Rais mstaafu hunyanyaswa na aliye madarakani? Wote wana mishahara mikubwa sana

eliesikia

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
787
755
Masharti ya kazi ya Rais Sheria ya 1984 Na.15 ib.9
1) Rais atalipwa mshahara na malipo meingineyo, na
atakapostaafu atapokea malipo ya uzeeni, kiinua mgongo au
posho, kadri itakavyoamuliwa na Bunge, na mshahara, malipo
hayo mengineyo, malipo ya uzeeni na kiinua mgongo hicho,
vyote vitatokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano na vitatolewa kwa mujibu wa masharti ya
ibara hii.
(2) Mshahara na malipo mengineyo yote ya Rais
havitapunguzwa wakati Rais atakapokuwa bado ameshika
madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.


Leo nimeamua kupitia sheria ibara ya 15 na kugundua mapungufu makubwa.. Nimekumbuka sheria hii kwa kuwa raisi aliyeyoko madarakani ni marufuku kujadili mshahara wake<<sio haki hata kidogo>>... Dr.Slaa aliamua kwamba mshahara wake utapunguzwa kwa asilimia 15... Sheria hii imejaa majungu kwa kuwa inasema wazi kuwa hautapunguzwa.

Mimi nawasilisha hoja lakini naomba CHADEMA waweze kufikisha bungeni hili ili ikiwezekana au ikigundulika mshahara wa mil45 ni mkubwa na lazma upunguzwe kwa vyovyote... isipowezekana ni lazma operesheni sangara itembezwe nchi nzima... Mshahara wa raisi ni mkubwa na lazma upunguzwe na wastaafu pia wapunguzwe 80% is too large hata kama tunaogopa wasifanye biashara wakiwa ikulu!!!!
 
Bado kuna sheria ibara siikumbuki inadai kwamba ni siri lakini mtaani wanadai mil45
 
Naona kweli au ni macho yangu! yahani unasema rais mstaafu wa bongo hulipwa aslimia 80 ya mshahara wa rais aliyoko madarakani, au Tsh36milioni kwa mwezi! Hii ni mbali na marupurupu mengineyo ambayo nayo yanatisha. Kweli viongozi hawa ni mzigo kwetu.
 
Back
Top Bottom