Rais Mh. Mama Samia Ukivunja baraza la mawaziri wachunguze kila mmoja

JOESKY

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
816
2,032
Asalaam Aleykum ndugu zangu...!

Natumaini ni siku nyingine tena tumeamka tukiwa na afya tele Asante nyingi kwake Mola muumba wa mbingu na ardhi.

Siku ya leo nina ushauri mfupi kwa Rais Mama Samia atakapolivunja baraza la mawaziri basi anatakiwa amfuatilie waziri mmoja baada ya mwingine katika wizara husika. Katika awamu iliyopita (5) Kuliibuka tabia ya waziri kupewa wizara hata kama hana vigezo vya kuongoza hiyo wizara ili mradi tu una urafiki na Magufuli au ni kada mwenye wingi wa mapambio mdomoni.

Hawa mawaziri waliweza kuwa ndio chanzo kikubwa cha upotevu wa mali za taifa letu ikiwamo ufisadi wa kodi za watanzania bila huruma kabisa kwa sababu tu wamepewa rungu la uongozo hekima iliwavuka walikuwa jeuri na wakati ( ukali wao ni kuwadhibiti wanaohoji)

Ilifikia kipindi mawaziri wanasema wapo kwa ajili ya matumbo yao na sio kusimamia na kuendeleza rasilimali za taifa letu kwa maendeleo endelevu ya wananchi wetu. Ikiumiza sana pale ilipofikia hatua hata waziri anadiriki kusema atakuua kwa risasi hadharani na hakemewi (Kigwangala) huyohuyo akatuhumiwa kwa upotevu wa bilioni moja mpaka leo yupo anadunda mtaani na hajachukuliwa hatua wala mbio.

Kwa leo niishie hapa huu ni ushauri wangu kwako. Tuna imani nawe kubwa sana kuwa umeletwa na Mungu utibu majeraha ya Watanzania wengi walioumizwa kwa namna moja ama nyingine.

Nakutakia majukumu mema na Mungu akulinde.
 
Amteue waziri mkuu kua.makamu.
Baraza litakua limejivunja lenyewe.

Watakaa kupanga safu mpya kabisa.
 
Amteue waziri mkuu kua.makamu.
Baraza litakua limejivunja lenyewe.

Watakaa kupanga safu mpya kabisa.
Naona tayari mambo yamekaa sawa sasa Samia anaanza rasmi na awamu yake ya sita japo maswali bado hayaishi. Inakuwaje anateua wabunge watatu wakati wale wabunge wa viti maalum vya Rais wapo bungeni hao akina polepole?
 
Naona tayari mambo yamekaa sawa sasa Samia anaanza rasmi na awamu yake ya sita japo maswali bado hayaishi. Inakuwaje anateua wabunge watatu wakati wale wabunge wa viti maalum vya Rais wapo bungeni hao akina polepole?
Hahahahahahahahahahahah.......
Aiseh!!

Sikumbuki vizuri,hivi mwenda zake alikamilisha hesabu yake ya wale 10 kweli.
Kama hakukamilisha nafikil nafikili siombaya labda kaamua kuendelezea.
Ila kama hayati alikamilisha basi kutakua na mkanganyiko hapo mkuu.
Duh.!!
 
Hahahahahahahahahahahah.......
Aiseh!!

Sikumbuki vizuri,hivi mwenda zake alikamilisha hesabu yake ya wale 10 kweli.
Kama hakukamilisha nafikil nafikili siombaya labda kaamua kuendelezea.
Ila kama hayati alikamilisha basi kutakua na mkanganyiko hapo mkuu.
Duh.!!
Hata mimi hapa bado sijaelewa kabisa maana kama magufuli aliteua viti kumi sasa Samia amepata wapi mamlaka ya kuteua wabunge wengine watatu?? Labda kuna nafasi magufuli hakuteua
 
Back
Top Bottom