Rais mfute Abubakari Kunenge Ukuu wa Mkoa. Mrudishe Makonda Tafadhali

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
3,507
2,000
Karibia week ya pili au Tatu.hatujasikia TAMKO LOLOTE TOKA KWA MKUU WA MKOA. Hakuna watu waliobagazwa au garagazwa. Mkuu wa Mkoa gani Kapoa kama supu ya sangara isiyo na ndimu?

Sisi wakazi wa Dar tulishajizoelea kubagazwa, kudhihakiwa na kugaragazwa kimwili na kiakili. Sasa mji umepoa utadhani mate ya mgonjwa inaudhi sana.

Kama haumwondoi mkuu huyu wa mkoa basi angalau aje hata na tamko kuwa hivi sasa Wanaume wa Dar hakuna kula chips mayai. Mtu akikamatwa ashtakiwe. Hapo najua tena kutachangamka. Hasa wanaume wa Kinondoni watalalamika sana.

Chadema wameandama juzi juzi hapa... hawakupigwa hata mabomu wakati maandamo tunajua yanahatarisha usalama maana yake huyu mkuu wa mkoa mpya hana hata intelejensia ya kumwambia hilo kafeli sana aende zake.

Alishindwa hata kutengeneza chaos kwenye yale maandamano polisi wetu wapate nafasi ya kuonesha utaalamu wao wa kupiga hadi kuchakaza? Polisi wanaanza kupata baridi sasa maana ni muda hawajangamsha damu.

Kiukweli Dar haina tena mchaka mchaka. Wale wanaume ambao waliotoa tu mimba kwa wanawake na hawatoi pesa za matumizi sasa hivi wanatamba mitaani kuwa hawatatoa tena pesa kwa wazazi wenzao. Wanagawa mimba tu basi.

Mkuu wa Mkoa hatujamwona akisisitiza watu wasiende mjini bila kuoga. Hatumwoni akisimulia jinsi anavyopata raha dunia hii kuliko wengine wote. Huyu hafai ni bora tu awe mzee wa kanisa au msikiti. Mkoa umepoa sana kwenye social media hamna amsha amsha kabisa.

Hata mkewe mpaka sasa hatujamjua hatutajua ana elimu gani na alisoma wapi maana amepoa hata akina Mange na Kigogo hawatamgusa... Basi atangaze followers wa Mange na Kigogo wakamatwe angalau tuone amefanya jambo.

Ni bora umrudishe Makonda aje kuanza na wajumbe waliomnyima Kula. Hawa majina atakuwa nayo tu watafunguliwa kesi ya uhaini na uhujumu uchumi. Ndiyo. Wamehujumu uchumi pakubwa tu. Why wamwambie Makonda wapo naye bega kwa bega na kumbe wapo nyuma yake?

Hiki ni kipindi kizuri kumrudisha Makonda kwenye nafasi yake. Please arudishwe haraka.
 

Ghiti Milimo

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
2,124
2,000
Tatizo lipo kwenu ambao hamjamwelewa mtoa mada he is true in disguise,anamsema makonda jinsi alivyokuwa akifanya mambo ya hovyo hadi akawafanya wana darisalam wote wadharaulike.
Wapo ambao hawajamuelewa! Povu linawatoka! Bado hawajaijua tu hii style ya P. Mayala!
 

MAFILILI

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,364
2,000
Huyu Kunenge ni Muislam hivyo ni mstaarabu anaongoza kama Allah anavyosema uwe na uadilifu kwa unaowaongoza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom