Rais Magufulli hawazii tena kuleta maendeleo ya Nchi ya Tanzania

Huwez ukamjaji rais huyu aliyekaa madarakani miaka minne na wale waliokaa miaka 10, Huwezi. Ndani ya miaka minne watoto wamasoma kwa elimu bure toka primary mpaka kidato cha nne. Asilimia kubwa ya wenye sifa hupata mikopo elimu ya juu. Nidhamu serikalini imerejea... yale mambo ya unanijua mimi nani hayapo.

Sijajua kuhusu uelewa wako na elimu yako, achilia mbali capacity yako ya kufikiri. Kuondoa umasikini kwenye nchi ambayo unoko wa diamond na wema ndio priority kuliko kutafuta pesa ni ngumu bro. Ni ngumu, ni ngumu sana. Asilimia kubwa ya watanzania hawafanyi kazi, wapo kwenye vijiwe vya kahawa, wapo kwa ndugu zao wanasubir ugali wa kengele. Siku hizi mtu anamiliki simu ya laki mbili aingie insta na hajawahi kufuga kuku wanaozwa 5000,

Nchi hii ni masikini na kuondoa umasikini ni suala mtambuka, hapa ndipo viongozi wanapopishana wapi pa kuanzia...

Mchukue lowasa awe rais, mbowe waziri mkuu na zitto kabwe waziri wa fedha muone kama baada ya miaka minne mtakua matajiri...
Wajinga km nyie ndo mmebaki kumuimbia mapambio......Uongoz waķe umepoteza muelekeo hauna matumain yoyote kwa watu wote
 
Hapo kwenye upendeleo wa uteuzi umeongea la msingi sana.
Ni makosa kuwasideline watu wa Taifa lako lile lile kwa sababu za UDINI, UKABILA, UKANDA etc. Nchi hii huwezi kuwa raisi wa dini fulani au kabila fulani au kanda fulani halafu ukadhani eti kwa kulipa privilege kundi moja dhidi ya jingine basi hilo ulilolipendelea litaleta maendeleo kwa niaba ya wote!. Hilo haliwezekani!
 
Akiwa Waziri katika awamu mbali mbali alikuwa ni mwana CCM na waziri anayefanya kazi na utendaji wake ulikuwa juu kuliko mtanzania yeyote aliyekuwa katika uongozi au sekta yeyote ile ya serikali, Utendaji wake ulikuwa mkubwa kuliko hata madaraka aliyo nayo, maono yake yaliona mbali kuvuka mipaka mpaka kuweza kuwashtua wengi waliosinzia katika sekta zao, utendaji wake wa kazi ulitukuka mpaka kuzitongoza akili za watanzania na wanaoipendea mazuri kutanzania kuanza kumfikiria katika ngazi ya juu ya uongozi wa Taifa hili ikiwemo urais uwaziri mkuu,

Bahati mbaya urais wa Tanzania una kasumba moja chafu. Huwa hauendi kwenye mikono ya mwanaume ambaye anaonekana kuwa mtendaji kazi mara zote uangukia mikononi mwa waliotengeneza mtandao na propaganda , kama tulivyoona kwa Rais Kikwete na awamu ya tatu bila mwalimu kuingilia ingeangukia kwa Kikwete au Lowassa,. Baada ya kukosa mtu mtaka maendeleo wa maana kwa muda mrefu watanzania wakaanza kufuata Magufuli kumuomba afanye hivyo awe mgombea akiwemo Kardinali Pengo, na Kitwanga, bila kumsahahu Mzee Mukama , wakidhani kwamba huyu akishika nchi itakuwa imepata mtu safi,

Uchukuaji wake form ya kugombea urais uliisisimua Nchi nzima na pengine watanzania wengi tuliokuwa nje ya Tanzania yaan kwenye dunia. Wengi waliamini amekuja na jeneza litalotumika kuisitiri maiti ya umaarufu wa Lowassa na Membe. Viumbe ambao mpaka muda huu ninapoiandika hii makala. Tanzania imegoma kusadiki kama kuna mtu amesha ondoa uchafu na makundi waliyotengeneza kwenye safu ya siasa, mbali zaid anastahili kuwa juu yao kwa umaarufu ambao wameupata kupitia ufisadi na ubadhilifu wa mali za Umma

Wakati CCM ilipotengeneza ule mpango wa kumpitisha Magufuli chini ya mipango ya kina Ben Mkapa na wengine. ambao ulisababisha muungano wa vyama pinzani, uiitazame CCM ya Magufuli kama mlango wa kuzimu, yaan ushindi ulikuwa lazima na wapinzani wakabaki kumung'unya maneno juu ya nani hasa awe mwakilishi wao. Magufuli alikuwa kwenye kiwango bora mno wakati kulinganisha na mtu yeyote kwa wakati ule. Uchaguzi mkuu wa 2015 CCM ilibeba dhamana ya kuliongoza Taifa tena kupitia kwa Magufuli ambaye alinasibishwa jina la TINGA TINGA kutokana na utendaji wake kazi.

