Rais Mkapa na Kikwete washirikiana kuiondoa CCM madarakani

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
​Rais Benjamin Mkapa kuanzisha shule za secondary za kata huku kukiwa hakuna mipango madhubuti katika sekta za Ajira, mitaji na uwekezaji ili kukabiliana na wimbi la wanafunzi watakaohitimu kulikuwa ni chanzo cha maangamizo na kuichimbia kaburi CCM.

Uongozi wa awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete kwa kuruhusu utandawazi zaidi wakati serikali yake bado inaendesha shughuli zake katika hali ya kimazoea (inactive) kulikuwa ni chachu katika kuhalakisha kifo cha CCM na kwa kufanya hivyo, anajiandaa kuizika.

Vijana hawa hawa ambao wengi wao wamepitia shule za secondary za kata ndiyo wataiangamiza CCM na inavyoonekana kwa sasa imekuwa ni mtindo mpya (new fashion) kwa kijana kuikataa CCM na kujiunga na "wanaharakati" kama CCM kinavyowaita bila kujali kimewafanyia nini na what's after CCM.

CCM kwa sasa wanawaita hawa vijana "wanaharakati" lakini CCM ikumbuke kuwa ni wanaharakati waliowaondoa wakoloni nchini na katika dunia hii, mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa au kijamii huchochewa na kuletwa na wanaharakati.

It's a "wind of change bomb" waiting to explode and CCM watch out.
 
CCM haikuwa na mpango kabisa kuwapeleka watu shule, ni mashinikizo kutoka nje. Kwani serikali ilishatoa hata senti moja kwenye hizo shule za kata? Ni misaada ya wafadhili na wananchi wanajichangisha wenyewe. Ndo maana hata waalimu wa hizo shule serikali haiwajali.

Kuanza kwa vyama vya upinzani ni mashinikizo pia. Ila sikia CCM wanavyotamba eti waliruhusu wao!!!
 
Asante baba Mkapa kuanzisha hizi shule. Na kwa vile sisi WALIMU hatujaliwi tunayo kazi moja kubwa zaidi ya kufundisha URAIA kwa kasi mpya na ari zaidi kwa wanafunzi na jamii nzima. Na huu ndio wajibu wetu kwa taifa. Ccm oyeeeeeeeeee.
 
huo ni ukweli wala haupingiki mkapa na kikwete ndio wameua ccm kwa kasi sana. na wasitegemee kurudisha hali ya utulivu ndani ya ccm
 
mkapa alianza kuimaliza ccm kwa kuuza viwanda kwa bwerere na jk kucheka na kila m2 hata anaye mtangazia kifo!
Nanukuu ; hawa mafisadi ni hatari sana kwa taifa hatuwezi kuwapeleka mahakaman ILA tutawaomba warudishe taratibu hizo pesa so mnajua wana hela nyingi sana!
 
Ila kwenye kuanzisha shule za kata Mkapa alifanya jambo zuri kwa upande mmoja na pia jambo baya kwa upande mwingine. Kwa mfano wakuu wa shule leo hii kuupata utajiri ni rahisi sana maana wanawachangisha wanafunzi michango isiyo na kichwa wala miguu, ni full kuwaibia watoto. Na pia leo hii kutokana na serikali kukurupuka kuannzisha shule hizi, vijana wengi wasio na ajira wanafundisha kwenye hizo shule tena hadi wenye div IV 32 anafundisha Math+ Physics.
.
"LONELINESS IS THE MOST TERRIBLE POVERTY".
 
sasa hvi tunawatafutia tu kaburi la kuwazika, sijui itakua makaburi ya sinza au kinondoni....
 
​Rais Benjamin Mkapa kuanzisha shule za secondary za kata huku kukiwa hakuna mipango madhubuti katika sekta za Ajira, mitaji na uwekezaji ili kukabiliana na wimbi la wanafunzi watakaohitimu kulikuwa ni chanzo cha maangamizo na kuichimbia kaburi CCM.

Uongozi wa awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete kwa kuruhusu utandawazi zaidi wakati serikali yake bado inaendesha shughuli zake katika hali ya kimazoea (inactive) kulikuwa ni chachu katika kuhalakisha kifo cha CCM na kwa kufanya hivyo, anajiandaa kuizika.

Vijana hawa hawa ambao wengi wao wamepitia shule za secondary za kata ndiyo wataiangamiza CCM na inavyoonekana kwa sasa imekuwa ni mtindo mpya (new fashion) kwa kijana kuikataa CCM na kujiunga na "wanaharakati" kama CCM kinavyowaita bila kujali kimewafanyia nini na what's after CCM.

CCM kwa sasa wanawaita hawa vijana "wanaharakati" lakini CCM ikumbuke kuwa ni wanaharakati waliowaondoa wakoloni nchini na katika dunia hii, mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa au kijamii huchochewa na kuletwa na wanaharakati.

It's a "wind of change bomb" waiting to explode and CCM watch out.

Mkuu umechanganya mambo kidogo, shule za kata ni brainchild ya awamu ya nne. Kama unakumbuka vizuri hili Lowasa alisimamia kwa nguvu kubwa sana. Na utandawazi ulishamiri na kupokelewa nchini kipindi cha Mkapa
 
Back
Top Bottom