Rais mfano wa kuigwa duniani Watanzania tungepata mfano wake tuishi maisha azizi yaliyojaa neema.

nuna mtu kaniuliza unamuona je huyu wa kwetu?ndo nikamjibu.

Angalia hapa chini tumetokea wapi kisha ujitutumue kwa hoja nzito kumtetea kikwete nitakuelewa, jenga hoja acha majibu ya kisiasa mkuu.

quote_icon.png
By betlehem mimi naona anafaa kuigwa duniani kwa jinsi anavyoshughulikia migogoro mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.ni mtu mwenye uwezo wa kukabiliana na changamoto nzito bila kupaniki.

quote_icon.png
By adolay
migogoro ipi mkuu hebu agalia hapa chini halafu utoe ufafanuzi.

1. Richmond mpaka leo anakaa na kula nao

2. Kiwira coal mine mpaka leo anakaa na kula nao pamoja

3. Rada mpaka leo anakaa na kula nao pamoja

4. Iptl mpaka leo wanavuna kwa mkataba feki kwa kwenda mbele yeye hana habari

5. Rushwa ndani ya ccm makada wanalalama kila siku yeye haon kama huo ni mgogoro

6. Madaktari na haki ya malipo mazuri alitatua vipi huu mgogoro kwa kuwafukuza au huu sio mgogoro

7. Waalimu na haki ya malipo mazuri alitatua vipi kwa kutishia kuwapiga, kuwapeleka mahakani na kutishia kuwa fukuza kazi

8. Mgogoro wa mafuta ya petrol na diesel je mpaka sasa ametoa tamko gani kuhakikisha hatutarudia tena kwenye aibu ya kukosa mafuta

9. Mgogoro wa ubaguzi kidi upo wazi lakini inapofikia makanisa zaid ya 20 kuchomwa zanzibar amefikia wapi na nan nani wanahusika kama rais wa jamhuri ya tanzania.....

10. Mgogoro wa kidin chin kwa chin makanisa kadhaa yamechomwa tanzania bara amechukuwa hatua gan kutufanya kupendana

11. Anashughulikiaje mgogoro wa fedha za watanzania huko uswis kama rais wa inch

13. Anashughulikiage mgogoro wa wananchi maskini kukosa afya na elimu bora

kumbe wewe unaona kwa malyenge na kufikili kwa malyenge mkuu kama ilivo avata yako nilikuwa sijafahamu ati.

quote_icon.png
By betlehem

mgogoro wa watumishi wa serikali kugoma nchi nzima aliushughulikia ki diplomasia,mgogoro wa madakrari aliushughulikia ki diplomasia,chadema kumsusia bungeni na kumuwekea vikwazo vya kila aina,akawaalika ikulu, akawapa juice walivyotoka hapo wanajisikia wepesiiiii! Kuanzia hapo hadi sasa mambo safi! Na sasa hivi anashughulikia mgogoro wa mpaka na malawi katika hali ya utulivu kabisa.hana jazba huyu mzee!

quote_icon.png
By adolay
kama nilivosema siasa za mzaha ndizo zinafanya wakenya kilasiku watuone watanzania kasuku wa maneno. Umeongea nini sasa hapo juu, hebu soma alafu utafakali!

Kiwira coal mine ????

Richmond .......????

Chenge na vijisent vipi?

Rushwa ndani ya ccm na serikalin ????

Waalimu na madaktari??

Ukiona kiongozi wa nchi anasaidia nyumba ndogo kama ray c badala ya vikundi hajuwi wajibu wake kama kiongozi wa taifa.

nabii haheshimiki nyumbani kwake nyerere ni moja yakiongozi aneye heshimika sana duniani ,nimeongea na watu wengi wa mataifa ya nje kiongozi wa tanzania wengi wanaye mjua ni nyerere ijapokuwa enzi ya nyerere technologia ya mawasilano ilikuwa chini sana lakini wana mjua.
bas kumbe inawezekana viongozi wetu wanajitahidi.sisi tu ndo hatuthanimi mchango wao!
 
bas kumbe inawezekana viongozi wetu wanajitahidi.sisi tu ndo hatuthanimi mchango wao!

