Rais mpya wa Gambia Baroow, awakamata maafisa wakuu wazamani wa USALAMA

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
8,106
3,967
Rais Barrow wa Gambia ameanza kuweka mizizi ya utawala wake. Baada ya kuwakamata na kuwaweka ndani wakuu wa ZAMANI usalama wa taifa (NIA) waliokuwa wakitumiwa sana na serikali ya zamani katika
MAUAJI,
KUPOTEA kwa wapinzani
ikiwa ni pamoja na UBAKAJI na
UTESAJI wa kutumia UMEME (Electric shock)

Miongoni mwao ni Yankuba Badjie aliyekuwa ni Mkurugenzi wa shirika la NIA- National Intelligence Agency.
Na Sheik Omar Jeng aliyekuwa ni mkurugenzi wa Operesheni.
Wote hawa wanatuhumiwa kufanya maovu mengi latika kipindi chote cha utawala wa Jammeh wa miaka 22 aliyeshindwa katika uchaguzo wa mwaka jana.
Pia watu 76 wanachama wa chama cha Jammeh waliokuwa wamefanya maovu dhidi ya wale waliokuwa wakimuunga mkono rais wa sasa Barrow nao wamekamatwa kwa kuhusika na maovu.

Rais Barrow ameamua kubadilisha jina la kitengo hicho na kukipa jina jipya State Intelligence Agency( SIA) Na kuwanyima MAMLAKA ya kumkamata mtu yeyote.

Huku akiwaambia wabaki tu katika kazi ya KUKUSANYA intelijensia Kuzi ANALYZE na KUVISHAURI vyombo husika vya serikali pekee.
Chanzo:News agencies
 
Hili liko pote Africa na yatawapata wengi! Time will tell
 
Kuna kipindi ilikuwa heshima kubwa kufanya kazi usalama wa Taifa ila for now ni historia, muda unakimbia Sana !
 
Kwa maana hiyo SIA hawatakuwa na kazi yakukamata? Hii maana yake nini? Sasa si atalazimika tu aunde section ndani ya SIA ipewe jukumu ka kukamata sivyo? Kwa mfano MI6 ya ungereza inakitengo section 20 kazi yao inakuwa sio tu kutafuta taarifa pia kazi yao ni kukamata (na hapa wanauwa sana tu). Hii kazi ya intelligence sio kama polisi wakawaida japo polisi wanaweza saidia kwenye kazi. Kwa kawaida intelligence units inaundwa na special forces. Ndani ya special forces inaundwa na commandos.
 
Back
Top Bottom