini, mfano ni: EPA
Ilifikia kipindi wakawa wanafanya meetings za EAC bila hata kumjulisha Mh. Kikwete.

Hivyo Mama nakuomba usifurahie Sana maneno yao matamu bali Pima maslahi ya watanzania.

Chini ni habari ya kipindi hicho 2013 Kikwete akilalamikia Hawa majirani zetu.

Zaidi soma > Hotuba ya Rais Kikwete, Bungeni Dodoma - Novemba 07, 2013

Ardhi ardhi ardhi ni chanzo. Majamaa yanataka mtelemko. SSH take note
 
Back
Top Bottom