Umerudia kosa lilelile la majumuisho.

Huwezi kuniambia Mkapa na kikwe wapo kwenye kundi la kufaa, hapa nitakuomba pia utoe sababu au unahisi tu huna vigezo?
 
umerudia kosa lilelile la majumuisho.

Huwezi kuniambia Mkapa na Kikwete wapo kwenye kundi la kufaa, hapa nitakuomba pia utoe sababu au unahisi tu huna vigezo?
kwa hiyo kuanzia kwa Mkapa ndipo tulipopoteza muelekeo sio?
 
lakini nyerere alishindwa kuiletea maendeleo yeyote nchi yake!

Na alisema ukweli, kwamba pamoja na kuwa na madini na vingine kama hivyo ila hatuna wataalamu hivyo akapigania elimu bora, sasa wale wale aliowasomesha wametuachia magofu na mashimo, huku wakibadilisha nyimbo zake za ujamaa na ukombozi na kuwa nyimbo za rushwa, ufisadi n.k Wameuchimbia uzalendo kaburi na kuufufua udini, ukabila n.k
 
ila mimi kinachonishangaza ni kwamba leo hii watu wanoongoza kwa kuhujumu mali za umma ni wasomi na wengi wao wamesomeshwa bure! wengine ni wanasiasa wengine ni wataalam,na tatizo hili lipo karibu kila idara.hivi mzizi ni nini haswa?
 
kwa hiyo kuanzia kwa Mkapa ndipo tulipopoteza muelekeo sio?

Toa sababu kwanini wanafaa ukishindwa nitakusadia kwanini hawafai, si wewe ndo umesema wanafaa soma hapo chin

quote_icon.png
By betlehem

bas kumbe inawezekana viongozi wetu wanajitahidi.sisi tu ndo hatuthanimi mchango wao!
 
Toa sababu kwanini wanafaa ukishindwa nitakusadia kwanini hawafai, si wewe ndo umesema wanafaa soma hapo chin

quote_icon.png
By betlehem

bas kumbe inawezekana viongozi wetu wanajitahidi.sisi tu ndo hatuthanimi mchango wao!
nanafaa kwa sababu wamesaidia bado tuko kwenye amani kwa sasa,wamejenga barabara kibao,wamefungua shule kibao,wamefungua vyuo kibao,wameweka demokrasia ya kweli tanzania miongoni mwa mambo mengi waliofanya.
 
ila mimi kinachonishangaza ni kwamba leo hii watu wanoongoza kwa kuhujumu mali za umma ni wasomi na wengi wao wamesomeshwa bure! wengine ni wanasiasa wengine ni wataalam,na tatizo hili lipo karibu kila idara.hivi mzizi ni nini haswa?

Katika yote hapa mkuu umeuliza swali zuri sana, hakika sina majibu ya msingi kutoshereza bali nitatoa mtazamo wangu.

1. Katiba yetu ndio chimbuko la matatizo yote (hapa nawalaumu CCM kwa kuibeba na kuipigia upatu katiba yenye mianya mingi ya kupindisha haki na kuruhusu utawala wa kifalme) hatuna sera za kudumu kuonesha kila anaengia madarakani anapaswa kufuata moja, mbili, tatu, na akienda kinyume na hapo atawajibika kwa moja, mbili, tatu. Hivyo watawala wetu wanapoingia madarakani hujiona mungu mtu na kuamua vyovyote hata kama kuligharimu taifa mfano kuuza viwanada na nyumba za serikli bora wao wanapata 10% walalahoi watajijuwa.

