Alexism
JF-Expert Member
- Aug 14, 2011
- 3,423
- 2,046
Bila shaka wanajamvi mko salama, kwakweli nimefuatilia sana kauli za mkuu wetu wa nchi kwa muda mrefu na leo naomba niongee yafuatayo. Hakuna ubishi kua tangu Mh. Magufuli tangu uapishwe kua rais wa nchi hii na badae mwenyekiti wetu wa CCM kuna mambo umefanya vizuri lakini kuna mengi kweli umeharibu sana.
Leo naomba nijikite kwenye kauli zako ambazo unatamka dhidi ya watanzania wenzako ingawa ata huku nyuma uliwai kutamka tu nyingi. Sina haja ya kuzirudia zote kama kule Kagera ila kauli uliyotoa Zanzibar na jana kuhusu vyombo vya habari zimetuangusha sana kama Taifa mbele ya majirani na marafiki zetu. Sikuona haja ya Mh. Rais kutoa kauli yenye vitisho dhidi ya raia wako uliowaomba kura ili uwatumikie.Unaposema kuwa hamna freedom ya hivyo moja kwa moja kumbuka unaivunja katiba ya nchi yetu ambayo uliapa kuwa utailinda ingawa mpaka leo bado una imani kuwa katiba sio kitu mbele yako.
Mh. Rais kuna mambo ambayo unabidi ujikumbushe au ukumbuke ....mfano vyombo hivi hivi vya habari ndivyo vimetumika kukutafutia kura na kukunadi wewe lakini vyombo hivi hivi ndio njia rahisi unayo itumia kupeleka ujumbe kwa watanzania.
Kumbuka pia sio rahisi na jambo hili haliwezekani kuwa kila siku habari iwe ni wewe tu au mawazo na habari unazo zipenda wewe...hata DJ ana miziki anayoipenda yeye lakini akiwa kazini analazimika kucheza miziki inayopendwa na wataje.
Mwisho Mh. Rais nakukumbusha kua Taifa ili ni zaidi yako na mimi .Tusifanye au kutamka kauli za kuliangusha Taifa maana limejengwa kwa nguvu kubwa.Badirika mkuu kwa maslahi ya Taifa ili Tanzania.