Rais Mstaafu Kikwete ahimiza uwekezaji katika elimu ya sayansi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1575026669324.png

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete amehimiza uwekezaji katika sayansi, hususani katika kipindi hiki ambacho nchi inajielekeza katika uchumi wa kati ifi kapo mwaka 2025. Aidha, Kikwete ametoa mwito kwa waajiri kuruhusu watumishi kujiendeleza kielimu isaidie kuongeza idadi ya watu wenye shahada.

Alitoa mwito huo jana kwenye mahafali ya 37 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), yaliyofanyika makao makuu ya chuo Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani. Akiunga mkono uamuzi wa OUT wa kujikita zaidi katika elimu ya sayansi, Kikwete aliwataka wasirudi nyuma kwa kuwa nchi ina mahitaji makubwa ya wanasayansi. “Maendeleo tunayozungumza yanaletwa na wanasayansi.

Haimaanishi sisi (wachumi) hatuna mchango wa maana. Lakini yale maendeleo ya mabadiliko ya watu yatakayoonekana ni ya sayansi,” alisema Kikwete. Alitoa mfano wa maendeleo ya ujenzi wa madaraja, barabara, huduma za afya kuwa ni matokeo ya sayansi.

Alisisitiza kwamba nchi isiyoendeleza wanasayansi imedumaa. Akitoa mfano wa wachumi, wanasheria, Kikwete alisema, “wote tuna mchango muhimu lakini maendeleo ya mabadiliko lazima tuwekeze katika sayansi. Hasa katika kipindi hiki serikali imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda kuipeleka nchi uchumi wa kati mwaka 2025.”

Alifafanua kwamba mwaka 2000 wakati wa uongozi wa Rais Benjamin Mkapa, ndipo ilibuniwa dira hiyo ya kuhakikisha mwaka 2025 Tanzania inakuwa na uchumi wa kati na pato la Mtanzania linakuwa dola 3,000. Kikwete alisema chini ya uongozi wake, alifanya tathimini na ukatengenezwa mpango wa miaka 15 wa namna ya kufikia mwaka 2025 nchi ikiwa na uchumi wa kati. Alielezea kwamba iliwekwa mipango ukiwamo wa kujenga uchumi wa viwanda.

“Mimi niliendeleza kuupa mwelekeo na sasa inaendelea kwa kasi sana chini ya Rais John Magufuli, tumuunge mkono kwa kuwekeza kwenye sayansi,” alisisitiza.

Rais Mstaafu alieleza furaha yake ya OUT kuendelea kuzingatia malengo ya kuanzishwa, ambayo ni kutoa elimu ya juu kwa wanaojiendeleza.

“Nafarijika kuona chuo hiki hakijachepuka kutoka katika dhamira na dhima yake licha ya kuwa na vishawishi vingi imeendelea kuwa kimbilio hata la watu kutoka nje ya nchi,” alisema.


Chanzo: Habari Leo
 
Kuongeza watu wenye shahada ndio kuwekeza katika sayansi??
Sayansi ni zaidi ya shaada sayansi ni kipaji. tunasoma sayansi darasani just to be able to explain kile tunachokifanya kila siku. Nchi inataka watu wanaoifanya sayansi na sio wanaoisoma sayansi.
 
Back
Top Bottom