2. Moja ya makosa makubwa nipale tulipoamua kuachana na azimio la Arusha

-Tukaacha uzalendo tukaamua kuuvaa ujasili wa kifisadi

-Tukaacha kila mtu afanye madudu yake bila kuwa na miongozo, china wanautaratibu wao haijalishi wewe ni nani ukikamatika umehujum au kula rushwa kitanzi hakikuepuki. (sisi hapa akina chenge na rada, kinana na meno ya tembo, Richmond na Lowasa hakuna tatizo wapo juu madarakani hakuna vipengere vya kuwabana) CCM wanabebana mpaka watia kichefuchefu

-Tukafungua njia kwa wawekezaji kuchota uchumi wetu bila kuwa na sera za kutuongoza tunafaidikaje,tukaingia kichwakichwa kunako soko huria bila kuweka misingi ya tunafanyaje, kwanini tufanye na kwa faida ya nani.

-Tumekuwa na wanasiasa matapeli hasa kuanzia kwa mkapa ambaye akauza kila kitu husan mashirika ya umma na viwanda kwa bei ya kupeana au ya bure.

-Ndugu yetu kikwete kwa sababu moja ama nyingine kaingia na jinamizi lake la udini, katuharibia kabisa inchi, watanzania hivi sasa tunatambuana na kupeana misaada kwa udin, ameshindwa kusahihisha makosa ya mkapa anaendekeza mfumo uleule wa majungu na fitina badala ya kuchukuwa hatua.

* wananchi wanalia rushwa na Rais analalama rushwa

* wananchi wanalia ufisad na yeye analalama ufisadi

* wanchi wanalia afya mbovu nayeye nalalama serikali haina uwezo
.
.
.
hayo ni machache na ukweli unabakia palepale ccm wanawajibika kubeba lawama zote za kwnini tunaviongozi wa ovyo wanaongoza ovyo nakutufanya kubakia maskini miaka 50 tangu uhuru japokuwa tuna raslimali lukuki kila kona ya Tanzania.
 
ila mimi kinachonishangaza ni kwamba leo hii watu wanoongoza kwa kuhujumu mali za umma ni wasomi na wengi wao wamesomeshwa bure! wengine ni wanasiasa wengine ni wataalam,na tatizo hili lipo karibu kila idara.hivi mzizi ni nini haswa?

Ckukua mataifa ya Ulaya na Amerika wananchi wana Uzalendo ulitukuka.....Afrika hasa Tz tumepoteza kabisa Uzalendo ndio maana Madaktari/Wauguzi/Waalimu/Waajiriwa wengine hawafuati kabisa miiko ya kazi zao, sasa siasa imekuwa kama LULU kila mtu anaitaka iwe ni halali au la, hata kwa gharamu ya uhai wa binadamu watu wanataka uongozi...Turudie misingi ya uzalendo, viongozi watende haki kwa wananchi wawe sehemu ya watawaliwa tofauti na sasa ukiwa na pesa unapewa nafasi ya kuamua kwa niaba ya walio wengi, wananchi waheshimu dola bila kinyongo na visasi, hapa mkuu pana shida kama hiyo dola imetenda haki kuwa hapo ilipo....Tuache propaganda za Udini,i.e mimi mkristu/muislam wengine hawana maana, dini sio kipimo cha wema kwa wenzetu..Ukabila sisi wa......tuna kila kitu hawa wa..... ni wajinga/wapumbavu/wachawi/wahuni n.k, kabila halijengi au kuleta nafsi ya mtu kila nafsi imeumbwa tofauti. Mimi nina kazi zangu nimeawaajira watu kutoka kila pembe ya Tz na dini tofauti ila wenye vigezo stahiki, jaribu kufuatilia makampuni mengi binafsi utapata jibu la ukabila na udini..ni hayo tu mkuu
 
mkuu umemwaga dhahabu humu jamvini.tungekuwa na watanzania wakutosha wenye hoja nzito na fikra dhabithi kiasi hiki baada ya muda mfupi tungefanya jambo.
 
Fideli castro or gadafi hawakutaka habari ya kunyenyekea nchi zilizoendelea ili wapate msaada bali walisimamia rasilimali zao ipasavyo na wananchi wakapata kuzifaidi, pia gadaifi alipigania umoja wa afrika ili tupate kuuziana rasilimali zetu wenyewe bila kuzitegemea nchi nyingine toka mabara mengine ambazo sasa zinajichukulia rasilimali zetu kwa bei ya kutupwa
 
Back
Top Bottom