jyfranca
JF-Expert Member
- Oct 3, 2010
- 297
- 8
Rais ametangaza Baraza lake la Mawaziri, kama kawaida ya watu wengi wanachojua ni kumsifia tuu bila kumkosoa. Uchaguzi huu tumeona kura za Rais zimepungua zaidi ya asilimia 20 na bado Rais hajaelewa kuwa wananchi hawaridhiki na utendaji wake. Kaunda baraza kubwa kama kawaida yake. Baadhi ya Wizara hazina maana yoyote na zilipaswa ziunganishwe.
Mapendekezo yangu ni kama ifuatavyo;
1. Kuliko kuwa na mawaziri watatu Ofisi ya Rais angebaki mmoja
2.Pawe na waziri mmoja ofisi ya makamu wa Rais badala ya wawili
3.Ofisi ya waziri mkuu iwe na waziri mmoja badala ya watatu wa sasa, pabakiwe na waziri wa TAMISEMI tuu.
4.Wizara ya Uchukuzi na Ujenzi iwe moja
5.Wizara ya mahusiano ya Afrika Mashariki irudi ndania ya Wizara ya Mambo ya nje.
6.Wizara ya maji irudi kwenye wizara ya chakula
Hapo Rais angeweza kupunguza wizara 8 kwa haraka, pia wizara nyingi hazihitaji manaibu waziri.
Tusiogope kuikosoa serikali, mambo ya kupongezana kila siku yanawaumiza walipa kodi