Baada ya kuapishwa alianza moja kwa moja kazi siku hiyo hiyo akiwa na shamla shamla na mbwembwe za kuinyoosha Tanzania ambayo Kikwete na Mkapa wameacha wameikunja kunja kama shati liliotafunwa na ndama, akaanzia hazina , akaenda Muhimbili, akaenda bandarini kwa ziara zake za kushtukiza, haja kaa sawa akaenda ziara maalumu uwanja wa ndege kabla ya kumtetemesha Beno Ndulu pale Benki kuu kama mtoto mdogo baada ya kuyagundua madudu waloiyokuwa wanafanya,
Tukumbuke hotuba yake yenye weledi pale dodoma ya kulifungua bunge la JMT ambapo hakuwa anasoma popote na jina maarufu la JIPU lilianzia hapo , watanzania wenye matumaini na ahadi za makaratasi wa kule namtumbo, namanyele, kibaigwa, Kakonko, KIbaha picha ya ndege na kilwa kivinje waliisikiliza ile hotuba wengine kupitia kwa majirani wenye luninga na wengine wenye redio za betri kwakuwa hakukuwa na umeme,

Huu ulikuwa ni wakati ambao Magufuli alipambana kuichumbia akili ya watanzania kumkubali. Lakini mwisho wa siku watanzania taratibu wakaanza kushangaa kwanini wanayemtegemea ndo anawafunga akina Lema miezi nenda rudi bila dhamana? huyu huyu ndo anaanza kuingilia sheria za bunge? watanzania wanaoona mbali wakaishia kupiga alama ya msalaba kwamba uwenda hatukumjua kiundani au hatukuchunguza vya kutosha.

Ndoto ambayo muda uligoma kuigeuza iwe simulizi ya kweli kwenye ubongo wa Magufuli na watanzania . Kila mwaka, mfumo wa calendar ulitimiza wajibu wa kuongeza namba kwenye idadi ya miaka ambayo Magufuli kaongoza nchi Lakini kadri miaka ilivyokuwa ikisogea. Ndivyo matumaini ya watanzania waliokuwa na matumaini makubwa na ahadi kama milion 50 kwa kila kijiji, mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuiu, mfumo wa hela , na kuyakabili mafisadi kama Lugumi, watu wa Escrow , Richmond na uuzwaji wa nyumba za serikali kiholela yalipungua na kuanza kupoteza imani taratibu na wale watetezi wake mtandaoni wakaanza kujiuliza hivi huyo ndo yule yule au pale Ikulu kuna mzimu wa kuwabadili walazendo kuwa wamagendo?

Magufuli alipoona hajui siku wala saa atayoshuhudia umasikini wa watanzania ukimalizika kuishi chini ya dollar. Akaamua kufanya maamuzi magumu. Maamuzi ambayo kwa sasa yameulaza ubongo wake ndani ya sayari ya majuto." ni kubana kabisa wakosoaji wake ili kuficha madhaifu ya serikali yake na saa nyingine kuwanyamazisha kwa nguvu wale wote ambao walionekana kujua baadhi ya mambo kuwa hayaendi, na kweli vyombo vya habari na wanaharakati wamenyamazishwa vya kutosha , tumeshuhudia sana wengi wanayajua,



Yaan wale wale waliomfanya Magufuli kupokelewa kama mfalme . Watu wa jiji la Dar e salaam na kanda ya ziwa waliyo mlaki kwa nderemo, shangwe na vifijo. Waliamini yeye ametangulia, viwanda , kukomesha wezi na maendeleo ya watanzania vinamfuata nyuma. Mashabiki wa CCM na watanzania wa kawaida hawakujua hii ilikuwa ndoto ya kufikirika. Iliyozaliwa kwenye usingizi wa mwendawazimu.

Maisha ya watanzania ndani ya uongozi wa Magufuli yamekuwa tofauti kabisa na picha aliyokuwa anaitengeneza vichwani mwao. Muda umetoa hukumu ya haki hadharani. Kwamba aliitenda dhambi ya kuwaona waliotangullia hawakufanya kitu yeye ndo bora, kwamba waliopita ni wazembe yeye tu ndo kila kitu, kwamba mawazo ya wapinzani yote ni ovyo isipokuwa ya CCM aliyo ya dictate yeye mwenyewe , hii inamfanya kuonekana kama mwanafunzi aliyeomba mwalimu ajiache ajisomee mwenyewe na kuingia kwenye mtihani akakuta kumbe kuna mambo mengi mwalimu wake alikuwa hajamfundisha na mbaya zaid alishamtambia kwamba mwalimu wake hakujua kufundisha, na ana aibu ya kumuuliza maswali au msaada kwa ajili ya paper two,

