mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,168
- 1,071
Tanzania tumekuwa na viongozi shupavu na makini kitaifa na kimataifa.
-Kutokana na ukubwa wa taifa letu kieneo ukilinganisha na majirani zetu
-siasa chafu zilizoshamiri kwa mgongo wa kinachoitwa demokrasia,
-umaskini wa kifikra kwa Watanzania tulio wengi,
-Changamoto za kimazingira {Umaskini/ufukara} na
-mapungufu ya mfumo wa elimu katika kuandaa wengi kukabiri changamoto za kimaendeleo..
-n.k
Imekuwa ni vigumu sana kuthamini na kuheshimu michango ya viongozi waandamizi hasa wanapotoka madarakani.Imekuwa desturi ya kuwa ni rahisi sana wanadamu kusahau mema mengi aliotenda mwanadamu mwenza kuliko mabaya machache.
Nadiriki kunena ya kuwa Rais Mstaafu B.W. Mkapa ni moja ya viongozi shupavu,bora,makini na anayepaswa kuheshimiwa kwa alioyafanya katika kujenga msingi wa maendeleo endelevu katika taifa hili.Yapo matunda mengi tunavuna leo ikiwa ni mavuno ya mazao yaliopandwa katika utawala wa Mh.Mkapa si katika maendeleo ya Jamii {Afya,elimu,makazi,n.k},Siasa,Usalama,Diplomasia,Uchumi na Sayansi...
Tusiache kutafakari kwa kina na kurejea historia chanya hasa katika inshu zinazohusu maendeleo ya taifa kwa ujumla.Yapo mapungufu pia katika utendaji wake yaliohusisha watendaji waandamizi,Maswahiba kisiasa na wateuliwa wasio waaminifu.Mapungufu husika hayana budi kubebwa nae sababu ya uwajibikaji wa jumla/pamoja ambayo kibinadamu hayaepukiki kutokana na sababu mbalimbali kiutendaji,kiusimamizi na kiufuatiliaji mfano Ufisadi,wizi,Rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.