Rais Mseveni aruhusu shughuli za uchumi kufunguliwa tena baada kufunga kwa takriban miaka miwili

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,545
Shuguli zote za kiuchumi zimefunguliwa tena nchini Uganda leo Jumatatu baada ya kufungwa kwa baadhi ya biashara kwa karibu miaka miwili.

Baa, vilabu vya usiku, kumbi za michezo na maeneo mengine ya burudani pamoja na shuguli nyingine za usiku vimefunguliwa rasmi baada ya kufungwa mwezi Machi, 2020.

Baadhi ya vilabu vya pombe na maeneo mengine ya burudani yamekuwa yakihudumia idadi chache ya watu, huku maeneo mengine yakifungwa kabisa.

Marufuku ya kutembea wakati wa usiku pia imeondolewa, isipokuwa kwa boda boda ambazo zinaruhusiwa kufanya kazi hadi saa moja jioni.

Katika hotuba yake ya kumaliza mwaka, Rais Yoweri Museveni aliagiza kwamba shuguli nyingine za kiuchumi zinaweza kufunguliwa tena wiki mbili baada ya kufunguliwa kwa shule.

Source: Star TV
 
Back
Top Bottom