Leo anauguza majeraha huku taswira ya kuumiza ikimrudia mara kwa mara. Analia Moyoni kila anapotazama, tamanio na ndoto za kuifanya Tanzania ya viwanda wakati umeme hautoshi, wawekezaji wanakimbia, watanzania hawawez hata kufinyanga hata vyumgu walivyofinyanga mababu kisa elimu haiwasaidii chochote kwenye ilo, hizi ndot za kuumaliza umasikini wa watanzania na matumaini vilivyomfia akiwa ameusitiri mwili wake kwa jezi zenye nembo ya CCM na cheti cha urais wa awamu ya tano akiishia kuushika upala wake pale ikulu kila aitazamapo picha ya mwalimu Nyerere ukutani na kuwaza kwamba wenda alikosea pia kuwaruhusu wapambe wanafiki kumfananisha naye.

na anajiulaumu alipofikiri anaenda magogoni kutengeneza bomu la kuwapoteza wale wote ambao alidhani ndo wakwamisha maendeleo ya watanzania..Hakuwa kwenye utimamu wake kifikra kama tunavyomjua. waliomdanganya jinsi ya kuanza uongozi waliuathiri na kuuharibu mfumo wake wakufikiri kiufasaha.

Leo CCM ina wanaoamini kichwa labda cha mwingine ndani yao kina msaada kuliko maamuzi ya kutonagalia mbele sana ya Magufulir. Magufuli ameonyesha wazi, mgongo wake hauna mifupa iliyokomaa kiasi cha kuweza kuibeba Tanzania muda inapohitaji msaada wake kuwaletea maendeleo na kutokomeza umasikini.

Na hizi makala zinazotoka kwa wakubwa zinazo muandama kila leo. Zinashawishi dunia iamini wazi, Magufuli hana tena ubongo wenye D.N.A ya maendeleo kwa watanzania. Watu pekee waliobaki na imani juu ya Magufuli ni watu wa aina tatu. wenye ulaji ndani yake, wenye ukoo naye na wale ambao ni CCM kindaki ndaki wasioweza kung'amua mambo,

Wengine tunadhani Magufuli ataweza kama atakubali kushauriwa na kuwa mnyenyekevu sana kwa wanaomzunguka asiwatengenezee nidhamu ya uoga, na kufikia hatua kumshauri vibaya, tunaamini ataweza kama ataacha kaupendeleo fulani wanakomtuhumu nako kwenye teuzi , tunamaamini ataweza kama atakubali kuwaheshimu waliomtangulia na kuuthamini mchango wao kwenye Taifa hili, Tunaamini atafanikiwa kama ataruhusu mawazo mbadala ya wapinzani wake nayo akayapinga kwa hoja si kwa mtutu au vyombo vya dola, tunaamini Mzee wetu ataweza kama ataamua kukubali kwamba si kila kitu yeye yuko sahihi, Tunaamini ataweza kama ataacha Double standard kwenye kuwawajibisha baadhi ya watendaji aliowateua, Tunaamini ataweza kama ataweza kuwakemea hata wale wanaojipendekeza kwake kuanzisha mambo kwenye jimbo lake bila kufuata utaratibu na mipango miji kama vile jinsi ya kuanzisha internationala airport , Mbuga na sehem za hifadhi za Taifa, Tunaamini ataweza kama atazitambua sekta binafsi bila kuwakomoa wawekezaji kutoka moyoni siyo mdomoni

Jamani naishia hapa siku hizi mi mzembe kuandika,

View attachment 1134641

Britanicca encyclopedia
Bado hujaandika
 
 
Pascal Mayalla na Jakasaye hili la kardinali pengo mtujuze
Huu ni uongo tuu wa Britanica,
hoja kuwa Magufuli hawazii tena kuleta maendeleo haina mashiko, kwa sababu Magufuli mwenyewe ndio maendeleo, sasa awaze nini?

Kuhusu Magufuli alikoibukia, ukweli ni huu
P
 
Wajinga km nyie ndo mmebaki kumuimbia mapambio......Uongoz waķe umepoteza muelekeo hauna matumain yoyote kwa watu wote
Pumbavu wewe, nchi inajenga standard gauge kuboost mizigo bandarini. Nchi inajenga stigliers gorge kusambaza umeme wa uhakika, elimu ni bure. Miradi yote ipo inajengwa, unafikiri maendeleo yanakuja siku moja??
 
Wakati mwingine kwenye mbio lazima ujue unakimbiaje ili uje kushinda hizo mbio..

Boxing inahitaji discipline kwa adui yako uweze kumshinda..

Fooball inahitaji pia discipline na kujifunza wakati mchezo unaendelea ili ujue mbinu gani uitumie ili usinde..

Kabla mechi haijaanza lazima umjue adui na umpangie mbinu za kimkakati umshinde, mbinu ulizoingiza nazo zikigoma inabidi uwe mwepesi wa kumuelewa adui ili ubadili mbinu huku mechi ikiendelea.
 
Back
Top Bottom