Rais Mama Samia, anatoa hotuba bila matusi wala kufoka hovyo, huu ndio uongozi

Napenda mama anavyofanya ila na wasiwasi.
Ustaarabu wa Raisi Samia utafanya kazi kama anao waambia na kuwaongoza pia ni wastaarabu. La sivyo watampanda mpaka kichwani.

Ni hivi, ukiwa kwenye kundi la wastaarabu wakati na wewe ni mstaarabu mambo yataenda, lakini ukiwa wewe ni mstaarabu katika kundi la washenzi watakupanda kichwani.

Sasa viongozi wetu na sisi wananchi ni wastaarabu?

Tusubiri tuone.
ameshasema atakuwa anapima mabega, yakinyanyuka tu...anakula kichwa.
 
Hakika!

Mama yetu huyu ni kiongozi na uwasilishaji wa hotuba anautendea haki sana.

Kwenye hotuba zake hatukani wala hafoki hovyo

Tunahitaji viongozi wa namna hii wenye uwezo wa kutoa hotuba zikaeleweka kwa njia nyepesi tena hata bila kutoa mifano ya ngono, Hongera Rais Wetu.
Ametenda vyema,hakuna "tumsifu yesu kristo"Wala asalaam aleikum,
Yeye kawasalimia kwa jina la "jamhuri ya muungano"
Raisi ametisha imethibitika hakuwa anapenda mambo ya hovyo ya Maghu,kwa kumtoa Kabudi mambo ya nje,pili kuiambia Wizara ya fedha,iache kutumia maguvu kutafuta pesa,badala yake itumie akili.
 
Kweli ukiwa na Kiu hata maji ya tope yataonekana matamu kama asali....

Yaani vitu basic vishakuwa vya ajabu kutokana na kile kilichotoka (Yaani Matusi au Kufoka inapaswa isiwe hata an extra quality but a given...)
 
Mama unavutiwa kusikia hotuba zake kwakweli hauhitaji kufoka ili uonekane mtendaji bora bali coordination na Hekima ya hali ya juu, ndio utaheshimika.
 
Back
Top Bottom