Rais mpya ajaye baada ya uchaguzi wa oktoba unashauri aanze kushughurikia nini ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais mpya ajaye baada ya uchaguzi wa oktoba unashauri aanze kushughurikia nini ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MZALAMO, Oct 18, 2010.

 1. M

  MZALAMO JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 471
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 60
  Ndugu wana JF kwa kuwa matatizo ya nchi hii ni mengi kupindukia kwa hivi sasa kama vile mfumuko mkubwa wa bei, umaskini mkubwa kwa wananchi walio wengi, elimu duni,ufisadi,rushwa, katiba ya nchi isiyokidhi kiwango, mishahara midogo kwa wafanyakazi, miundombinu mibovu, kutofaidika na mapato yatokanayo na madini, n.k. Mgependa rais mpya ajaye aanze kushughurikia tatizo gani kwanza?
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ufisadi sababu ndo kitu kinachoisumbua nchi! UFISADI NA RUSHWA!
   
 3. gillard

  gillard JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 227
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 60
  nafikiri kitu kibubwa sana cha kuanza nacho ni kubadili katiba ili tupate
  katiba itakayowezsha mambo mengine kwenda vizuri nafikiri katiba ni nguzo kubwa sana katika maendeleo ya nchi yoyote.
   
 4. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Aanze na kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wakuu wa ufisadi na ahakikishe sheria inachukua mkondo wake, hawa ndo wanalididimiza Taifa lisisonge mbele, pia mikataba mibovu ya madini maana tunaibiwa kwa kiasi kikubwa mno.
   
 5. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Aanze na kurudisha pesa yetu iliyoporwa na mafisadi. halafu ndo aingie kwenye suala la mabadiliko ya katiba.
   
 6. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwanza kabisa Afunge Kiwanda cha Neti badala yake.......tutokomeze MAzalia na vyanzo vya mmbu......

  Ashughulikie Policies mbali mbali,
  Asimamie Utawala wa sheria Kiukweli kabisa. Yaani kama ilivyo upanga hukata pandembili.
  Sheria na Sera, taratibu za kiutendaji ziwe wazi kwa watendaji wote katika kada tofauti tofauti. Asimamie kusiwepo na uchakachuliwaji wa taratibu kwa maslahi binafsi: Kama ni upatikanaji wa zabuni kwa mfano Taratibu husika zisimamiwe ipasavyo.

  Policies ziwe wazi na zi eleze kila swala la msingi, nini kifanyike na nani wakati gani......Usimamizi madhubuti ukifuatana na na uwazi wa adhabu kwa maswala husika..................................Wasomi wapewe nafasi ku exercise wanachojjua na tupime mchango wao..............Wakwepa kodi waadabishwe na reserve ya Serikali ijiongeze kutokana na Collections za kodi zinazo ibiwa kwa sasa. Urafiki wa kinafki usio na manufaa Uachwe.
   
 7. L

  Linababy Member

  #7
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza aunde baraza la mawaziri makini lenye kujali na kusimamia maslahi ya uma, then abadilishe katiba.
  Apunguze mamlaka ya raisi kwani raisi ana mamlaka kubwa sana, ikiwa ni pamoja na safari za raisi.
  Suala la afya na elimu lipewe kipaumbele.
  Ahakikishe sekta muhimu kama vile sekta za madini zinapewa viongozi makini.
   
Loading...