Rais Mstaafu J. Kikwete: Safari zimenifunza ni heri "Mtembea bure kuliko Mkaa Bure"

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
DaQaONUXcAAcqFo.jpg

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, amesema safari mbalimbali alizozifanya akiwa madarakani na anazozifanya sasa hivi, zimemsaidia kujifunza na anaendelea kujifunza mambo mengi zaidi.

Kikwete anasema miongoni mwa mambo hayo ni namna ambavyo nchi nyingine hasa zilizoendelea zinavyokabiliana na vifo vitokanavyo na uzazi.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam juzi usiku katika hafla ya kusherehekea miaka mitano ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Childbirth Survival International (CSI), inayoelimisha jamii kuhusu masuala ya uzazi salama.

“Wanasema heri kutembea bure, kuliko kukaa bure, nimekaa bure Msoga lakini nimetembea nimeona, wenzetu wamewekeza mno katika suala la afya ya mama na mtoto,” alisema.

Kikwete alisema kina mama wengi na watoto wanafariki dunia kwa matatizo na magonjwa yanayoweza kuzuilika.

“Maisha ya mama na mtoto yanapotea kila siku, lazima …

Chanzo: MTANZANIA
 
Kukaa bure, kutesa na kunyanyasa waliotofauti naye

Hakai bure anaharibu uchumi wa watu nataifa kwa ujumla

Yeye kusherekea kambomba ka ndege majirani wa madege aibu sama
 
Ila huyu mzee JK anatuchora sana aisee.

Yani yeye zile fadhila za ustaafu wa rais unambeba sana.

Yani huwezi amini hasi MaPM waliopita wansomeshwa namba.
 
Ukweli mtupu hili garasa lenyewe lugha ni tatizo

Waswahili hatuna jema. JK alivyosafiri mlimuita Vasco dagama. Leo mnamsifia kwa safari hizo hizo! Kipi kimebadilika? Leo JPM hasafiri tunamuita Kilaza! na kebehi za kila aina!

Duh... uongozi msalaba mzito sana! Inabidi mtu ujitoe ufahamu...walimwengu wakiamua kukuchukia hata ungefanya nini...watakuchukia tuu!
 
Ila huyu mzee JK anatuchora sana aisee.

Yani yeye zile fadhila za ustaafu wa rais unambeba sana.

Yani huwezi amini hasi MaPM waliopita wansomeshwa namba.
Acha waisome vizuri maana walipoambiwa kuhusu katiba walikuwa wananuna wanaona haiwahusu,wakati nafasi walikuwa nayo, hata jiwe haliwezi ona umuhimu wake hadi litakapokuja someshwa no
 
Waswahili hatuna jema. JK alivyosafiri mlimuita Vasco dagama. Leo mnamsifia kwa safari hizo hizo! Kipi kimebadilika? Leo JPM hasafiri tunamuita Kilaza! na kebehi za kila aina!

Duh... uongozi msalaba mzito sana! Inabidi mtu ujitoe ufahamu...walimwengu wakiamua kukuchukia hata ungefanya nini...watakuchukia tuu!
Tatizo sio kusafiri au Kutokusafiri, tatizo ni kupitiliza katika hayo.
Wanaomkosoa Kikwete wanajenga hoja kws kitendo cha Kikwete kusafiri sana. Na sio kusafiri tu, maana Nyerere, Mwinyi na Mkapa wote walisafiri nje, na safari zao hazikuwa mjadala.

Sasa jiulize kwanini ukosoaji uwe kwa Kikwete na Magufuli tu?
Maana yake kuna tatizo mahali.
 
Back
Top Bottom